Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
UMUHIMU WA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA SYKES KATIKA KUIJUA HISTORIA YA MWALIMU NYERERE, TAA NA TANU 1
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika hotuba yake maarufu ya kuwaaga wazee wa Dar es Dar es Salaam aliyotoa Ukumbi wa Diamond mwaka wa 1985 alisema yeye alipelekwa nyumbani kwa Abdul Sykes na Joseph Kasella Bantu baada ya kumuuliza nani anaongoza TAA Dar es Salaam. Kasella Bantu akamwambia ni Abdul Sykes.
Hivi ndivyo Nyerere alivyofikishwa nyumbani kwa Abdul Sykes.
Katika hotuba ile Nyerere akasema kuwa anadhani, Abdul Sykes alikuwa katibu.
Mwalimu alikuwa hana hakika na nafasi ya uongozi wa Abdul katika TAA.
Kiasi kumbukumbu zipotee kwani miaka mingi ilikuwa imepita toka ajuane na Abdul mwaka wa 1952 enzi za TAA na hadi mwaka wa 1985 wakati anastaafu uraisi, miaka 33 ilikuwa imepita. Kwa bahati mbaya kwa kipindi hicho chote cha miongo mitatu historia ya TANU haikuwa imehifadhiwa kwa uhakika wake.
Lakini ukweli ni kuwa Nyerere alipokutana na Abdul Sykes, Abdul alikuwa Kaimu Rais na Katibu wa TAA.
Kabla ya hotuba hii Nyerere hakuwahi hata siku moja kueleza historia yake vipi alifika hadi kuwa Rais wa TAA 1953 na TANU 1954 na katika mambo ya kushangaza sana katika uandishi wa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika hakuna mtafiti yeyote aliyeeleza hili.
Hata kitabu cha historia ya TANU kilichoandika na Chuo Cha CCM Kivukoni mwaka wa 1981, kitabu hiki hakikueleza vipi Nyerere alikuja Dar es Salaam na kuongoza chama kilichokuja chini ya uongozi wake kuwa na nguvu kubwa na moja ya vyama vya siasa vilivyoheshimiwa sana Afrika wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Lakini miongoni mwa wale wazee bila shaka walikuwapo wale ambao walimuona Nyerere toka siku ya kwanza iwe labda Sokoni Kariakoo ofisini kwa Abdul Sykes alipokuwa akipenda kwenda baada ya kujiuzulu ualimu na kuishi kwa muda nyumbani kwake au walimuona mitaani akiwa na Abdul na Dossa Aziz katika juhudi za Abdul kumjulisha Mwalimu kwa wenyeji wa Dar es Salaam.
Katika hotuba ile ya kuwaaga wazee wa Dar es Salaam Mwalimu labda kwa kusahau, au kwa makusudi au kwa kutoona umuhimu wake, hakueleza hadhira yake kuwa yeye alipata kugombea urais wa TAA dhidi ya Abdul Sykes katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Arnautoglo tarehe 17 Aprili, 1953 msimamizi wa uchaguzi ule akiwa Denis Phombeah Meneja wa Ukumbi wa Arnautoglo.
Uchaguzi huu ni mada inayoweza kujitosheleza na ni kuanzia hapa katika ukumbi ule uliojengwa na Mgiriki tajiri George Arnautoglo mtu anaweza kusema ndipo Nyerere alipoanza safari yake ndefu ya siasa na uongozi wa Tanganyika hadi kufikia uhuru mwaka wa 1961.
Kasella Bantu ndiyo sababu ya mimi kufunguliwa nyaraka hizi na Ally Sykes na yeye pia akiwa kati ya waasisi 17 wa TANU mwaka wa 1954.
Kasella Bantu alikuwa kaghadhibishwa na historia ya TANU kama ilivyokuwa inaelezwa na TANU yenyewe na kwa ajili hii akaandika makala katika jarida moja lililokuwa likichapwa London akieleza mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika na akalaumu kwa historia ya TANU kumtaja Nyerere peke yake (New African March, 1985).
Nilibahatika kusoma makala ile na mimi nikajibu makala ile kwa kusema kuwa ni muhimu historia ya TANU ikatazamwa upya kwa nia ya kuwaadhimisha wapigania uhuru wote (New African, May 1985).
Ally Sykes alisoma makala hii yangu na akaipenda sana kiasi akaniita ofisini kwake kunipongeza.
Katika mazungumzo yetu akanieleza kuwa yeye siku zote amekuwa na hii fikra ya kumtafuta mwandishi aandike historia ya ukoo wao katika siasa za Tanganyika kuanzia miaka ya 1920 baba yake alipokuwa katika kundi lililoasisi African Association hadi kupatikana uhuru mwaka wa 1961 ambamo wao kama watoto wa Kleist Sykes walishiriki kikamilifu.
Akaniambia kuwa ana nyaraka ndani ya sefu yake ambazo zina taarifa nyingi kuhusu harakati za uhuru wa Tanganyika.
Mimi palepale bila ya kusita nikamuomba anionyeshe hizo nyaraka ili niandike hiyo historia.
Yeye fikra yake ilikuwa kuwapata wataalamu kutoka Ulaya awakabidhi hizo nyaraka kwa minajili ya kusaidia utafiti na mwishowe kuandika kitabu.
Bwana Ally akaniuliza kama mimi nina uwezo wa kufanya kazi hiyo.
Nilimwambia nitajaribu na kama hatoridhika basi anaweza kuwapa hizo nyaraka watafiti wengine.
Nyaraka hizi Bwana Ally alinieleza alikuwa amezifungia kwenye sefu kwa takriban miaka 30 na alikuwa hajui funguo za sefu alimohifadhi hizo nyaraka ziko wapi.
Akaniomba nimpe siku tatu atafute hizo funguo na ikiwa hataziona ataleta mafundi wavunje ile sefu.
Funguo zilipatikana na akanikabidhi mafaili ambayo kwa muonekano tu picha niliyopata ni kuwa zilikuwa ni mafaili kutoka miaka mingi iliyopita wakati Waingereza ndiyo watawala wa Tanganyika.
Yale yalikuwa mafaili kutoka dunia ambayo ilikwishamaliza muda wake wa kuishi.
Nilizichukua faili zile na kuanza kazi mara moja nikisoma karatasi moja baada ya nyingine nikianza mwanzo wa faili hadi mwisho wake.
Kusema kuwa nilishtushwa na yake niliyokutananayo bado itakuwa sijaeleza ukweli wa hali yenyewe.
Kwa ufupi wa maneno labda niseme mfano wake ni kama mtu aliyenishika mkono akanigeuza kurejea nyuma na kuniingiza katika dunia nyingine iliyopita miaka mingi nyuma.
Ikiwa imeandikwa kwa mkono basi itakuwa imeandikwa kwa wino na kwa hati nzuri ya kupendeza iliyolala.
Lugha ikiwa ni Kiswahili iwe barua au ‘’cutting’’ ya gazeti itakuwa lugha ambayo maneno yake hayatumiki sana siku hizi. Kila kitu nilichoshuhudia katika nyaraza zile kilikuwa kigeni kwangu.
Haya mafaili kwangu mimi ilikuwa sawa na ‘’Alice in Wonderland.’’
Katika nyaraka hizi ndipo nilipokutana na Kassella Bantu na Julius Nyerere, wapigania uhuru wawili ambao miaka ile walikuwa marafiki na kwa pamoja walichukuzana kuja kwa Abdul Sykes safari ambayo ikaja kuwa chanzo cha maisha ya Nyerere kubadilika na kupelekea kuacha ualimu na kuwa kiongozi aliyewaongoza Watanganyika kudai uhuru wa nchi yao kutoka kwa Muingereza.
Nyaraka za Sykes zina historia ya Kasella Bantu ambae Nyerere.
Halikadhalika nyaraka hizi zina historia ya kutosha sana ya Nyerere mwenyewe.
Iweje na hili ni swali mtafiti yeyote litamjia mara moja kuwa Nyaraka za Sykes zina historia ya wazalendo hawa wawili waliochukuzana Jumapili moja asubuhi baada ya kutoka kanisani wakaenda nyumbani kwa Abdul Sykes na wote hawa wawili wakachaguliwa katika mkutano wa TAA Arnautoglo Hall, kuongoza TAA Nyerere kama President, Abdul Sykes Vice-President na Kasella Bantu Secretary General (Tanganyika Standard 19th June, 1953).
Ukiangalia gazeti hili utakuta majina ya viongozi hawa wa TAA pamoja na majina ya wazalendo wengine kutoka nje ya Tanganyika lakini wamechaguliwa katika uongozi wa TAA kama Dome Okochi Budohi kutoka Kenya na Denis Phombeah kutoka Nyasaland.
TANU ilipokuja kuundwa mwaka wa 1954 Budohi kadi yake ya TANU ilikuwa no. 6 na Denis Phombeah no. 5.