Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 557
- 858
Zab 104:34 SUV
[34] Kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake; Mimi nitamfurahia BWANA.
Tunaweza kutafakari jambo kwa uzuri au kwa ubaya, inategemea umejikita haswa kwenye kitu gani wakati unafanya hivyo.
Mtu kuwa na mawazo ya kina juu ya Mungu ambayo tunasema ni kutafakari, ni kujua umuhimu wa Mungu katika maisha yake, mtu hawezi kupoteza muda mwingi akimtafakari Mungu akiwa hajuia nafasi ya Mungu katika maisha yake.
Mtu anapozama ndani kumtafakari Mungu na kazi zake, inaonyesha wazi mtu huyo anatoa nafasi kwenye moyo wake kujijenga zaidi na zaidi, kutafakari huko kunampa furaha na utamu kadri anavyozidi kuona yale Mungu ametenda katika maisha yake.
Ipo sababu ya kujenga mazoea ya kufikiri kwa kina kuhusu wema wa Mungu, uaminifu wake kwetu, kazi yake kwetu, vile amejitoa kwa mambo mengi, akitusaidia na kutuinua mahali tulikwama.
Kumtafakari kwetu kwa kina tunainua hisia zetu za ndani na kuleta furaha na upendo juu ya Mungu wetu, yapo mengi mtu atayajua, atakumbuka vile Mungu amemtetea na kumvusha katika maeneo mbalimbali.
Wakati mwingine tumekosa amani na furaha ya kweli ndani ya mioyo yetu kwa sababu tunatumia muda mwingi kutafakari matatizo yetu, kama tungegeuza uelekeo na kuanza kumtafakari Mungu kwa muda mwingi ingetusaidia kuwa na furaha nyingi.
Ukiwa na muda wa kusoma biblia na kutenga muda wa kutafakari yale umejifunza, unajijenga zaidi na kukaribisha vitu ambavyo watu wanavitafuta kwa gaharama yeyote ile, ila hawavipati kutokana njia wanazotumia kuvitafuta.
Ukitaka kupata amani ya moyo wako, ukitaka kuwa na furaha ya kweli, unahitaji kuwa na muda mwingi wa kumtafakari Mungu wako, kupitia kutafakari kwako Roho Mtakatifu atakuwa anakukumbusha na kukupitisha katika maeneo mbalimbali katika maisha yako, hasa yale ambayo Mungu amekusaidia mpaka kufikia hapo.
Kutafakari kunaweza kufanyika wakati wowote na mazingira yeyote, nafasi unayoipata unaweza kuitumia kumtafakari BWANA, itakuimarisha sana katika maisha yako ya kila siku.
Nitakuwa sijakutendea haki kama sitakukaribisha kwenye kundi hili zuri la wasap la kusoma biblia kila siku na kutafakari, ni moja ya kundi linaloweza kukusaidia kumjua Mungu wako vizuri kupitia neno lake. Ukipenda hili wasiliana nasi kwa wasap +255759808081 ili uweze kuunganishwa kwenye kundi hili zuri.
Mwisho, nikukaribishe kwenye channel ya wasap kupata maarifa mbalimbali bonyeza link hii kujiunga=>>Samson Ernest | WhatsApp Channel
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia yako
Mungu akubariki sana