Umuhimu wa kuoa/kuolewa mapema

Umuhimu wa kuoa/kuolewa mapema

Candela

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2021
Posts
817
Reaction score
2,180
Habarini wana jf, leo nitazungumzia mada tajwa hapo juu.

Kumekuwa na kasumba ya watu kusubiri afike umri flan ndio aingie katika ndoa.

Hii inasababishwa na iman miongon mwa watu kuwa kuoa katika umri mdogo kuna changamoto lakini ukweli ni kama hivi;

1. Kuoa mapema kunakuepusha na hatari ya kupata maradhi kwan badala ya kuzunguka huku na huko unatulia na mmoja
2. Ukioa mapema unazaa mapema pia. hii itasaidia kukuweka karibu na wanao. Unapozaa katika umri mkubwa watoto wako wanapata changamoto ya kushindwa kuwa karibu hasa katika masuala yahusuyo makuzi.
3. Kuaminika. Unaopokuwa umeoa inaongeza imani yako katika jamii. Watu waliooa wanaheshimika zaidi kuliko wasiooa.
4.Unafuu wa maisha. unapokuwa umeoa unakuwa na mwenza ambae mnaelewana hata inapotokea uchumi hauko vizuri anaweza kukuvumilia mapungufu yako, tofauti na kama hujaoa mwanamke anaweza asikuelewe ukisema huna pesa.
5. Usalama. unapokuwa umeoa ni kawaida sana kuweka akiba kwa ajili ya dharura. hii inakuweka katika hali ya usalama tofauti na ukiwa unaruka nao wa kila aina.

NB: ZINGATIA HAYA UISHI KWA FURAHA.
 
Back
Top Bottom