SoC04 Umuhimu wa Katiba Mpya kuifikia Tanzania tuitakayo

SoC04 Umuhimu wa Katiba Mpya kuifikia Tanzania tuitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Nyanda Banka

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2023
Posts
304
Reaction score
1,054
Tanzania ni nchi yetu iliyojaa amani, umoja, mshikamano na upendo. Jambo kubwa na la msingi ambalo linahitajika na kufaa katika dira ya nchi yetu kwa miaka ijayo ni kama ifuatavyo

SUALA LA KATIBA MPYA, ili kupiga hatua katika kila sekta yetu yoyote ile msingi mkubwa ni kuwepo kwa katiba mpya ambayo italeta usawa na kuondoa ubaguzi kwa kila jambo ambalo linahusu taifa letu. Ni ukweli usiopingika kuwa katiba yetu ya sasa ina mapungufu mengi ambayo kwa kiasi kikubwa kuna baadhi ya maamuzi huonekana yana ukakasi pindi yanapoamuliwa kutokana udhaifu wetu wa katiba iliyopo. Na huu ni umuhimu wa katiba mpya katika nyanja mbalimbali kama ifuatavyo;

Siasa, umuhimu wa kuwepo kwa katiba mpya katika siasa inasaidia kutupatia viongozi wazuri na waadilifu kutokana na kuwepo kwa mfumo mzuri wa uchaguzi ambao utatokana na kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi ambayo haiegemei katika upande mmoja. Ukingalia kwa umakini mfumo wetu wa sasa ambaoo mgombea ndiye huchagua tume sio sawa kwa kuwa itazalisha upendeleo kwake.

Utawala, umuhimu wa katiba mpya katika utawala utatuondolea upendeleo kwa baadhi ya viongozi katika ngazi za utawala, hapa tuanajikita zaidi katika suala zima La "uteuzi" kwani viongozi wa kuteuliwa mfano ma RC na ma DC watakuwa wakifanya kazi kwa matakwa ya mtu fulani aliyewateua na sio upande wa wananchi na pia teuzi huzalisha viongozi wa sio wazalendo kwani yawezekana wasiwe wazaliwa wa eneo husika hivyo kukosa uchungu wa kupambania eneo hill kwa dhati akiaamini muda wowote anaweza kuhamishwa ama baada ya kustaafu atarudi kwao na sio hapo.

Afya, kupitia katiba mpya itatupatia sera nzuri zenye kuleta usawa katika suala zima la afya suala la bima kwa wote liwe sasa kwa wananchi wote na kusiwe na aina ya bima tofauti ambazo hubagua aina ya maradhi hata kwa wananchi wa hali ya chini, kusiwepo bima za viongozi wala watumishi bali ziwepo bima kwa wote na kwa usawa ule ule sio viongozi wakiumwa hao ndio wanapaswa kusafirishwa kwenda nje kwa matibabu iwe hata kwa wananchi wa kawaida pia.

Elimu, katiba mpya kwenye suala la elimu itatusaidia kuondoa huu mfumo wetu wa elimu ya kikoloni ambao kwanza hutumia muda mwingi kuipata elimu hiyo kitu ambacho ni ngumu kwetu kuona vijana wa miaka 25 - 35 kupata hadhi ya kuwa profesa ukilinganisha na baadhi ya nchi nyingine ulaya, kutokuwepo kwa elimu kwa vitendo kuannzia ngazi za awali mpaka juu na ndomana tunakuwa nyuma katika uvumbuzi na ugunduzi wa vitu mbalimbali duniani, tuondoke katika elimu bure ambayo wanafunzi wanakaa chini kwa kukosa madawati na kujenga mejengo mengi ya shule huku walimu hawaajiriwi wapo mtaani na Degree zao wanauza pweza. Pia sera mpya ya lugha ya kufundishia kuanzia ngazi za awali hadi juu iwe lugha yetu ya taifa yani kiswahili ili kurahihisisha uelewa kwa wanafunzi na kufaulu vizuri kwani matumizi ya lugha ya kigeni imekuwa sababu ya ufaulu mbovu kwa wanafunzi nchini, haina haja ya kusoma udaktari kwa kingereza ama kilatin au kigiriki, kiswahili kinatosha.

Mawasiliano, katiba mpya italeta uhuru wa kutosha kwa vyombo vya habari katika kuleta ufanisi katika majukumu yao ya kazi bila kuhofia juu ya mtu fulani ama chama fulani hii itapelekea kupunguza na kuondoa waandishi makasuku, vile vile kuwalinda na kuwaheshimu wale wote wanaokosoa iwapo kweli kutakuwa na ubadhirifu ama utovu wowote uliyosababishwa na viongozi ama chama fulani, isitumike nguvu kubwa kwa wakosoaji kama kuwapeleka polisi na vipigo kama sio raia wa nchi kuwepo na mifumo ambayo itamuwezesha kila raia kutoa maoni take kwa uhuru kuanzia ngazi za chini mpaka juu.

Hivyo basi, katika kuiangazia Tanzania tuitakayo kwa miaka ijayo ni bora zaidi tukajikita zaidi katika upatikanaji wa KATIBA MPYA ambayo itakuwa muongozo sahihi katika kila hatua ya maendeleo yetu, kupitia katiba mpya isiyompa kiongozi fulani madaraka na mamlaka makubwa zaidi itatusaidia kuepuka mikataba ya hovyo, ubinafsishaji na matumizi mabaya ya madaraka, katiba mpya italeta nidhamu, uzalenfo na usawa kwa wote bila kujali cheo cha mtu wala hadhi yake. Katiba inagusa kila kona ya hatua za nchi hivyo kujikita zaidi katika hili itakuwa tumejikomboa kifikra, hatuwezi kuwa na miaka 60 ya uhuru alafu bado huduma za kijamii kama vile maji, umeme ni tatizo. TURUDI MEZANI KATIBA MPYA NI SASA.

Hussein .M. Bendera
0676917970
 
Upvote 1
Back
Top Bottom