Juliana James
New Member
- Jul 13, 2021
- 2
- 1
Afya ni mtaji wa kwanza kwa kila mtu anayehitaji maendeleo yake binafsi na hata ya jamii na taifa lake. Afya ni mabadiliko ya uimara katika utendaji wa binadamu kimwili, kiakili na hata kiroho ili kuweza kuendana na changamoto katika mazingira yanayomzunguka.
Afya ya mwili inatusaidia katika mijongeo mbalimbali mfano kuweza kufanya shughuli anuai wakati afya ya akili n uwezo wa kuwa imara kifikra na mawazo kwa ujumla ikiwa ni kuweza kutatua changamoto zinazohitaji utulivu wa ubongo ili uweze kufanya maamuzi na uchaguzi sahihi katika mifumo ya maisha.
Na afya ya kiroho hii inahusisha uwezo wa binadamu kuweza kuyaishi matendo mema yanayopendeza lakini pia kuwa karibu na mungu ili kumuepusha mtu huyu na matendo hatarishi na yenye kuweza kuutia walakini utu wale.
Katika kuitunza afya ya kimwili ni muhimu kula vyakula vyenye virutubisho sahihi kwa uimara wa miili yetu,kunywa maji safi na salama ya kutosha kwani asilimia 75% ya miili yetu inaendeshwa na maji,kufanya mazoezi kwa ajili ya kuimarisha miili yetu lakini bila kusahau usafi wa mazingira yanayotuzunguka ili kujiepusha na magonjwa mbalimbali ambayo yanaweza kuathiri afya za miili yetu kama kipindupindu,kuhara na mengine kama hayo.
Kwa upande wa afya ya akili kama binadamu tunahitaji mapumziko ili kuupumzisha ubongo(kwa sababu ubongo ni kama mashine unahitaji kupumzishwa ili kuongeza ufanisi),pia kujiepusha na mambo yanayoweza kuleta athari za kuchosha akili kama vile msongo wa mawazo na sonona,tuwe na tabia ya kujifunza mambo mapya yatakayoulisha ubongo wetu vitu vya kutupatia ufanisi zaidi(kujisomea vitabu na majarida,kusafiri sehemu mbalimbali kujifunza mambo mapya nk).
Pia kufanya vile vitu tunavyovipenda kama kuimba kusikiliza muziki hii husaidia sana hasa nyakati ambapo unahisi afya ya akili yako inazorota.
Afya ya kiroho tunaitunza kwa kuwa karibu na mungu lakini tunaweza kujiuliza ni kwa vipi tuwe karibu na mungu?Hii ni kwa kutenda matendo mema yatakayofanyika baraka kwa wengine kama kusaidia wasiojiweza,kuchukuliana pamoja na madhaifu tuliyonayo kama wanadamu na pia kujifunza kusamehe pale tunapokosewa hii itasaidia katika kutunza afya siyo ya kiroho tu bali ata ya kimwili na kiakili itakuepusha na kuweka mambo mazito moyoni na akilin yanayoweza kukupelekea msongo wa mawazo na hata magonjwa kama presha na vidonda vya tumbo na mengine.
Zaidi sana tukumbuke kuwa afya bora ni kipengele cha kwanza cha maendeleo yako hutaweza kufanya kazi endapo afya yako haiko imara,pia kuna maeneo na nyanja ambazo ukiwa na matatizo ya kiafya huenda ni ya kimwili,kiakili au vinginevyo hutaweza kukidhi vigezo vya kuwepo katika nafasi iyo mfano kazi mbalimbali waajiri wanategemea kuajiri watu watakaokuwa na faida kwa kampuni au taasisi zao na siyo mizigo kwa taasisi ivyo ni muhimu kukinga na kutunza afya zetu ili tuwe imara nyakati zote.
Na pia kumuona daktari na kujifanyia uchunguzi wa kitabibu mara kwa mara hata kama kwa macho ya kawaida unajiona uko imara na mwenye afya yapo magonjwa yanayojipandikiza ndani yetu bila kuonyesha dalili za awali na endapo ukichelewa dalili zinapokuja kujitokeza tunakuwa tumekwishachelewa na tatizo linakuwa ni kubwa na linawezekana likagharimu kiuchumi na muda pia katika kujitibu mfano kansa,figo,homa ya ini na magonjwa mengine hatari kama hayo.
Kwa kumalizia niwakumbushe ndugu zangu afya yako mtaji wako.
Mawazo yangu binafsi.

Upvote
1