TheMaster
Member
- Aug 10, 2023
- 36
- 68
Nimesikiliza hotuba yote ya Ndugu Mwenyekiti F A. Mbowe. Pamoja na mambo mengi ya kushangaza katika hotuba ile ikiwemo kuonekana Mwenyekiti amekamia kukomoana, lakini binafsi nimeshtushwa sana na kauli yake ya kusema anataka amalizie ngwe yake ya mwisho kwasababu hadi sasa ana miaka 63, hivyo akimalizia mitano ijayo atakuwa na miaka 68.
Huku akitanabahisha wazi kabisa kuwa hata watangulizi wake Edwin Mtei alistaafu uwenyekiti akiwa na miaka 68 pia alomfuatia Mtei, Bob Makani nae alistaafu uwenyekiti akiwa na miaka 68.
Je, kustaafu uwenyekiti kwa umri wa miaka 68 ni kifungu ndani ya katiba ya chama au ni utaratibu ulokuwepo CHADEMA au ni Tamaa zake tu mwenyekiti?