SoC04 Umuhimu na nafasi ya waandishi wa habari uthaminiwe katika kuleta mabadiliko na kuifikia Tanzania tuitakayo

SoC04 Umuhimu na nafasi ya waandishi wa habari uthaminiwe katika kuleta mabadiliko na kuifikia Tanzania tuitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Jun 17, 2024
Posts
7
Reaction score
5
Sekta ya habari na mawasiliano ni sekta muhimu sana katika taifa lolote linalohitaji maendeleo. Kwa kuwa sekta hii inahusisha kukusanya taarifa mbalimbali,kuzichakata na kuzihariri na baadaye kuzitoa kwa watu(jamii) juu ya matukio mbalimbali. Mwandishi wa habari ni mtu anayefanya majukumu hayo kwa miiko ya taaluma ya uandishi wa habari. Serikali huwahitaji sana waandishi wa habari kwani ndio huwa wanasambaza masuala mbalimbali yanayolihusu taifa kupitia vyombo mbalimbali kama vile magazeti, redio, runinga na mitandao ya kijamii. Hivyo kurahisisha habari kuwafikia wananchi kwa wakati uliokusudiwa. Ipo wazi kwamba hii ni sekta yenye mchango mkubwa sana katika kuleta muunganiko baina ya serikali na wananchi wake, ni vema serikali na jamii kufanya mambo yafuatayo ili kuchochea tasinia ya habari na mawasiliano kufanya kazi kwa weredi,uhuru na misingi ya taaluma.

Kuboresha sera za habari na mawasiliano.
Sera za utoaji wa habari zikiwa zinawabana waandishi wandishi wa habari zitapelekea woga na upendeleo. Mfano sera ikisema mwandishi wa habari atakayefichua vitendo vya rushwa vinavyofanya na serikali basi afungwe jela. Haitakuwa sera rafiki kwa waandishi wa habari kufanya kazi yao kwa uhuru. Waandishi wa habari huibua hoja muhimu kuhusu udhaifu fulani,hali inayoweza kupelekea wahusika kurekebisha makosa yao mfano kiongozi kuhusishwa na rushwa.

Serikali itoe mikopo ya kuwezesha kununua vifaa bora vya kisasa.
Iko wazi habari huwa haziwi sehemu moja. Habari au matukio hutokea sehemu tofautitofauti. Waandishi wanahitaji usafiri kuyafikia maeneo yenye matukio, kamera za kisasa, nishati n.k. Hivyo vifaa hivyo vikipatikana kwa urahisi waandishi wataripoti taarifa kwa wakati mwafaka.

Zitungwe sheria zitakazowalinda wanahabari watakapofichua uovu na matukio mbalimbali.
Ikiwa sheria zitawabana waandishi wa habari haitaleta manufaa ya uwepo wao. Lakini ikiwa zitakuwa ni sheria zinazothamini mchango wa wanahabari na kuwapa uhuru wa kuripoti taarifa pasipo tu kuvunja sheria za nchi, hali hii itawapelekea kujiamini na kutoa taarifa muhimu kama za rushwa na ufisadi ambazo zingelisababishia taifa hasara. Hata baada ya kutoa taarifa wasichukuliwe hatua kwani hawakukiuka sheria za nchi.

Kuwe kunatolewa motisha kwa vyombo vya habari vinavyotoa habari zenye mchango chanya katika jamii pasipo upendeleo.
Kuna mambo mengi ya maana ambayo yanaweza kuibuliwa na vyombo habari na mambo hayo yakaleta hamasa kwa jamii katika kutenda. Mfano kukawa na midahalo mbalimbali inayowawezesha vijana kujiajiri, viongozi kutekeleza ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi. Au kuripoti matukio kama namna ya kulima zao fulani kutoa matukio ya kero za wananchi ili zishughulikiwe na viongozi n.k.

Kupunguza gharama za uzalishaji na utoaji wa maudhui.
Kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia gharama za upataji na utoaji wa taarifa unaweza kuwa gharama sana kutokana na kuhitaji intaneti,vifaa vya kisasa nk . Hivyo kupelekea kutumia gharama kupata taarifa na kuwasilisha pia. Hata hivyo hali hii inaweza pelekea taarifa zingine kutokurushwa kutokana na kuhitaji gharama zaidi. Ni vema kupunguza gharama kama za intaneti ili isiwe kikwazo wakati wa kutoa taarifa.

Serikali na jamii itoe ushirikiano wa kutosha kwa wanahabari katika kutoa taarifa sahihi katika matukio mbalimbali.
Mwandishi wa habari huhitaji watu ili apate taarifa inaweza kuwa kiongozi wa serikali au mtu ambaye alishuhudia tukio fulani au ni mhusika wa tukio fulani. Kushirikiana vema na wanahabari hurahisisha kutoa taarifa sahihi isiyo na kanganyiko kwa wasomaji,wasikilizaji na watazamaji. Ni vema kushirikiana kikamilifu kwa lugha nzuri ili kumrahisishia mwandishi kutekeleza majukumu kwa muda mwafaka na umakini.

Mwisho,sekta ya habari na mawasiliano imebeba sehemu kubwa ya mabadiliko ya taifa kuelekea maendeleo. Kwani hutoa habari za nini kinaendelea katika hatua mbalimbali za utendaji na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya serikali kwa wananchi. Serikali iwape nafasi ili mchango wa waandishi wa habari udhihirike katika taifa.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom