habilo mtweve
New Member
- Jul 27, 2022
- 1
- 2
UHIMU WA KUWEPO KWA DARASA MAALUMU KUHUSU ELIMU YA KUJITEGEMEA KWA VIJANA WA KITANZANIA
Ni hali ya kawaida sana kwa jamii ya kitanzania kuona kijana aliyehitimu chuo au masomo yake, au kijana yeyote yule ambaye jamii inategemea kumuona akianza kujitegemea au umri wake wa kujitegemea umefika ,lakini kijana huyo asiweze kujitegemea na matokeo yake kubaki kuwa tegemezi kwa wazazi wake, jamii na Taifa kwa ujumla.
Jamii ya watanzania bado haijaona kuna umuhimu mkubwa sana kwa Taifa kuwa na darasa maalumu litakalo mwezesha kijana wa kitanzania kujikimu au kuwa na uelewa wa kujitegemea mwenyewe baada ya kutoka kwa wazazi na kuingia katika maisha ya kwenye jamii.
Miaka ya nyuma enzi za mababu na mabibi zetu, jamii nyingi za kitanzania zilikua suala la Jando na Unyago kwa ajili ya kuwaandaa vijana kujitegemea na kujikimu na maisha binafsi mbali na malezi ya wazazi au walezi , lakini ni ngumu sana mfumo huo wa elimu kuanzishwa kwenye jamii hii ya kidijitali, maarufu kama kizazi cha kupyatila. Lakini kuna uwezekano elimu hiyo ikatolewa katika mfumo huu wa kidijitali kwa kutengenezewa mfumo maalumu kwa vijana kupata kozi hii ya elimu ya kujitegemea kwa vijana wa nchi nzima na matokeo yake tukaokoa wimbi kubwa la vijana wanaoshindwa kujitegemea baada ya kufikia ummri huo na mwisho wake kugeuka kuwa tegemezi kwa jamii na familia zao.
MTAZAMO KUHUSU MAANA YA DARASA MAALUMU LA ELIMU YA KUJITEGEMEA KWA VIJANA
Hii ni dhana inayoelezea kuwepo kwa darasa maalimu ambalo litakuwa likitoa mafunzo yanayomuanda kijana hasa wa kitanzania kwenda kujitegemea mara tu umri wa kujitegemea utakapo fika au mara tu baada ya kumaliza masomo yao , darasa hilo linapendekezwa kutolewa kwa kijana yeyote yule (vizuri kuanzia miaka 18), pasipo kujali kiwango cha elimu , dini , kabila wala chama, na darasa ambalo litafundishwa zaidi kwa vitendo kuliko nadhalia , huku likitoa elimu hiyo ya kujitegemea kwa kuzingatia mila , taratibu , hali ya uchumi , mifumo ya maisha , ya Mtanzania na jamii ya kitanzania kwa ujumla kumwezesha kijana huyu wa kitanzania kujikimu na kumjengea hali ya kujitegemea na kuwaondolea baadhi ya wasomi kasumba ya kwamba lazima waajiriwe ndipo waanze kujitegemea.
BAADHI YA MADHARA YA KUTOKUWEPO KWA DARASA MAALUMU LA ELIMU YA KUJITEGEMEA KWA VIJANA WA KITANZANIA
1. Ongezeko la vijana wengi wa kitanzania waliofikia umri wa kujitegemea lakini kubaki kuwa mzigo kwenye familia; wengi tunajua kuwa damu ni nzito kiliko maji kama watanzania wengi tumezoea kusema , hivyo kwa mila na taratibu zetu za kiafrika ni nadra kuona wazazi au walezi wakiwafukuza vijana waliofikia umri wa kujitegemea nyumbani watabaki kuwahimiza tu lakini kuhimizwa pasipo elimu maalumu ni vijana wachache tu watakaofanikiwa kutoka kwenye hilo wimbi na matokeo yake kubaki kuwa mzigo kwa familia
2. Kuibuka wimbi la vijana wanaokimbia familia wegine kutupa watoto kutokana na uoga wa kuhudumia familia au kulea familia;pia kwa miaka kadhaa ni rahisi sana kukutana na taarifa bza viajna kukimbia familia zao kwa uoga wa kuzilea au kuhudumia familia zao lakini uwepo wa darasa maalum kutasaidia kupunguza wimbi hili la vijana wanaotelekeza familia na wengine kutupa familia zao
3. Makundi ya kiharifu na wauzaji wa madawa ya kulevya huenda pia wakawa wanachangiwa ukosefu wa elimu hii; itambulike kuwa sio kila mfumo unaoanzishwa huwa unasaidia tatizo kwa asilimia mia moja lakini kuna namna mifumo hii saidizi huweza kupunguza tatizo mfano kufunguliwa kwa nyumba za matibabu kwa watu walioadhirika na dawa za kulevya hakujatibu vijana wote Tanzania ila imesaidia kupunguza tatizo ni imani yangu na huu mfumo utasaidia kupunguza tatizo hili.
BAADHI YA UMUHIMU WA KUANZISHWA KWA DARASA HILI LA ELIMU MAAALUMU YA KUJITEGEMEA
1. Itamsaidia kumuandaa kijana wa kitanzania jinsi ya kuanza maisha binafsi bila uwepo wa mzazi au mlezi; kwa maana kwamba hapa kijana sasa anafundishwa maisha au anaandaliwa yeye binafsi kuwa baba au mama wa familia, mume au mke, itambulike kuwa elimu hii itolewe bila kujali mila za kabila Fulani ila mila na taratibu zilizooeleka Tanzania nzima , ikumbukwe pia hapa kijana anayefundishwa ni kijana wetu ambae amezoea akitoka kutembea anakuta chakula cha wazazi bila uelewa binafsi wa yeye kujitfutia au kijana ambae yupo shule ameshazoea kutumiwa hela ya matumizi au kutumiwa hela ya kujikimu anayopewa na serikali ndio anaandaliwa kwenda kuanza maisha ya kujitegemea kwa kila kitu yeye binafsi.
2. Itaongeza chachu ya vijana katika ujasiliamali ; kijana baada ya kupokea elimu hii anaweza akaona kama kusubili ajira litamfanya azidi kuwa tegemezi kwenye familia hivyo itapelekea vijana wengi kuingia kwenye ujasilimali na kupunguza tatizo la uhaba wa ajira
3. Itasaidia kuandaa vijana kuwa wazazi na walezi bora pia kuwa viongozi wazuri , unampomuandaa kijana mapema aende kujitegemea inamjengea hali ya kujiamini na kujenga hoja , pia inamuongezea zaidi udadisi katika jamii na ii itamjenga kuwa mzazi au kiongozi bora hapo baadae.
PENDEKEZO NAMNA YA UANZISHAJI WA DARASA MAALUMU LA ELIMU YA KUJITEGEMEA KWA VIJANA
Ni vyema elimu hii ikaingizwa katika mfumo wa elimu moja wa moja huku ikitolewa pia katika kila kata au wilaya kwa kuandaa wataalamu maalumu watakao wanatoa elimu hii kwa vijna inaweza ikawa inatolewa kwa misimu huenda ikawa kila baada ya kipindi Fulani watalamu hao wanaenda katika sehemu hizo wanazopangiwa katika ukubwa ambao serikali utaona unafaa , huku kwa vijana ambao wapo katika mfumo wa elimu kuandaliwa darasa maalumu juu ya hii elimu au iingizwe katika mfumo wa elimu na kuwa kama somo , au kutolewa kama mfumo wa mafunzo ya Jeshi yanavyotolea , mfabo baada ya kuhitimu form four vijna hukaa mtaani zaidi ya miez sita had saba hapa vijana wangewekewa hata miezi miwili walau bila kujali ufaulu wao tena kwa umuhimu wa elimu hii itolewe pia bure na hata kupewa cheti kwa wahitimu wake ambacho pengine kingetumika kama kigezo baadhi ya sehemu kupata watu sahihi
HITIMISHO
Suala la kujitegemea kwa vijana wa kitanzania huwa halizungumziwi sana kwenye majukwaa na midaharo mbalimbali lakini ni suala muhimu sana kumuandaa kijana kwenda kujitegemea kwa kuwa mfumo wa elimu wa Tanzania haukutilia manani sana swala hili , uwepo wa darasa maalumu la kujitegemea itakuwa suluhisho la kudumu na mkombozi kwa kijana wa kitanzania ambae hajui aanzie wapo katika kujitgemea.

Upvote
3