Umuhimu wa Ally Mshamu jina lake kupewa mtaa alioishi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
UMUHIMU WA ALLY MSHAM JINA LAKE KUPEWA MTAA ALIOISHI

Majina mengi ya mitaa imebadilishwa Dar es Salaam kwa sababu ya kuweka kumbukumbu za wapigania uhuru.

Pugu Road imebadilishwa jina na kuitwa Nyerere Road kwa kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwani alikuwa akipita njia ile wakati anasomesha Pugu kuja Dar es Salaam katika harakati za TANU.

Upanga Road ikabadilishwa jina sasa ni Barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

Bi. Titi kwa mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika kapewa mtaa uliokuwa ukijulikana kama Umoja wa Wanawake.

Bi. Tatu bint Mzee kapewa mtaa uliokuwa ukiitwa Kirk Street kisha Lindi sasa ni Mtaa wa Bi. Tatu bint Mzee.

Bi. Tatu bint Mzee ni katika wanawake wa mwanzo kujiunga na TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Omari London kapewa Mtaa uliokuwa unaitwa Somali.
Sheikh Yusuf Badi aliyekuwa mwanazuoni maarufu Lindi na mpigania uhuru kapewa mtaa.

Bi. Khadija Bint Kamba ana mtaa Ilala, Bungoni.

Mifano iko mingi sana.

Magomeni tumepata fursa ya kumwadhimisha shujaa wetu, mwana TANU, mzalendo na rafiki wa Nyerere na Mama Maria aliyejitolea nyumba yake kuwa tawi la TANU na kumfungulia Mama Maria duka la mafuta ya TAA katika kipindi kile kigumu cha kupambana na ukoloni wa Mwingereza.

Ikiwa sisi hatutachukua fursa hii kumuenzi Ali Msham mzee wetu huyu kwa mchango wake wa kuikomboa nchi hii kutoka ukoloni tutakuwa tumejidhulumu wenyewe.

Tunataka tuweke kibao kisomeke, "Mtaa wa Ali Msham."

Miaka 100 ijayo watakaokuwepo Magomeni hii watoto wao watawauliza wazazi wao, "Huyu Ali Msham ni nani?"

Mzazi anamjibu mwanae, "Ali Msham alikuwa mpigania uhuru wa Tanganyika na rafiki kipenzi wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na mkewe Mama Maria Nyerere na aliishi nyumba ile na pale ndipo lilipokuwa tawi la TANU."

Hapo mtoto kafunzwa uzalendo.

Mtoto atakuwa kasomeshwa historia ya Mwalimu Nyerere, historia ya nchi yetu na mashujaa wetu kwa njia nyepesi sana.

Ndugu zangu tusijidhulumu wenyewe kwa sisi wenyewe kujidharaulisha.

Ndugu zangu tusijiangamize kwa mikono yetu wenyewe.

Sisi tukijithamini na wengine watatuthamini.

Tusiipe nafasi hasad na wivu kuzuia kufanikiwa kwa jambo hili adhim.

Picha: Kulia wa kwanza ni Ali Msham na aliyekaa kwenye meza ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Siku hii Ali Msham alimwalika Mwalimu kwenye tawi lake la TANU Mtaa wa Jaribu amkabidhi zawadi ya samani alizomtengenezea pamoja na saa ya ukutani kwa ajili ofisi yake Rais wa TANU iliyokuwa New Street (sasa Lumumba Avenue).

Screenshot_20220330-175136_Photos.jpg
 
Babu yangu Rueben Mswia hajapewa mtaa mpaka leo.

Huyu alikuwa mwafrika wa mwanzo kumiliki gari.Akimkaribisha Mwl Nyerere na kuifadhili TANU kanda ya kaskazini.
 
View attachment 2169587
Muongo wewe Mzee. Kama ilivyo kila kitu unachozusha, maneno yanakuwa mengii., lakini kuna unafiki na maswali kibao nyuma yake. Waswahili wana msemo: "Tenda wema, Nenda zako": Wewe kama nani leo hii kuanza kudai thawabu za marehemu unayedai apewe jina la mtaa? Mlikuwa wapi wakati Nyerere bado yu hai, au hata warithi wake tokea Mwinyi hadi huyu mama wa sasa?
 
Nadhani Kuna haja ya historia ya nchi yetu kuandikwa kwa usahihi na kufundishwa mashuleni...

Vyuo vikuu, TEA, TIE, Mamlaka ya hifadhi ya kumbukumbu [National Archives].....

Historia ya Tanzania is the most controversial, disputed and infamous to a certain sect of the population....

Ni wakati sasa kuwa kipaumbele na kuwekwa sawa
 
sawa...ni wazo zuri lakininje?? kila mpigania uhuru apewe jina??
 
Bol...
Huwezi "kila" ila hapa katika zoezi hili la anuani za makazi wametoa fursa kwa kubadili majina ya mitaa.

Hapa Magomeni Mtaa wa Jaribu ndipo ilipokuwa tawi la kwanza la TANU alilofungua Ali Msham.

Mimi nimependekeza kwa wakazi wa Magomeni wabadili jina la Jaribu liwe Ali Msham.

Soma historia yake ipo hapa JF.
 
Back
Top Bottom