SoC01 Umuhimu wa Ardhi kwako kijana

SoC01 Umuhimu wa Ardhi kwako kijana

Stories of Change - 2021 Competition

Filbert FD

New Member
Joined
Dec 12, 2014
Posts
1
Reaction score
8
Umuhimu wa Ardhi kwako kijana:

Salaam ndugu wana jukwaa la “Stries of change”. Ujumbe wangu wa leo kwenu wana jukwaa utabeba “story” ihusuyo ARDHI. Jukwaani hapa nitajikita Umuhimu wa ardhi, upatikanaji wake, mambo ya kuzingatia katika mchakato wa umiliki wa ardhi na mwisho nitatoa sababu za kijana wa kitanzania kumiiki ardhi mapema.

Ndugu wana jukwaa, Mwaimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema kwamba ili tuendelee tunahitaji Watu, Ardhi, Uongzi bora na Siasa safi. Kwa msisitizo wangu katika Ardhi, hii inaonesha ni kwa namna gani Ardhi ni moja ya Nguzo muhimu sana katika maendeleo ya kila mmoja wetu na Taifa kwa uumla.

Umuhimu wa Ardhi.

Moja, Ardhi ni moja ya misingi ya uzalishaji mali katika uchumi wa mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. Mtu mmoja aliwahi kusema, Mali ipo shambani akiaribu kurejelea umuhimu wa kilimo ambacho kwa hakika hufanyika katika Ardhi. Wachimba madini nao huyachimba madini kutoka katika ardhi.

Pili, Ardhi hushikiria sekta ya usafirishaji kwa maana kuu kwamba barabara, reli, gati za kuegesha meli, viwanja vya ndege vyote hujengwa juu ya Ardhi na hivyo kurahisisha usafirishaji sana.

Tatu, Ardhi ni makazi ya viumbe hai vingine ambavyo ni muhimu sana katika kuwezesha urahisi wa Maisha, uhusiano na iklojia kwa ujumla wake.

Kwa ujumla wake Ardhi ni kiunganishi kikuu cha kuwezesha Maisha duniani kuwezekana na kuendelea kuwepo.

Upatikanaji wa Ardhi.

Watanzania wengi wanamiliki ardhi kwa kadri waivyoweza kupata na wengine wengi hawajapata fursa ya kumiiki kipande cha ardhi japo kidogo richa ya njia za upatikanaji wake kuwa rahisi na wazi kabisa. Kama mtanzania anayo haki ya kumiliki ardhi sehemu yoyote nchini Tanzania ilimradi anafuata taratibu na mingozo iiyopo. Njia kadhaa za upatikanaji wa Ardhi.

  • Asili: Kwamba mtanzania ataweza kupata Ardhi kwa njia ya asili tu, kutokana na kuzaliwa eneo Fulani na kuendeleza kiwango cha ardhi kwa shughuli za kila siku hasa kilimo na kutengeneza mipaka ya asili ya eneo na kutambuliwa kuwa ni lake na majirani zake Pamoja na uongozi wa eneo husika. Maeneo ya namna hii huwa ni ya vijiini.
  • Urithi: Njia nyingine ya upatikanaji wa ardhi ni kupitia kurithi ardhi iliyoachwa na mmiiki wa awali baada ya kufariki. Hii huzingatia taratibu zilizopo za mirathi an wosia uliachwa na aliyefariki.
  • Zawadi: Njia nyingine ya upatikanaji wa ardhi ni kupitia kutoa au kupewa zawadi ya ardhi. Mara nyingi wazazi huwazawadia Watoto wao au watu hutoa zawadi ya ardhi kwa wawapendao na kufurahishwa nao. Mfano ni kama alichowahi kufanya aliyewahi kuwa rais wa Tanzania maheremu John Pombe Magufuri kwa kuwapa viwanja vijana kadhaa walifanya vizuri katika michezo mbalimbali Kimataifa, Bondia Mwakinyo akiwa miongoni mwao.
  • Kununua: Njia hii ndio maarufu sana na hutumiwa na wengi ktika kujipatia ardhi. Mhitaji humlipa muuzaji wa ardhi kiasi cha pesa ilia pate kumiliki kipande cha ardhi. Wachache hujua mambo ya kuzingatia katika mchakato wa kununua ardhi na wengine wameishia kwenye migogoro ya ardhi kwa sababu hiyo.


Mambo muhimu ya kuzingatia katika mchakato wa kununua Ardhi:

Ndugu wana jukwaa, ni ukweli wa wazi kabisa kwamba sehemu mbalimbali za nchi yetu imekuwepo migogoro mingi sana ya ardhi, na hivyo kusababisha madhara mengi sana kwa jamii na Taifa kwa ujumla. Migogoro ya ardhi imesababisha chuki, vifo na kuzorota kwa maendeleo ya jamii na Taifa pia kwa kushindwa kuzalisha na kutenga muda na pesa kutatua migogoro ya ardhi nchini.

Kwa mujibu wa hotuba ya Waziri wa wizara ya ardhi, Nyumba na makazi bunge la bajeti mwaka huu 2021 alisema takribani Mashauri 49,638 kero za ardhi ziliripotiwa kwa ajili ya kuamuliwa, mengi yakiwa ni migogoro ya adhi. Hivyo ili kuendelea kutokommeza migogoro ya ardhi ni muhimu kujua mambo kadhaa ya kuzingatia hasa wakati wa kununua ardhi.

  • Hakikisha ardhi imepimwa; ardhi iliyopimwa na yenye ramani ya upimaji iliyoidhinishwa na mamlaka husika hukupa uhakika wa matumizi ya ardhi husika hivyo kuepuka kuchanganaya matumizi ya ardhi, kama ni makazi, bishara, viwanda au shamba, au ni eneo la umma au la wazi
  • Fahamu mmiiki wa ardhi halisi; kwa kumfahamu mmiliki halisi hupunguza utapeli wa kidalali wa kuuziwa enneo ambalo lilishauzwa tayari au ambalo hauzwi kabisa.
  • Fahamu mipango ya serikali ya baadae; kwa kufahamu mipango ya baadae ya serikali kwa ardhi au eneo hilo hupunguza sintofahamu itakapotokea kuhamishwa kwa ajili ya maendeleo ya ujumla.
  • Bei sahihi; bei sahihi husaidia kufanya maamuzi kwa mnunuzi na hivyo kutouziwa kwa bei ya juu sana ambayo huweza kusababisha pia migongano kuhusu umilikishwaji. Bei ya ardhi huamuliwa na mambo kadhaa kama vile;
  • Bei elekezi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na makazi
  • Aina ya upimaji , je ni makazi, biashara au viwanda, kama makazi ni makazi ya kati, ya kubanana au ya nafasi?
  • Hali ya maendeleo ya maeneo husika
  • Bei ya soko
  • Uhitaji, kama muuzaji anashida na pes asana anaweza kuuza hata bei ya chini sana na ikiwa mnunuzi anahitaji arddhi hiyo sana anaweza kupandisha bei.


Ndugu mwana ukwaa hili, bila kupuuza umuhimu mkubwa wa ardhi niliutoa awali, naomba nihitimishe andiko langu hii kwa kukukumbusha ndugu mwanaukwaa hili kuwa ipo sababu nyingine Uhaba wa ardhi unaokua nchini Tanzania ukusukume kuanza mchakato mapema wa kumiliki kipande cha ardhi mapema.

Kutokana na takwimu za umoja wa Mataifa ya mapema mwaka huu mwezi wa saba, ilionesha kuwa idadi ya watanzania imefikia 61,942,797 na ongezeko ni 3%. Ukubwa wa ardhi iliyopo ni 885,800 KM za mraba ikijumuisha ardhi iiyotengwa kwa ajili ya mapori tengefu, mbuga za Wanyama.

Hivy hesabu hunesha kuwa ukigawa ardhi yote kwa watanzania kwa uwiano sawa kila mtanzania atapata kipande kidoogo sana cha ardhi.



Umiliki wa ardhi kwa kila mtanzania = Kiasi cha ardhi kilichopo

  • Idadi ya watanzania wote
= 885,800/61,942,797

=14,300SQM





Shukrani
 
Upvote 8
Back
Top Bottom