Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda amekabidhi Lori tatu za vifaa vya Msaada kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe Queen Sendiga ikiwa ni muendelezo utoaji wa misaada kwa watu waliopata majanga.
Akizungumza Mara baada ya kukabidhi Misaada hiyo Mwenyekiti Chatanda amesema msaada huo ni Muendelezo wa ahadi waliyotoa Kusaidia watu waliopatwa na Maafa ya Mafuriko Hanang kama Mashuka 2000, Khanga 400, balo za Nguo, taulo za kike, Shuka za Kimasai, Vikombe 1440 na Vifaa mbalimbali.
"Mimi kama Mwenyekiti wa wanawake Tanzania kwa Kushirikiana na Makamu wangu na wanawake wote tutaendelea kuleta misaada mbalimbali ili kuweza kuwafariji wananchi wetu wa Manyara.
#UWTImara #JeshiLaMama #KaziIendelee