ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 150
- 173
Dunia ya leo inahitaji utaalam/ufundi wa namna nyingi/Mbalimbali kwa mtu mmoja ili afanikiwe na kuwa kivutio katika soko la ajira na kuweza kwenda na wakati kulingana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia. Ndio maana waswahili husema kuwa “Mgaagaa na upwa hali wali mtupu (mkavu), lazima ataambulia angalau dagaa tu” vivyo hivyo katika kuipata elimu ni muhimu kutokata tama mapema.
Tusijiweke nyuma katika elimu yoyote yenye faida maishani, japo “Elimu yenye faida” inaweza kuwa na tafsiri tofauti kwa watu tofauti na elimu ina umuhimu wake kwa namna yake kama ifuatavyo...
Maisha ya msomi na mtu asiyesoma ni tofauti kabisa kwani msomi ana upeo mkubwa wa kufikiri na wa kukabiliana na changamoto za kimaisha kuliko mtu asiye na elimu ya kutosha.
Hivyo yatosha kusema kuwa, Elimu ndiyo utajiri usioweza kuibiwa au kuharibika hadi mtu anapoondoka hapa duniani; ingawa kuwekeza katika elimu ni mkakati wa muda mrefu unaohitaji dhamira, subira na kwamba matokeo yake huonekana baada ya muda mrefu wa uwekezaji..
Maana watu Wengi wamefeli katika Elimu kutokana na Changamoto mbalimbali ambazo zilikuwa ni sehemu ya kikwazo cha wao kufikia ndoto zao katika upande wa Elimu...
Msikilize jay moe katika wimbo wake unaitwa "Narudi shule" msanii jay moe baada ya kuingia mtaani, na kuona maisha ya mtaani yapo Tafu , wazo la haraka haraka aliona ni Bora Arudi shule..
Vijana wengi kwa 85% waliochezea Elimu ndio wanaojutia nafsi wakiwa mtaani kutokana na Ugumu wa maisha wanaokutana nao mtaani, wakati wakiwa wanasaka shilingi ili angalau mkono uweze kwenda kinywani!!!
Wakikaa wakitafakari wanajuta kwa kuchezea nafasi Enzi hizo wakiwa bado masomoni..
Wapo wengine pia huwa wana kauli kama ya jay moe . " Nirudi Shule"
Ila black rhino hakuwa nyuma aliamua kutoa ushauri kwa vijana..
Enjoy..
BLACK RHINO 🦏
"Nafunga mjadala kwa maneno yenye usia/ mambo muhimu vijana wezangu ya kuzingatia/ gonjwa la ukimwi hivi sasa limeshamili/ shiriki mazoezi ili kuepuka tamaa za mwili/ kama wewe ni mpenda ngono basi tabia badili/ tusije tukakuzika ukiwa na kilo mbili/ ukilikwa ujue hakuna tena jasiri/ kwan baada ya muda watu watasiona dalili/Nidhamu ya kijana wa sasa naona inashuka/ mpaka mtoto wa kiume nae sasa nywele anasuka/ wengi mtanichukia kwakuwa nasema ukweli/mtafutaji maisha sio lazima uzamie meli/ nenda kaulize masela keko na sengelea/ tabu wanazopata hazifai hata kuongelea/ kijana akizipata fedha ujue ni balaa/ japo sio desturi yake siku hiyo atakesha bar/ kivumbi siku ya mbili kilometa zinapokata/ kupingana mzinga ndio tukio linalofuata/ unapotenda wema ndugu hakikisha unajiondokea/Kama ni kalama molana atakuongezea/ binadamu wa leo wana roho za ajabu/ mtu anakuchukia pasipo kuwa na sababu/ na hoji maswali mengi majibu sipati kichwani/ yapata miaka sita nasota na hi fani/ muulize steve na becca wakupe picha halisi jinsi nilivyoteseka/ kinywa changu kipo huru lolote lile kusema/ fasihi yenye ujanzo na vina vimeshehena/ nashindwa kuelewa niite bahati ama ng'ekewa/ kabla sijakonga mlango tayari mgeni napokelewa/...
🔥🔥🔥🔥🔥🔥
#funguka
Unakumbuka nini ulipokuwa shuleni.
Ukwaju wa kitambo
0767 542 202