SoC02 Umuhimu wa kuchangia damu

SoC02 Umuhimu wa kuchangia damu

Stories of Change - 2022 Competition

rammy19

New Member
Joined
Sep 15, 2022
Posts
1
Reaction score
4
UMUHIMU WA KUCHANGIA DAMU.

Damu ni zawadi ya thamani ambayo mtu anaweza toa. Damu inayotolewa hutumika kwa wagonjwa waliojeruhiwa na majanga mbali mbali ,wagonjwa wa saratani ambao wanahitaji kuongezewa damu,na wagonjwa wanaopoteza damu wakati wa upasuaji mkubwa. Kabla ya kupatiwa mgonjwa damu iliyokusanywa hupimwa vvu,homa ya ini na kaswende..Mchango mmoja wa damu unaweza kuokoa maisha hadi ya watu watatu.

Kumekuwa na imani porofu nyingi na mambo yasiyo ya kweli ambayo watu wanayaamini katika jamii kuhusu utoaji wa damu ikiwemo fikra kuhusu watu wasiokula nyama kuwa hawawezi kutoa damu kutokana na wasiwasi wa kwamba hawapati madini ya kutosha hii si kweli iwapo mtu huyu anakula lishe bora yenye virutubisho vizuri basi bila shaka atapata madini ya kutosha ya iron mwilini na ataweza kuchangia damu.

Pia kuna watu wanaamini kuwa watu wenye michoro ya tattoo kutoweza kuchangia damu ukweli ni kwamba ni lazima wasubiri kwa miezi minne kutoka siku uwaliochorwa tatoo na baada ya hapo wanaweza kuchangia damu.

Vilevile kuna jamii zinaamini kwamba uchangiaji wa damu hupelekea damu kuisha mwilini ,wakati hakuna kiwango cha mwisho cha damu mwilini na unapochangia damu mwili hufanya kazi ya kurudisha seli na maji uliopoteza mwilini na kwa kawaida damu uliochangisha inarudi mwilini baada ya siku moja.Na huwezi kupata maambukizi kwa kuchangia damu kama wengi wanavyodhani.

Umuhimu wa wachangiaji damu unaonekana wazi na umuhimu mkubwa kabisa ni kuokoa maisha ya mtu ambae angefariki kwa upungufu/ukosefu wa damu mwilini tendo hili ni la kishuja na ni ishara ya upendo wa kweli kwa mgonjwa muhitaji wa damu.

Pia uchangiaji wa damu unapunguza madini joto mwilini ambao yakizidi yanaweza kusababisha mapigo ya moyo kuongezeka na mwili kujihisi kuchoka. Na unapochangia damu unachoma kalori na kupunguza uzito wa mwili.vile vile kichangia damu kunapunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa saratani,na kunaboresha kujiamini na kuongeza uelewa juu ya uchangiaji wa damu. Aitha unawezesha kupima afya bila malipo na kupatiwa kitambulisho cha uchangiaji wa damu.

Mbali na yote kuna vigezo/sifa za mtu mwenye uwezo wa kuchangia damu: kwanza Awe ni mwanamke au mwanaume mwenye umri usiopungua miaka 18,kwa upande wa mwanamke asiwe mjamzito au mtu anayenyonyesha,asiwe ma uzito usiopungua kilo 50, asiwe na magonjwa kama vile kisukari au shinikizo la damu, asiwe na ugonjwa wa kifafa na pia asiwe Katika tiba yoyote ile.

Changia damu okoa maisha
 
Upvote 4
Back
Top Bottom