Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Huu ndio umri wa watu wengi wa lala salama katika mahusiano ya kufa na kuzikana.
Kama umefikisha huo umri,na mahusiano yako hayaeleweki eleweki, chukua hatua mapema.
Kama ni mwanamke, na una kipato na hujapata mtu wa kueleweka, tafuta mwanaume yeyote choka mbaya ambaye atakuheshimisha na kukupa faraja huko tuendako; awe karibu na wewe utakapoanza kukutana na changamoto za uchakavu wa viungo vya mwili, maradhi n.k
Kama umeolewa,na unaona kabisa ndoa yako haitakuwa na manufaa pale uchakavu wa mwili utakapotokea, nakushauri uipige chini ukatafute wa kufanana na wewe ata asiyekuwa na kipato; kwa sababu huko tunakoelekea utu unahitajika zaidi kuliko pesa.
Kama ni mwanaume na huna mahusiano ya kueleweka, tafuta mwanamke yeyote bila kuangalia sura, muonekano wala kipato, tafuta mwenye utu muanze kusindikizana kwenye nyakati zako za mwisho wa hapa duniani.
Kama umeoa, na bado unaona chenga chenga; piga chini na utafute mtu sahihi mwenye utu; huko tuelekeapo tunahitaji faraja ya utu zaidi kuliko muonekano wa sura na shepu.
Pia kumbuka, katika umri huo wewe ndio baba na ndio mama; baba yako na mama yako waliokuzaa watakuwa choka mbaya kwa uzee na hawatakuwa na msaada mkubwa na wewe; kwa hiyo ile kauli ya kusema nitakimbilia kwa baba au mama, hiyo inakuwa haipo.
Hapo ndipo ile kauli inakuja; ''asiyefunzwa na mamaye........''
Kwa leo ni hayo tu.