Inategemea mnataka kuwa na watoto wangapi. (Mtizamo wangu tu, watoto wawili watatu wanatosha ili kupata muda na nafasi ya kulea na kuhangaikia maisha, sio mnazaaa tu mpaka uzeeni. Mkizaa mapema, mnapumzika mapema. Watoto wenu wanakuwa na kufikia umri wa kujitegemea mkiwa bado hamjazeeka kabisa).
Watoto wakiwa hawakupishana sana umri (kati ya miaka 2 na 3), inakuwa rahisi katika malezi kwani huduma zao zinalingana, mnakuwa mnatatua mataatizo na mahitaji mawili kwa wakati mmoja: vyakula, mavazi, elimu, afya...michezo n.k.
Kuhusu umri mzuri wa kupata watoto, ni kati ya miaka 25 na 35. Mara nyengine inaweza kushuka hadi 20 kwa mwanamke na kupanda hadi 40 kwa mwanamume. Chini au zaidi ya umri huo ni hatari kwa afya, sio ya mama tu bali hata malezi yanakuwa tabu kidogo. Fikiria mnazaa na 45, mtoto wenu wa kwanza akifika 20 nyinyi mko above 60. Jaribuni tafauti kati yenu na watoto isizidi miaka 25, mfano, wewe uko na 40 mtoto yuko 15.