DidYouKnow
JF-Expert Member
- Jul 28, 2019
- 1,229
- 1,950
Katika jamii yetu ya Watanzania, suala la kuzuiliwa kwa miili ya marehemu hospitalini kutokana na madeni ni tatizo ambalo limekua likijirudiarudia mara kwa mara na kuzua mijadala mikali.
Wengi tunaamini kuwa madeni haya yasamehewe kwa sababu aliyekufa sasa ni maiti, na kwa mtazamo wetu, mwili kuachwa hospitalini hautaleta madhara yoyote kwa wadaiwa maana mwisho wa siku lazima utazikwa tu.
Hata hivyo, mtazamo kama huu si mzuri na hutokea zaidi katika jamii ambazo ni maskini na ambazo mara nyingi huwa hazijali uwajibikaji wa kifedha na kijamii.
Hospitali zina jukumu la kutoa huduma bora za afya kwa wananchi. Huduma hizi zinahitaji rasilimali nyingi, ikiwemo dawa, vifaa tiba, na mishahara ya wafanyakazi. Wapendwa wetu waliofariki katika hospitali hizi, watakuwa wameigharimu hospitali, eneo moja au lingine la vitu vilivyotajwa.
Madeni yanaposhindwa kulipwa, hospitali zinapata changamoto kubwa katika utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa wengine. Hali hii inaweza kusababisha upungufu wa dawa na vifaa tiba, na hivyo kuhatarisha maisha ya wagonjwa wengine.
Kuna mifano mingi ya watu na taasisi zinazochangia hospitali, vyuo au programu za magonjwa baada ya kupoteza wapendwa wao, ili kuzuia vifo vingine kwa watu wengine.
Mfano huko duniani baadhi ya wagonjwa hutoa wosia kwamba wakifariki miili yao au sehemu ya viungo vya miili yao vitumike kama sehemu ya mafunzo ili kuzuia vifo kwa wengine.
Hapo ndipo moja ya sehemu ambayo marehemu anakuwa mwalimu kwa walio hai. Pia kuna familia ambazo huchangia vifaa au pesa katika hospitali baada ya ndugu zao kufariki kutokana na magonjwa mbalimbali kama kumbukumbu au kusaidia kuboresha huduma za afya kwa wale waliosalia.
Mentality kama hii inajengwa na imani kuwa kifo changu au chako, si mwisho wa maisha ya wengine. Michango hii husaidia wagonjwa wengi kupata huduma bora na kuepuka vifo vya magonjwa mbalimbali. Hii inaonyesha kuwa, ingawa mpendwa wao amefariki, msaada wao unaweza kusaidia kuokoa maisha ya wengine.
Ukiacha lindi kuu la umasikini, bado pia jamii yetu imekuwa inakumbana na changamoto ya uwajibikaji kutokana na historia ya kupata huduma za bure za elimu na afya mara baada ya Uhuru.
Huduma hizi zilikuwa nzuri kwa wakati huo, lakini hazikutujengea utamaduni wa uwajibikaji na zikatutengenezea mentality ya utegemezi katika baadhi ya vitu ambavyo sasa watu wakikosa huilamu serikali.
Watu wengi walizoea kupata huduma za afya na elimu bila malipo, hali ambayo katika ulimwengu wa sasa inahitaji kubadilika ili kutujengea uwajibikaji.
Mfano ambao hauhusiani na maiti, ni ujauzito na uzazi - wakati watu wanapofanya uamuzi wa kupata mtoto, ni muhimu pia kufikiria kwa kina kuhusu gharama za ujauzito na kuzaa. Hii haipaswi kuwa jukumu la hospitali na serikali pekee au kutegemea huduma za bure pekee.
Ili kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa kila mtu, ni muhimu kwa wananchi kuchangia kwa uwezo wao kwa njia mbalimbali, ikiwemo kulipa madeni ya hospitali na kujiunga na mifuko ya bima za afya.
Hii itasaidia kuimarisha mfumo wa afya na kuhakikisha kuwa huduma muhimu zinapatikana kwa wote.
Ni muhimu kuelewa kuwa kulipa madeni ya hospitali hata baada ya kifo cha mpendwa ni ishara ya uwajibikaji na upendo kwa jamii nzima.
Kwa kulipa madeni haya, tunasaidia hospitali kuendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa wengine na kuhakikisha kuwa hakuna maisha yanayopotea kutokana na matatizo yanayoweza kuzuilika.
Tunajenga jamii inayowajibika na yenye afya bora kwa wote, huku tukionesha heshima kwa maisha ya wale waliotangulia mbele ya haki.
Mshana Jr Numbisa Mmawia BAK Erythrocyte Nyani Ngabu FaizaFoxy johnthebaptist

Upvote
1