Umuhimu wa kumuombea mume wako

Umuhimu wa kumuombea mume wako

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Umuhimu wa kumuombea mume wako

Kumuombea mume wako ni muhimu kwasababu unapomuombea mumeo ni kama unajombea wewe. Mafanikio ya mume wako ni ya kwako pia

Unapomuombea mumeo inaongeza na kukuza upendo wako kwake

Inakuamsha kwenye upendo mkuu zaidi wa Mungu aliokuunganisha na ndoa yako

Unakabiliana na mashambulizi ya kiroho maan wewe ni mlinzi wa mumeo. Mlinzi sio kwa maana ya kukagua simu zake muda wote na kuzidaka juu kwa juu. Mlinzi kwa kusugua goti yaani kwa maombi

Waume zetu sio maadui zetu. Hata kama ana kuudhi na kukukera lkn wewe ndiye ulimchagua kuwa naye hivyo muombeee sana. Nyakati ambazo huwezi kumuombea ndizo nyakati anazokuhitaji zaidi

Maombi yana faaa zaidi kuliko kujilalamisha. Kumuombea mumeo kunaweza kukubadirisha zaidi mtazamo wako kwake ukabadirika kabisa na ukaanza kumpenda zaidi

Tunawaombea kwasababu ktk ulimwengu wa roho wanawake wana nguvu zaidi kuliko waume zetu hivyo usichoke kumuombea mumeo kila siku.

Kama unachakuongezea hapo karibu tuelimishane
 
Bujibuji umekuwa nabii siku hizi?
 
Mwanamke anapaswa kutembea na nakala ya picha ya mumewe kwenye Biblia, akienda kanisani kwenye kipindi cha maombezi awe anaipeleka hiyo picha ikaombewe na mtumishi wa Bwana.
Niliyaona hayo kwa manabii. Maombi ninayomaanisha ni Yale ya kumlingana BWANA
 
Back
Top Bottom