Umoja wa Vijana wa Vyama vya Siasa vya Upinzani nchini umemtumia salamu za pole Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mumewe, Marehemu Hafidh Ameir Hassan.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Umoja huo, Masoud Mombo, amesema msiba huo umewakumbusha kuwa tofauti za kisiasa na kiitikadi hazipaswi kuondoa ubinadamu.
Mombo amesema katika kipindi hiki wanamwona Dkt. Samia kwanza kama mama aliyepoteza mwenza wa maisha, hivyo wametoa pole na kuungana naye katika kipindi hicho kigumu cha maombolezo.