Umuhimu wa falsafa ya Kihistoria ya Kiafrika

Umuhimu wa falsafa ya Kihistoria ya Kiafrika

princebujonde

Senior Member
Joined
Jan 7, 2013
Posts
198
Reaction score
55
Kwa mujibu wa marejeo ya kihistoria (historical facts) tunaelezwa kuwa hadi kufikia karne ya 15 Africa na Ulaya walikua katika usawa wa kimaendeleo na kiteknolojia lakini walikuja kutuzidi maada ya maendeleo kibiashara(mercantalism na baadae mapinduzi ya viwanda), tena historia inazidi kutufunza kua hata kabla ya karne ya 15 Afica ilikua na historia yake na falsafa yake kile kinachoitwa falsafa ni chimbuko la uyunani ya kale(Greek philosophy) kinakoma kupata mashiko.

Kuna ushahidi wa kipekee kuwa Afrika ina falsafa yake kihistoria hata kabla ya karne ya kwanza.

Hata wanafalsafa maarufu kama Plato na Aristotle waliwahi soma falsafa Afrika, tunaelezwa kuwa Misri hasa Kemet na Timbuktu ilikua kitovu cha maarifa ya falsafa.

Hivyo basi kuna haja ya kuendeleza Falsafa ya kiafrika na kuacha kukumbatia falsafa za kigeni, kujikomboa kifikra tunahitaji kuikomboa nafsi kwanza.

Maoni yangu: Mtaala wenye somo la falsafa ya kiafrika uanzishwe kuanzia ngazi ya msingi hadi vyuoni.

Pamoja tutafika.

:A S thumbs_up:Tujadili hili..
 
Naam,

Lakini mkuu ungegusia japo kwa kuanzia. Wewe una maoni gani juu ya maeneo yapi hasa ya kuangazia kwenye uandishi huo wa Falsafa ya Kiafrika?

Una hoja nzuri na inajadilika..
 
Back
Top Bottom