Umuhimu wa Kiarabu kuwa lugha Rasmi Tanzania

Kaka ulitumia hapa juu maneno 88.

Kati ya maneno haya uliona vema kuingiza maneno 26 ya Kiingereza (sijui kama ni dalili ya ubora au uhaba wa elimu?).

Maneno 62 ni Kiswahili. Kati ya hayo ni maneno 48 yenye asili ya Kibantu, na 14 yenye asili ya Kiarabu.

Hakuna aliyesema Kiswahili ni Kiarabu ila tu Kiswahili kwa bahati nzuri ni kati ya lugha zilizotokea kwa kuathiriwa na lugha ya nje (yaaniKiarabu) na hivyo hadi leo zenye uwezo wa kupokea maneno ya nje kirahisi. Hapo kinafanana na Kiingereza kilichanza pia kama lugha ya Kigermanik (kama Kiholanzi, Kijerumani) kilichopokea maneno mengi sana kutoka Kifaransa / Kilatini. Mimi naona lugha za aina hii zinakua kwa upesi kushinda lugha nyingine ambako wasemaji wanavutana zaidi kuhusu "usafi" wa lugha.
 
Mbona 50% ya maneno ya Kiswahili ni ya Kiarabu likiweno neno "Swahili"?

Kiswahili ni more Bantu than Arabic. Kama ingekuwa hivyo watu wanaoongea Kiarabu wangesikilizana bila shida na waongeaji Kiswahili.

Proof: Waislamu karibu wote hapa Tanzania waliokaririshwa Qur'an hawaelewi maana ya kile walichokikariri kwa Kiarabu japo wanaeelewa Kiswahili.
 
Hawa waarabu itakuwa kuna jambo wanakutenda siyo bure.
 
Kama kiarabu kisingekuwepo,kiswahili kingekuwepo
Kwanza Kiswahili si kiarabu na kiarabu si kiswahili.
 
Mkuu wa kwanza alipotea tokea mwanzo, hivi Kiswahili kilitokea wapi! Tungeendelea na Kiingereza toka wakati ule tungekuwa tumekizoea na tungekuwa mbali. Angalia sasa hivi tunahangaika kupeleka watoto shule za “English medium” kisa tu ajuwe Kiingereza!!!!!!!
 
Hii ni kasumba tu ya mataifa yasiyoendelea
Leo hii wachina wapo juu bila kuwa wazungumzaji wa kiingereza.
Waitaliano wapo vizuri na siyo wazungumzaji wa kiingereza.
Wajerumani,wafaransa,wakorea,kiingereza siyo ishara ya usomi wala maendeleo.
Wengi tunakimbilia kiingereza kwa ajili ya ajira za kuajiriwa na kwa sababu kubwa ni uchumi mdogo.
Ila nacho jisifu ni kuwa,Nazungumza ligja tatu bila wasiwasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…