SoC02 Umuhimu wa Chanjo

SoC02 Umuhimu wa Chanjo

Stories of Change - 2022 Competition

tee smiley

New Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeainisha kuwa "kusitasita kwa jamii katika masuala ya chanjo" kumekua ni tishio kubwa kwa afya duniani. Hii husababishwa na watu kukataa au kuchelewa kuchanjwa ilihali wana uwezo wa kupata chanjo.

Chanjo ni dutu ya kibiolojia inayotumika kuiwezesha kinga ya mwili kupambana dhidi ya magonjwa ya kuambukiza. Na huundwa na kiwango kidogo cha bakteria, kirusi au sumu ambayo nguvu yake imepunguzwa au kuharibiwa maabara kwanza.

Hivyo hufanya aina mbili za chanjo, mosi chanjo hai : hii hutokana na virusi au bakteria waliomo kupunguzwa nguvu hivyo hupewa watu wenye kinga imara ya mwili na hutumika kuupa mwili ulinzi wa muda mrefu.

Pili chanjo iliyouawa: kwenye chanjo hii virusi huwa vimeharibiwa kabisa na yaweza kutolewa kwa watu wasio na kinga imara ya mwili pia huhitaji dozi nyingi ili kuupa mwili ulinzi kamili.

Chanjo zilianzishwa kwenye muongo wa 15 miaka ya 1400 hadi 1700. Na hakuna athari yeyote kwa mtu mwenye afya kupata ugonjwa unaosababishwa na chanjo aliyopewa.

Maranyingi chanjo huchukua miaka mingi ya majaribio na vipimo kabla haijathibitishwa pia ikianza kutolewa Tanzania hufuatiliwa na Mamlaka ya dawa na vifaa tiba nchini (TMDA) kwa ajili ya madhara yatakayojitokeza.

Ni salama kupata chanjo ukiwa mzima kuliko usubiri kuugua ili mwili ujitengenezee kinga ya asili kwani chanjo huufanya mwili wako kutengeneza kingamwili zinazo kulinda kwa muda mrefu kuliko utakapougua na kutibiwa maana utatumia gharama kubwa ya matibabu, utapata madhara yatokanayo na ugonjwa husika kama vile saratani ya ini inayosababishwa na virusi vya Hepatitis B au kifo.

Athari za chanjo ni za wastani na hudumu kwa muda mfupi tu nazo ni:

Mosi, eneo ambalo sindano hupita huweza kuvimba, kupata wekundu na kuwasha kwa takribani siku mbili au tatu.

Pili watoto waliochanjwa huweza kupata homa na joto la miili yao kuongezea kwa siku moja au mbili .

Hazina madhara makubwa ya mzio. Na hazihusishwi na magonjwa ya usonji, kupungua kwa kinga ya mwili wala madini ya mercury au viambata vyenye madhara .

Isipokuwa kama una tatizo la mzio wowote mueleze daktari .

Faida za chanjo ni nyingi nazo hujumuisha ;

Mosi, hukulinda wewe na mtoto wako dhidi ya magonjwa yanayopelekea kifo. Imeripotiwa kuzuia vifo milioni 3.5 hadi 5 kwa mwaka duniani kote.

Pili, Hupunguza gharama za matibabu kwani magonjwa yenye chanjo ni ghali kuyatibu .

Tatu,Huwalinda watu wasioweza kupata chanjo; hawa ni wale ambao kinga zao si imara, kutokupata magonjwa ya kuambukiza.

Nne, Huzuia kusambaa kwa magonjwa ya wasafiri kwenye nchi za ughaibuni pindi msafiri anapotembelea sehemu zenye mlipuko wa magonjwa.

Tano, Huzuia kuzuka kwa magonjwa na kufanya kutoweka kwa baadhi ya magonjwa kama surua, dondakoo na tetekuwanga kwani watu wamepewa chanjo.

Sita, Hutengeneza "kinga ya mifugo" hii ni pale ambapo watu wengi wamechanja hivyo ugonjwa hauwezi kuambukizwa kwa wasiochanja kwani jamii kubwa ina kinga na haiwezi kupata maambukizi.

Mwisho chanjo ni muhimu kwa afya yako kiujumla kama ilivyo mazoezi, kula mlo kamili na kufanya uchunguzi wa afya yako kwani ndio njia salama ya kuzuia magonjwa. Hivyo vijana , watoto na jamii nzima ielimishwe na kupewa chanjo ili tutengeneze kizazi chenye afya bora ambacho kitakuwa na nguvu kazi ya kutosha kwani jamii yenye afya huchochea Maendeleo.

“Wanangu tuchanje”
 
Upvote 0
Back
Top Bottom