Kuna watu wanaishi kwa maigizo. Anataka vazi kulingana na bei yake bila kujali uimara na unadhifu. Mwingine atataka vazi flani kisa kuna mtu fulani maarufu kavaa la aina ile. Ni kweli lakini kuna profession zinahitaji mavazi ya kipekee na yenye ubunifu wa hali ya juu kama vile waigizaji, wanamitindo na wanamuziki. lakini utakuta mtu labda ni mwalimu au mwanasiasa au ni mfanyabiashara basi ana complicate kwenye mavazi hadi anasahau kufuatilia mambo mengine, inafikia anasahau hadi majukumu yake.
Ila mimi sijui nikoje, sichaguagi kabisa mitindo wala siishobokei. ninachojali ni nguo safi, za heshima na zinazonisetiri. Amini usiamini...... hata nikikutana na mtu huwa siangalii kavaa namna gani au kavaa mtindo gani, labda awe uchi au nguo zake chafu ndio nitagundua. vinginevyo hata akiniuliza baada ya kuachana alikuwa kavaa nguo gani sitakumbuka.