echuma
JF-Expert Member
- May 20, 2010
- 311
- 80
Asilimia kubwa ya watu hutengeneza nembo(logo) kwa sababu tu wanahitaji biashara yao ionekane inanembo lakini umuhimu wake hawaujui.
Nembo ni alama maalum ya kwako peke yako inayokutambulisha sokoni na alama hiyo ndio
Itakuwa inasimama kwa niaba ya kampuni yako.hivyo alama hii inatakiwa kuwa
Iwapo vitu vyote hivi utavifatilia kwa umakini basi nembo yako itakuwa inafaa kuingia katika soko na ushindani, kwa sasa kumekuwa na wimbi la watu kuvamia weledi kwa vile tu wamejifunza kutumia program. Inahitaji utambuzi wa mambo ili utambue ni kipi kinafaa sio inahitaji ujuzi wa program ili ufanye kinachofaa.
Karibu Legacy Impresion Company tunatoa huduma ya kutengeneza nembo na kufanya graphic za aina zote,aina yetu ya ufanyaji wa kazi tunajielezea kama wabunifu tunaotengeza vitu kutokana na kuelewa matumizi yake, hata kama huelewi matumizi ya kitu unachotengeza tutakushauri na kukuelekeza ni kipi kinafaa kwa muda na wakati huo. bei zetu ni nafuu kulingana na huduma tunayotoa. karibu sasa upate elimu na utengeneze kinachofaa biashara yako
Mawasiliano
Web:.:LEGACY TANZANIA:.
Blog:legacycompany.blogspot.com
Fb page:legacy impresion Company
Email: info@legacytz.com
Phn: 0713603699

Vitu ambavyo vinatakiwa vionekane kwenye nembo yako
Nembo ni alama maalum ya kwako peke yako inayokutambulisha sokoni na alama hiyo ndio
Itakuwa inasimama kwa niaba ya kampuni yako.hivyo alama hii inatakiwa kuwa
- Iwe ya kipekee
- Inatakiwa iwasilishe uhalisia wa biashara ,bidhaa au huduma
- Iwe na uwezo wa kuonekana kwa wateja unaowategemea
- Iwe na uwezo wa kusimama na kujiimarisha muda hadi muda ( isipitwe na wakati)
- Iwe na uwezo wa kutumika na kuoneka kwenye kila nyanja ya mawasiliano
Iwapo vitu vyote hivi utavifatilia kwa umakini basi nembo yako itakuwa inafaa kuingia katika soko na ushindani, kwa sasa kumekuwa na wimbi la watu kuvamia weledi kwa vile tu wamejifunza kutumia program. Inahitaji utambuzi wa mambo ili utambue ni kipi kinafaa sio inahitaji ujuzi wa program ili ufanye kinachofaa.
Karibu Legacy Impresion Company tunatoa huduma ya kutengeneza nembo na kufanya graphic za aina zote,aina yetu ya ufanyaji wa kazi tunajielezea kama wabunifu tunaotengeza vitu kutokana na kuelewa matumizi yake, hata kama huelewi matumizi ya kitu unachotengeza tutakushauri na kukuelekeza ni kipi kinafaa kwa muda na wakati huo. bei zetu ni nafuu kulingana na huduma tunayotoa. karibu sasa upate elimu na utengeneze kinachofaa biashara yako
Mawasiliano
Web:.:LEGACY TANZANIA:.
Blog:legacycompany.blogspot.com
Fb page:legacy impresion Company
Email: info@legacytz.com
Phn: 0713603699
Katika matoleo yangu ya nyuma nilielezea vitu vinavyotengeneza biashara yenye afya na moja kati ya vitu hivyo ilikuwa ni nembo (Logo) leo nitaelezea kwa undani kidogo maana yake katika nyanja ya biashara na kwanini biashara inahitaji logo.
Logo/Nembo ni nini?
Nembo ni alama maalum inayokutambulisha sehemu fulani katika jamii, hiyo ni maana ya nembo kwa ujumla lakini nembo ( logo) maana yake haitofautiani sana na maana ya hapo juu,logo maana yake ni alama ya utambulisho wako katika biashara ambayo inatengenezwa kwa umakini na utaalamu maalum kwa ajili ya biashara yako.
Logo/Nembo inamaana gani kwako
Imekuwa kawaida kwa watu kutengeneza nembo mtu anapomiliki biashara basi anajua kitu cha kwanza ni nembo japo hajui inaumuhimu gani katika biashara nilishawahi kukutana na mmiliki wa biashara moja nikamuuliza kwanini ananembo katika biashara yake majibu yake ilikuwa ni " kama biashara lazima na mimi niwe na logo, na unapomiliki biashara nembo ni lazima ndio maana ninayo" nikamuuliza tena inakusaidia nini katika biashara yako alinijibu " inasaidia kwenye business card na invoice ndio naiweka pale inanionyesha professional katika ninachokifanya" hayo yanaweza kuwa ni mawazo yako pia kuhusu nembo au logo na ukweli ni kwamba hiyo sio maana ya nembo katika biashara yako.
Historia ya Logo/Nembo
Nembo au logo imeanza kutumika miaka mingi iliyopita ambapo matumizi yake yamekuwa yanabadilika kizazi hadi kizazi mwanzoni logo ilikuwa inatumika kama alama tu ya kuonyesha biashara kama ipo bila kuwa na maana nyingine na umuhimu mwingine .Baadae mambo yakaanza kubadilika zikaanza kutengeneza nembo/ logo ambazo zilikuwa zinaonyesha kazi ya biashara na kuitambulisha kwa wateja wake peke yake logo za kipindi hiki nyingi zilikuwa za kuonyesha kazi za biashara hivyo nembo hizo zilikuwa zinamabo mengi na zilikwa na kelele ( kwa maana ya kuonekana na vitu vingi ambavyo vinaonekana katika logo hiyo) hali imebadilika sasa hivi nembo sio alama ya kuonyesha kazi za biashara tena sasa nembo imehamia sehemu nyingine kabisa nembo ni alama inayokutambulisha katika wigo wa biashara .
Kwa kuangalia baadhi ya mapitio ya nembo hapo juu tangu ilipoanzishwa hadi leo hebu jiangalie kama mfanyabiashara nembo yako iko upande gani na uko zama zipi ? Na je uko sawia sehemu uliyopo? Nembo sio alama tu ya kuwekwa katika biashara au alama ya kukutambukisha kwa wenzako tu nembo inamaana kubwa zaidi ya hiyo ambayo watu wengi hawajui ila wanafanya tu, nembo yako leo hii inafanya vitu vifuatavyo katika biashara yako.
Toleo lijalo nitaeleza logo inatakiwa iweje na uifanyeje ili iendane na wakati pamoja na soko linavyohitaji.
Vitu ambavyo vinatakiwa vionekane kwenye nembo yako
- Iwe ya kipekee
Watu wengi wamezoea kuwa wanatengeneza logo kwa kuigilizia ya sehemu fulani au kwa kufuatisha mfumo wa kampuni fulani , wengine hufanya kama logo nyingine kisa tu ni kwa vile imempendezea machoni kwake au ameipenda bila kujali ujumbe utakaotoka baada ya hapo, nembo yako mara zote inatakiwa iwe ya kipekee na isifanane na nembo yoyote dunia nzima. Hasa katika soko ulilopo, unatakiwa kuifuata maana halisi ya nembo kama nembo ni utambulisho wako iweje uwe unafanana na utambulisho wa mwingine na iwapo umeigilizia kutoka kwa mwenzako inamaanisha tayari yeye brand yake ni kubwa kuliko yako hivyo ukitengeneza nembo inayofanana nayakwake ni kama vile unamsaidia kumkumbushia watu na kumtengenezea nafasi katika vichwa vya wateja wake. Mfano: leo hii ukipita sehemu ukaona nembo inayofanana na ile nembo ya brand ya cocacola utamkumbuka nini brand ya cocacola au brand ya yule aliyeitengeneza . Ukweli ni kwamba utaikumbuka cocacola na unaweza hata kuanza kujiuliza kama wamebadilisha nembo utabaki na maswali hata baadae unaweza kuigawa hiyo brand kwa mwingine sasa hivi cocacola wamebadilisha nembo wanatumia nyingine inatofauti kidogo na ile ya mwanzo. Tayari kwa namna moja au nyingine umeshaiua brand yako na umetengeneza tangazo la cocacola bila kujua.
- Inatakiwa iwasilishe uhalisia wa biashara ,bidhaa au huduma
Nembo yako haitakiwi kuwa nembo tu kama nembo,kwa vile nimesema hapo juu inatakiwa iwe ya kipekee sijamaanisha basi utengeneze nembo ambayo haina hata kiwango wala haina maana kwenye biashara yako inatakiwa nembo yako iwe na maana ndani yake ambayo maana hiyo inapatikana ndani ya nembo au jina la brand hii inasaidia kutokumpoteza mtu kutoka katika soko ulilopo mfano unahusika na usafirishaji sio lazima kenye nembo yako kuwe na magari, ndege au meli ilikuonyesha kwamba unahusika na usafirishaji unaweza kutengeneza nembo yako ikawa ni duara la dunia na alama ya mshale juu unaoonyesha kuzunguka dunia tayari utakuwa umetoa zile alama halisi kama gari na vyombo vya moto kwa kuweka alama ya mshale tu. Hivyo hakikisha nembo yako inawasilisha unachokifanya lakini sio lazima iwe kwa picha ya moja kwa moja.
- Iwe na uwezo wa kuonekana kwa wateja unaowategemea
Nembo sio alama tu unayoitengeneza kukutambulisha tu katika soko inatakiwa pia iwe na mawasiliano na mteja mtarajiwa iwe na uwezo wa kuonekana kwa wateja unaowategemea, mfano kwa mteja ambae anampango wa kusafiri nje ya nchi anapoona alama ya dunia na mshale katika logo yako na jina la kampuni ni comfort Transportation Company tayari kichwani mwake anahisi hili kampuni ni la usafirishaji sio ndani ya nchi tu hata nje ya nchi , hapo tayari kunakuwa na mawasiliano ya alama na hisia kati ya nembo na mteja wako bila ya wewe mwenyewe kuwepo. Nembo yako hakikisha inatosha kwenye macho yote mawili.
- Iwe na uwezo wa kusimama na kujiimarisha muda hadi muda ( isipitwe na wakati)
Nembo yako haitakiwi kuwa ya muda mfupi au ambayo inapitwa na muda unatakiwa kuwa na nembo ambayo inauwezo wa kujisimamia muda wote na inauwezo wa kukaa kwenye soko muda wote bila kupitwa na wakati mfano nembo ya brand ya maji ya Kilimanjaro ni nembo ambayo inaonyesha mlima, japo ni brand ya maji lakini imetumia brand nyingine (mlima) kujiongezea wateja na nembo yake haiwezi kupitwa na wakati hata kama mlima utapunguza theruji na kupungua urefu bado nembo itaendelea kusimama vile vile na haitapitwa na wakati , unatakiwa na wewe nembo yako pia iwe ya namna hiyo isiwe ile ambayo inapitwa na muda .
- Iwe na uwezo wa kutumika na kuoneka kwenye kila nyanja ya mawasiliano
Katika ulimwengu wa utandawazi nembo yako inatakiwa iwe na uwezo wa kuonekana kwenye kila nyanja ya mawasiliano isiwe logo ambayo ukiweeka sehemu fulani haiwezi kuaksi sehemu ilipo na mazingira yake logo ambayo ukiiweka sehemu inapoteza muonekano wake wa asili, hiyo sio aina ya logo unayotakiwa kuwa nayo au kuitumia kukutambulisha logo yako inatakiwa iwe na uwezo wa kuonekana vizuri kwenye kila nyanja za mawasiliano.
