Nilikuwa nasoma bajeti ya elimu.
Nimeona mambo mazuri ya vyuo vya ufundi vya cheti, astashahada, stashahada na shahada, na kuona kila wilaya inatarajiwa kuwa na chuo cha veta na vinginevyo. Najua ni jambo jema. Lakini havyo vyote na vya kujiajiri na wanahitaji kula.
Ninachojiuliza kwanini hakuna mkazo mkubwa kuhusu kilimo kielimu?
Sijaona po pote inaelezea vyuo au mafunzo ya muda mfupi kwa ajili ya kilimo yanafanyika. Nashukuru kwa kuongeza vyuo vikuu lakini tunahitaji elimu ndogo ndogo kuhusu kilimo na mifugo na umwagiliaji isambae kwa wananchi au kuanzisha vyuo vya muda mfupi ili watu wajitegemee kwa kilimo.
Je wizara ya elimu haihusiki na hili?