Data mining
JF-Expert Member
- Jul 10, 2022
- 406
- 484
Maelezo ya gari tiba linalo safiri
Kwa maelezo zaidi vituo afya vinavyo safiri ni magari maalumu yanayotoa huduma moja kwa moja kwenye jamii husika yakiwa na idara mbalimbali za matibabu na wataalamu wa huduma kutoka eneo moja hadi lingine. Ni magari ambayo yatakuwa yana safiri katika maeneo ambayo hakuna huduma za afya au huduma za afya zipo mbali kutoka kwenye makazi ya watu.
Umuhimu wa gari tiba linalotembea
upande wa malipo kutakuwa na mifumo ya bima ya afya kwa ngazi mbalimbali kwa wale wenye vipato vya chini,mfano mzuri chf(mfuko wa afya ya jamii),hapa mgonjwa anatakiwa pindi tu huduma ya gari tiba linalo safiri likifika anatakiwa awe nayo ili waataalamu waweze kutoa huduma kwa wakati kwa mgonjwa.
Malipo baada ya huduma kwa wagonjwa wa mjini
Changamoto.
Serikali iboreshe miundombinu yote ya mawasiliano ili jamii iweze kunufaika na huduma.
Kwa maelezo zaidi vituo afya vinavyo safiri ni magari maalumu yanayotoa huduma moja kwa moja kwenye jamii husika yakiwa na idara mbalimbali za matibabu na wataalamu wa huduma kutoka eneo moja hadi lingine. Ni magari ambayo yatakuwa yana safiri katika maeneo ambayo hakuna huduma za afya au huduma za afya zipo mbali kutoka kwenye makazi ya watu.
- Ni magari ambayo yatakuwa na idara za matibabu ndani na yatakuwa yana uwezo wa kutoa huduma maeneo mbalimbali ndani ya nchi kuanzia ngazi ya kata,wiliya na kitaifa.
- Ni magari ambayo yatakuwa na mitambo maalumu kwa ajili ya matibabu kwa wagonjwa mbalimbali
- Ni magari ambayo yatakuwa yaki safiri sehemu mbalimbali kutoa huduma.
Umbali wa vituo vya afya
Mara nyingi vituo vikubwa vya matibabu vipo katika miji mikuu aumaeneo yanayoendelea,hivyo basi wahitaji wa huduma ya matibabu wanakuwa wanapata shida kwenda kupata matibabu ya kina katika miji mikuu au mjini,kwa ujio huu wa magari tiba maalumu yanayo safiri yatasaidia watu wengi kupata huduma kwa wakati sehemu yoyote na muda wowote ili kuokoa uhai wa binadamu.
Kulemewa kwa huduma za afya
Vituo vingi vya afya vinaelemewa kutokana na wingi wa wagonjwa,hii inapelekea huduma kuwa mbovu na pia husababisha vifo kwa wale wagonjwa wanaohitaji huduma kwa wakati,idadi kubwa sana ya vifo inaongezeka kutokana na kuelemewa kwa kuduma kwenye vituo vya afya, pengine ni kwa sababu na kuwa na idadi ndogo ya wauguzi au wataalamu wa afya ndani ya kituo.
Huduma za afya kuwa chini ya kiwango kwa wahitaji
Mara kwa mara baadhi ya vituo vya afya vinakuwa na idadi kubwa ya wagonjwa ila utoaji wa huduma unakuwa upo chini ya kiwango kwa wahitaji,hivyo basi kwa miaka mingi changamoto za huduma za afya zimekuwa kubwa sana na kuleta utoaji wa huduma chini ya kiwango kwa wagonjwa katika maeneo tofauti ndani ya hospitali za wilaya na taifa.
Umuhimu wa gari tiba linalotembea
Itasaidia kupatikana kwa huduma karibu na jamii
Magari tiba yanayo safiri yatarahisisha upatikanaji wa huduma za afya karibu na kwa wakati katika maeneo mengi katika jamii,ikiwemo vijijini na mijini kwa wahitaji wa huduma kwa muda wowote.
Itapunguza vifo visivyo vya lazima
Ujio wa haya magari tiba yanayo safiri yatasaidia sana kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo visivyo vya lazima kwa wahitaji wengi wa huduma,ikiwemo kufika kwa wakati katika eneo ambalo lina mgonjwa.
Itarahisisha kupungua msongamano ndani ya vituo vikubwa vya afya
Huduma ya gari tiba linalo safiri itarahisisha kwa sana kupunguza msongamano wa wagonjwa hospitalini,gari hili linalotembea lita weza kusafiri sehemu ambazo wagonjwa wanapatikana kwa idadi kubwa au ndogo.kwa huduma hii ya gari tiba linalotembea litasaidia sana jamii kupata huduma sehemu yoyote na kuokoa Maisha kwa wakati ndani ya jamii.
Itasaidia makundi yote ya jamii kupata huduma kwa wakati.
Kuna makundi katika jamii wana ulemavu wa kudumu ambao ni vigumu kupata huduma za uwakika katika hospitali za taifa zilizo mbali na maeneo yao wanayo ishi,hivyo kwa hii huduma ya gari tiba linalotembea itaweza kufika sehemu yoyote kuhudumia makundi maalumu kwa muda husika.
Gharama za matibabu zitapungua
Changamoto kubwa hospitalini ni pale wagonjwa wanaposubiri kuhudumiwa na wataalamu wa afya kwa mda mrefu na pengine bila mafanikio,wakati mwingine ni pale wagonjwa wanatoka mbali kwa gharama kubwa ili kupata huduma katika vituo vikubwa vya matibabu,kwa ujio huu wa gari tiba linalotembea litarahisisha kutoa huduma ndani ya makazi ya watu na kuokoa gharama.
Jinsi gari tiba litakavyofanya kazi.
- Gari litakuwa na mifumo maalumu ya tehama inayowasiliana moja kwa moja na mifumo ya afya ya idara kuu inchini ili kuweza kuwa na kanzidata moja ambazo zina taarifa za wagonjwa,hii itasaidia wataalamu kuwa na taarifa za wagonjwa ili kutoa huduma kwa ufanisi zaidi.
- Gari litakuwa na mfumo maalumu ambao utawasaidia wataalamu kujua wagonjwa walipo.
- Gari litakuwa na mifumo wezeshi ya mawasiliano ya simu janja na simu kitochi ili kutoa huduma kwa watu wote wenye kuhijati huduma tiba katika maeneo wanayopatikana.
- Mgonjwa au mteja atalazimika kupiga simu kama hana uwezo wa kufika katika kituo cha afya pengine kipo mbali na makazi husika,hivyo wataalamu wa gari tiba watahitajika kujua taarifa sahihi za mteja wao mahali alipo,kutokana saivi inchi yetu kwa kiasi kikubwa maeneo mengi yana postikodi inayo rahisisha kwa haraka kujua makazi ya watu,hivyo basi wataalamu wa afya wataweza kufika kwa wakati ili kuokoa Maisha ya mgonjwa wao.
- Gari tiba litakuwa na vituo maalumu pale tu kama miundombinu itakuwa mibovu ,litalazimika kupiga kambi eneo ambalo haliwezi pitika ili kuruhusu familia yenye mgonjwa wao kufika eneo ambalo gari tiba lipo ili kupata huduma.
upande wa malipo kutakuwa na mifumo ya bima ya afya kwa ngazi mbalimbali kwa wale wenye vipato vya chini,mfano mzuri chf(mfuko wa afya ya jamii),hapa mgonjwa anatakiwa pindi tu huduma ya gari tiba linalo safiri likifika anatakiwa awe nayo ili waataalamu waweze kutoa huduma kwa wakati kwa mgonjwa.
Malipo baada ya huduma kwa wagonjwa wa mjini
Gari tiba linalo safiri lita kuwa na mfumo wa malipo kupitia simu janja ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa haraka kwa mgonjwa, kutakuwa na namba maalumu ya ulipaji wa matibabu ili kuruhusu malipo ya haraka kupitia simu za wateja.
Changamoto.
- Miundombinu ya usafirishaji kuwa mibovu.
- Ukosefu wa mawasiliano kwa maeneo ya vijijini
Serikali iboreshe miundombinu yote ya mawasiliano ili jamii iweze kunufaika na huduma.
Upvote
14