Umuhimu wa kupanga muda

Umuhimu wa kupanga muda

badshah

Member
Joined
Mar 16, 2013
Posts
51
Reaction score
32
Staryte - Elimu, Burudani na Maendeleo

Nini maana ya kupanga muda?

Hizi ni kanuni, mazoezi, ujuzi, zana na mifumo inayokusaidia katika kutumia muda wako kwa ajili ya kukamilisha jambo unalolitaka.

Ni kwanini kupanga muda ni muhimu?
Upangaji wa muda ni muhimu kwa maisha yako binafsi na mafanikio katika kazi. Inakufundisha jinsi ya kupangilia muda wako ipasavyo na kuutumia vizuri.

Hizi ni sababu chache zinazotujulisha kuwa kwanini jambo hili ni muhimu, na jinsi gani inaweza kukusaidia kutumia na kuupangilia muda wako kwa manufaa:


  1. Muda ni zana maalum ambayo huwezi kuihifadhi kwaajili ya matumizi ya baadaye. Kila mtu ana kiwango sawa sawa cha muda katika kila siku. Muda ambao haukutumiwa vizuri hauwezi kuurudisha.
  2. Watu wengi hudhani kuwa wana kazi nyingi kiasi ambacho muda hautoshi, hulalamika kwa kiwango kidogo cha pesa, malengo yasiyokamilika, mawazo mengi, uhusiano mbaya na kutokufanya mazoezi ya mwili. Ukifanya busara katika kupanga muda kutakusaidia kupata muda wa kufanya yale uliyopenda kufanya.
  3. Unahitaji muda ili kufanya kile unachotaka kufanya katika maisha. Kama ukisubiri muda wa ziada utokee, unaweza kupoteza mambo muhimu katika maisha. Kwa kupitia upangaji mzuri wa muda wako, unaweza kutengeneza muda unaohitaji, na sio kuusubiria uje. Kwa kupanga muda wako kwa busara, utakuwa na muda mwingi wa kufanya vitu vingi.
  4. Upangaji wa muda utakusaidia kupangilia yale unayoyahitaji kuyafanya hasa.
  5. Masaa yana kikomo cha masaa 24 kwa siku, hivyo panga muda wako kwa busara.
  6. Upangaji wa muda unakusaidia kutengeneza chaguo lenye akili, hivyo unaweza kutumia muda wako mwingi kufanya vitu ambavyo vina thamani na umuhimu kwako.
  7. Unaweza kujifunza kutafuta muda kwaajili ya vitu ambavyo ni muhimu kwako. Hata kiasi kidogo tu mara moja kwa siku, au hata mara moja kwa wiki, itakupelekea karibu kufikia katika malengo yako, na utashangaa kuona maendeleo unayofanya.
  8. Unakuwa mzalishaji bora kwa kutumia ujuzi wa kupanga muda ulio bora na zana, na unaweza kufanikisha mengi kwa muda mchache. Upangaji wa muda unaweza kupunguza upotezaji wa muda na nguvu,, unakusaidia kuwa mbunifu, na unakuwezesha kufanya vitu muhimu kwa muda wake. Hii itakuendeleza katika kukamilisha yale uliyoyapanga.
  9. Muda wa siku hizi umechanganyika na mambo mengi mabovu, na hivyo, ni rahisi sana kupoteza muda kwa kufanya mambo yasiyo na maana. Jiulize, kuangalia TV au kipindi fulani, au kusoma hili na lile au kushiriki katika mabaraza na vijiwe kutaniongezea lolote la maana katika maisha yangu? Na je muda niliotumia katika shughuli fulani niliutumia vizuri? Au ni kupoteza muda na nguvu?
  10. Muda huweka mambo mengi mbele ya mtu kila siku, na swali linakuja kuwa, unafuata kile kinachokujia mbeleni au unafuata na kuchagua kile unachohitaji kufanya? Na je unaruhusu matatizo ya nje kuingilia mipangilio ya malengo yako, au unajitahidi kutumia akili, busara na nguvu ya ziada kuhakikisha uko katika mstari wa kukamilisha malengo yako, bila ya kupoteza muda na nguvu?
  11. Baadhi ya mambo ya ndani ya akili na amani ndani ya moyo wako yana msaada mkubwa sana katika kupangilia muda wako ipasavyo. Kama ukiepuka kutumia hisia na nguvu za akili yako juu ya kile watu wanachosema au kufikiri juu yako, na kama ukitulia badala ya kuwa na mawazo, matatizo na ugumu fulani, unaweza kuokoa muda mwingi na nguvu, ambao unaweza kuutumia kwa mambo mazuri na yenye faida na manufaa kwako.

Kuna vitu vingi sana unaweza kuvifanya na zana ambazo zitakusaidia kupangilia muda wako. Kuna muda mwingi unapotezwa kila siku, ambao unaweza kutumiwa kwa mambo mazuri na ya maana. Kuna mabadiliko unayoweza kuyafanya, ambayo kwa uzuri kabisa yanaweza kukuongezea muda uliokuwa nao katika mipangilio yako ya kila siku.

Kufikiri, kupanga, kutafuta jinsi gani wengine hupanga muda wao, na kusoma vitabu na makala zinazohusiana na kupangilia muda, kutaendeleza ujuzi huu na kukupa mawazo bora.

Katika mabadiliko mengi ambayo unaweza kuyafanya katika kupangilia muda wako, kuna moja ambalo ni muhimu na rahisi kupatikana, na hilo ni kuamka mapema sana asubuhi. Punguza kuangalia TV usiku sana na jitahidi kulala mapema. Itakusaidia kuamka mapema.

Jitahidi uamke mapema angalau dakika 15 kabla ya wenzako. Muda huu unaweza kuutumia katika kusoma, kutafakari, kufanya mazoezi, au kupanga siku yako.

Kuepukana na zile fikra za kwamba hauna muda wa kutosha na hali ya kuwa kazi ni nyingi, jitahidi kuhisi na kufikiri kana kwamba una muda mrefu sana mbele yako.

Aina hii ya kutafakari au kufikiri inaweza kukuondolea uchovu na mawazo, na kukuwezesha kutizama kile unachotaka kufanya bila ya mawazo na uchovu.

Siku zote panga muda wako vizuri, usiupoteze kwa mambo yasiyo na maana, na usikawie. Fanya kila unachofanya kwa kadiri ya uwezo wako, kwa kutazama na kuwa makini juu ya unalofanya.

Staryte - Elimu, Burudani na Maendeleo
 
Asante kwa darasa zuri sana la kupanga muda. ni kweli kabisa ukiweza kupanga muda wako hakika mafanikio yapo mlangon
 
Moja ya mada bora kabisa ambayo nimesoma hapa JF.Bahati mbaya ,uzi ulikosa wachingiaji na hivyo ukawa mfupi.
Mleta mada, ubarikiwe sana.
 
Back
Top Bottom