SoC04 Umuhimu wa kuwa na sera ya kudhibiti vizazi vingi (Uzao mkubwa) Tanzania

SoC04 Umuhimu wa kuwa na sera ya kudhibiti vizazi vingi (Uzao mkubwa) Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

Kidagaa kimemwozea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
3,680
Reaction score
6,554
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi Tanzania, idadi ya watu ilifikia, 61,741,120(milioni sitini na moja, mia saba arobaini na moja elfu na mia ishiri) huku ikiorodheshwa kuwa miongoni mwa mataifa yenye idadi kubwa zaidi ya watu katika bara la Africa. Fauka na hayo , idadi kubwa ya watu Tanzania niwatoto chini ya miaka 15, wakitajwa kufikia asilimia 43%. Kubuniwa kwa sera ya kudhibiti vizazi vingi Tanzania nimchakato utakaoweka idadi maalumu ya watoto kuzaliwa kwa muunganiko mmoja wa baba na mama, mathalani inaweza kuwa watoto wawili au watatu , au kama itakavyoshauriwa na wataalamu.

Utekelezaji wa sera hiyo utatakiwa kwenda sambamba na ,
  • Kuongeza nguvu katika kuhimiza uzazi wa mpango katika familia; Uzazi wa mpango utasaidia kuepuka mimba zisizotarajiwa, kupunguza idadi ya watoto wa mitaani, pamoja na kutoa nafasi kwa wazazi kushiriki katika shughuli za kiuchumi na kuweza kulijenga Taifa letu
  • Kuweka mikakati mikali ya kudhibiti mimba za utotoni ; Mikakati hiyo itazuia pakubwa mimba kwa watoto wenye umri mdogo, na hivyo wasichana hao kupata muda wa kujishughulisha na masomo zaidi kuliko malezi katika umri mdogo. Mikakati hiyo nipamoja na kuzipa makali sheria zilizopo zinazohusiana na adhabu za ubakaji na kusababisha ujauzito kwa wanafunzi na watoto
  • Elimu itolewe kwa watanzania kuhusu umuhimu wa kuwa na idadi ndogo ya watoto katika familia na madhara ya kuwa na idadi kubwa ya watoto, hii itasaidia kujenga uelewa na kuondoa dhana potofu miongoni mwa watu hasa katika familia za vijijini
  •  Utayari miongoni mwa watanzania katika kukubali kutekelezwa sera ya kudhibiti vizazi vingi (holela) Tanzania. Bila utayari huenda sera hii ikakumbana na vikwazo vya kidini na kitamaduni hivyo kushindwa kutekelezeka, hivyo nimuhimu kila mwananchi kuwa nautayari katika kutekeleza jambo hili kwakuwa lina manufaa makubwa kwa taifa.
Sehemu inayofuata tunajadili umuhimu wa kuwa na sera ya kudhibiti vizazi vingi Tanzania.
Kama sera hiyo itatekelezwa kwa weledi tunatarajia kufaidika kama ifuatavyo katika miaka ijayo,

Mosi, Kupunguza uwiano wa umri tegemezi ; Uwiano wa umri tegemezi unapatikana kwa kujumlisha umri wa chini ya miaka 15 na zaidi ya 65 gawanya kwa watu wenye umri zaidi ya miaka 15 hadi 64 kuzidisha kwa 100 . Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Uwiano wa umri tegemezi ni 87.4 kwa Tanzania bara na Zanzibari ni 77.7 Uwiano huo unatokana na kuwa na idadi kubwa ya watoto Tanzania wenye umri chini ya miaka 15 ambao wapo katika kundi la utegemezi (wasioweza kuzalisha) huku wakiwa na mahitaji makubwa kama vile, malazi, elimu na mavazi. Taifa linapokuwa na idadi kubwa ya umri tegemezi nivigumu kuendelea kiuchumi kutokana na kuwa na wazalishaji wachache huku likiwa na wategemezi wengi. Hivyo kama sera ya kudhibiti vizazi vingi itaundwa na kutekelezwa kwa usahihi tutaweza kupunguza Uwiano wa vizazi tegemezi na kuwa na nchi yenye maendeleo makubwa kiuchumi.

Piramidi ikionesha idadi kubwa ya watu Tanzania ni watoto miaka 0-15

Screenshot_2024-06-18-22-19-50-36.jpg

Chanzo idara ya taifa ya takwimu katika kiungo hiki Census Information Dissemination Platform

Pili, Kuimarika kwa huduma za kijamii kama vile hospitali na shule; Kuwa na idadi ndogo ya watoto kutatoa nafasi kwa watoto waliopo kupata huduma bora za afya na elimu, pamoja na huduma mbalimbali zinazohitajika kwa watoto kama vile lishe bora. Kuwa na idadi kubwa ya watoto kunasababisha kukosekana kwa huduma au wazazi kushindwa kumudu mahitaji ya watoto jambo ambalo linaweza kusababisha watoto kudhoofu na kuongezeka kwa idadi kubwa ya vifo vya utotoni.

Tatu, Kuimarika zaidi kiuchumi ; Sera ya kudhibiti vizazi vingi itasaidia kutoa nafasi kwa wazazi kujishughulisha kiuchumi kwani watapata muda wakutosha wakujishughulisha kiuchumi kuliko kutumia muda mwingi katika kulea hasa kwa upande wa wanawake ambao hutumia muda mwingi katika kulea kuliko kujishughulisha kiuchumi. Hivyo sera hii ikiwa itaundwa itaweza kusaidia kukuza uchumi wa familia na taifa pamoja na kupunguza uwepo wa Kaya maskini Tanzania.

Nne, Sera yakudhibiti vizazi vingi , itasaidia katika Utunzaji wa mazingira; Kutokana na idadi kubwa ya watu Tanzania inakabiliwa na tishio kubwa la uharibifu wa mazingira unaoweza kufanywa na shughuli za kibinadamu. Kuwepo kwa sera ya kudhibiti vizazi vingi kutaleta ahueni kwa mazingira kuwa bora kwa faida ya kizazi hiki na vizazi vya baadae.

Hata hivyo kuundwa kwa sera hii kunaweza kukabiliwa na changamoto kubwa kama vile za kidini na kitamaduni kwani baadhi ya dini na tamaduni haziruhusu matumizi ya njia za uzazi wa mpango, vile vile bado kunalo kundi kubwa la watu ambao hawana uelewa kuhusu uzazi wa mpango. Nini kifanyike? Kwanza elimu inatakiwakutolewa kwa makundi yote pamoja na kuelezwa kina faida tunazoweza kunufaika nazo kama tutatekeleza sera ya kudhibiti vizazi vingi Tanzania, pia mchakato huu nimuhimu ukahusisha wataalamu wa demografia, wa ndani na nje ya nchi ili kufanikisha jambo hili kwa weledi.
 
Upvote 1
Ili kupigia kura chapisho hili Bofya sehemu ulivyoandikwa vote mwisho wa post
 
Back
Top Bottom