SoC02 Umuhimu wa kujitolea baada ya kuhitimu chuo na jinsi kulivyobadili maisha yangu

SoC02 Umuhimu wa kujitolea baada ya kuhitimu chuo na jinsi kulivyobadili maisha yangu

Stories of Change - 2022 Competition

olais reuben

New Member
Joined
Jul 2, 2014
Posts
3
Reaction score
11
Mimi ni kijana wa Kitanzani nilietokea katika familia ambayo mimi pekee ndio niliesoma mpaka elimu ya chuo kikuu.

Nilipomaliza chuo Kikuu cha Muhimbili(MUHAS) mwaka 2019 Course ya ENVIRONMENTAL HEALTH SCIENCE nilijawa na hofu sana kwani vijana wengi waliomaliza miaka mingi nyuma hawakupata ajira wengine mpaka miaka 7 nyuma wapo mtaani wanakula msoto.

Basi Baada ya kuhitimu mwezi wa nane mwaka 2019 nikaanza kusambaza wasifu (cv) ofisi za Halmashauri mbalimbali na pia kupeleka Wizara ya Afya kwa bahati nzuri kulikuwa kuna uhitaji sana wizara ya Afya nikapata nafasi ya kujitolea rasmi bila malipo ikabidi nijitose ili kufukuzia ndoto zangu.

Nilipoanza kujitolea yapata mwezi wa tisa mwaka 2019 vijana wengi waliohitimu nyuma walianza kunisema sana kuwa sitapata hela lakini mimi lengo langu ilikuwa ni kuongeza ujuzi katika kazi.

Yapata mwezi wa tatu mwaka 2020 nikabahatika kupata mkataba na shirika la Mkapa Foundation kwani walikuwa wanaajiri watu wote waliokuwa wanajitolea Wizara ya Afya na Tamisemi kada za Afya ili kusaidia kupambana na ugonjwa wa Corona, kujitolea kwangu kulinibeba sana kiasi kwamba kila mkataba ukiisha wakitaka kurenew mkataba mpya wananiweka na mimi.

Kutokana na kujitolea kwangu na pia kufanya kazi kwa mkataba ilinisaidia kuajiriwa rasmi Serikalini mwezi wa 6 mwaka 2022 kwani nilipoomba kazi nilikuwa na uzoefu wa kutosha na pia Serikali wanafahamu juhudi zangu katika kazi hata kipindi nikiwa najitolea.

Kwa uzoefu wa kujitolea nimepata maana halisi ya kujitolea kuwa ni njia rahisi kwa watu wasio na watu wa kuwasemea(mtaani wanaita connection) kuuza ujuzi wao na muda wao ili kupata kujulikana kwani ndio njia pekee ya kujionesha ili uajirike. Vijana wajuzi husema kama huna pesa za kuwekeza wekeza katika muda.

Jambo lingine ni kuwa kujitolea ukiwa unachapa kazi utapata fursa kama semina za kiofisi, malipo ya kazi za ziada( etra duty allowance) na vyanzo mbalimbali vidogo vidogo ambavyo vinamsaidia anaejitolea kujikimu japo mshahara hautakuewepo lakini pesa za kuishi zitakuepo.

Kujitolea ni kauli inayotumika kuwaogopesha vijana wengi lakini ni njia sahihi ya mafanikio na kukutana na watu sahihi watakaosaidia kupata ajira za kudumu kwa kukuelekeza njia sahihi za kufata.

kwa kumaliza niseme kujitolea ni muhimu kuliko kukaa mtaani bure na kusahau utaalamu uliojifunza vyuoni na hili ni wazo langu kwani mimi na vijana wenzangu zaidi ya 1000 tulioajiriwa ajira mpya tulipitia kujitolea atleast kuanzia miezi mitatu mpaka miaka kadhaa.

Ni mimi kijana wenu

Afisa Afya mazingira mbobezi kabisa
O.R.M
 
Upvote 7
Back
Top Bottom