SoC02 Umuhimu wa kuzingatia na kutekeleza sera za maji ili kutatua tatizo la uhaba wa maji

SoC02 Umuhimu wa kuzingatia na kutekeleza sera za maji ili kutatua tatizo la uhaba wa maji

Stories of Change - 2022 Competition

Theorist Mosses

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2022
Posts
345
Reaction score
253
Utangulizi
Binadamu tunahitaji vitu kadhaa ili tuweze kuishi, ni vitu muhimu sana katika maisha na kama tukivikosa binadamu hatuwezi kuendelea kuishi na ili tuishi lazima tupate maji.

Huduma ya maji hapa nchini, ilianza kutolewa tangu enzi za ukoloni katika miaka ya 1930. Ujenzi wa miradi ya maji kwenye vijiji ulianza mwishoni mwa miaka ya 1950, Utaratibu wa kuendesha huduma za maji mijini ulianza mwaka 1994. Ambapo mwaka 1998 mpaka 2005 zilianzishwa Mamlaka za Majisafi na Majitaka na hadi sasa kuna jumla ya Mamlaka 20 katika ngazi ya Miji Mikuu ya Mikoa na Mamlaka 109 katika ngazi ya Miji ya Wilaya na Miji Midogo pamoja na miradi ya Kitaifa 8.

Katika makala yangu nitazungumzia kuhusu mapungufu ya sera za maji katika kutekeleza na kusimamia usambazaji wa maji, kwa maeneo ya vijijini na mijini alafu mwishoni nitatoa mapendekezo kwamba nini kifanyike ili kutatua mapungufu katika sera za maji na changamoto kwa wananchi wote kwa ujumla.

Ufafanuzi
Sera, ni kanuni au muongozo uliowekwa kwaajili ya kusimamia na kutekeleza miradi kwa wakati katika utatuzi wa changamoto za wananchi. Uwepo wa sera mbovu za miradi ya maji hapa nchini ni chanzo cha huduma zenye mapungufu kwenye utekelezaji.

Sera ya Maji, ilikuwa na lengo la kuhakikisha wananchi wote wawe wamepata maji safi na salama kwa kiwango cha kukidhi mahitaji yao. Lakini kumekuwa na mapungufu ambayo yamesababisha migogoro sugu iliyo dumu kwa miaka mingi bila kutatuliwa na kusababisha wananchi kuwa na huduma mbovu za maji.

Mfano
Uchafuzi wa maji uliotokea mto mara march 2022, Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Seleman Jafo aliunda kamati kuchunguza chanzo cha tatizo hilo lakini baada ya majibu kuwasilishwa kwa wananchi, ilizua mjadala karibu nchi nzima kwamba sera za maji zilizopo hazitekelezwi.

Baadhi ya wabunge walikataa ripoti ya uchunguzi wa uchafuzi wa maji kuwa na rangi nyeusi na kusababisha vifo vya samaki katika mto Mara, ambayo ilikuwa chini ya Profesa Samweli Manyele na wajumbe wengine 10 na kuomba isiwekwe kwenye mtandao maalum wa serikali kwa kuwa maelezo yake ni ya aibu.

Baadae ilikuja kupelekea balozi wa Mazingira aliyekuwa akiwakilisha Bunge, Joseph Kasheku mbunge wa geita vijijini (Msukuma), kujiuzulu nafasi hiyo akisema ni aibu kuwa mwakilishi wakati aliyemteua ameunda ripoti ya hovyo.

Ni wazi kwamba mamlaka husika hazitekelezi sera zilizopo tatizo linalo sababisha wananchi wengi kuteseka. Maji yaliyopo kwenye taifa letu ni mengi sana kiasi kwamba taifa letu limebalikiwa hadi wanyama pori wa kila aina. Wanyama mbalimbali ndani ya taifa letu wanazaliana kwa kujivunia uwepo wa uoto wa asili na maji mengi kwenye mabwawa, mito, maziwa na bahari. Lakini watu ambao tuna watawala wanyama kwenye taifa letu tuna poteza maisha kwasababu ya uhaba wa maji ni wazi kwamba sera za maji ni batili.

Changamoto za uhaba wa maji
Tunapo zungumzia juu ya changamoto za wananchi zinazo takiwa kufanyiwa mabadiliko ndani ya taifa letu lazima kimoja wapo tutaje tatizo la uhaba wa maji. Mapungufu ya sera za maji zimesababisha changamoto hizo ndani ya jamii kwenye mikoa yote ndani ya taifa letu.

Kwa mfano kwenye mkoa wa dar es salaam, maji yamekuwa mgao na yanapatikana mara moja tu kwa wiki tena ni kwa bei ya gharama kubwa. Maji yamekuwa ya shida sana kwa wananchi, ikiwa ni kinyume cha sera za maji zilizowekwa ni kuhakikisha maji yanapatikana mara kwa mara kwenye maeneo yote nchini.

Asilimia kubwa ya wananchi, wamekuwa wakipoteza maisha na wengine wakipata magonjwa ya mlipuko kwa kutumia maji machafu yasiyo salama kwa afya zao. kwasababu ya mienendo mibovu katika utelekezaji wa sera zilizo wekwa ili kutatua changamoto za uhaba wa maji kwa wananchi. Changamoto za maji zimekuwa nyingi kwenye jamii zetu katika sehemu mbalimbali bila kupata suluhisho la kutatua changamoto hizo.

Haipendezi, taifa letu kuwa na changamoto ya uhaba wa maji hadi wananchi wengine wapoteze maisha au kunywa maji machafu ambayo ni hatari kwa afya zao. Kweli ni aibu sana kwenye taifa, Lazima kuna baadhi ya sera ambazo hazifuatwi na mamlaka husika ili kutekeleza kwa wakati kwenye usambazaji wa majisafi mijini na vijijini.

FB_IMG_16595234714843784.jpgFB_IMG_16595230530029254.jpgFB_IMG_16595227976987377.jpgFB_IMG_16595232058351043.jpgFB_IMG_16595231761922591.jpg
(Picha kutoka mtandaoni)​

Mapendekezo
• Serikali iweke bajeti ya usambazaji wa maji itakayo tekeleza huduma za maji kwa wakati. Mara nyingi ni kwa wananchi wanaoishi vijijini wamekuwa wakipata huduma za maji kwa shida. wananchi wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kutafuta huduma za maji, sisi kama taifa tuweke bajeti maalum itakayo tekelezwa kwaajili ya usambazaji wa maji nchi nzima. Bajeti za usambazaji wa maji nchini zitalenga kuwafikia wananchi ambao wanasafiri umbali mrefu kutafuta maji.

• Serikali ihakikishe Wananchi wanapata maji bure kwenye maeneo ya vijijini. Maeneo mengi ya vijijini ni sehemu ambazo kwa kiwango kikubwa kuna changamoto za uhaba wa maji. Ndani ya maeneo ya vijijini maji yamekuwa yakiuzwa kwa gharama za juu ukilinganisha na vipato vya wananchi wa vijijini ambavyo ni vidogo. Kwahiyo wananchi wa vijijini wapate maji bure kwenye mikoa yote ili kutekeleza sera zilizopo na kutatua changamoto za wananchi wa vijijini.

• Serikali ichukue hatua Kali za kisheria kwa viwanda vyote vinavyo mwaga kemikali na maji machafu kutoka viwandani kwenye vyanzo vya maji wanavyo tumia wananchi. Viwanda vingi vimekuwa vikimwaga maji machafu kwenye vyanzo vya maji wanavyo tumia wananchi kwenye mahitaji yao muhimu ya kila siku mfano kunywa, kuogea, kufulia, kupikia. kwahiyo umwagaji wa maji taka kutoka viwandani unawapa wakati mgumu wananchi na kusababisha uchafuzi wa maji na mazingira ikiwa ni kinyume cha sera za maji hivyo serikali ichukue hatua za kisheria kwenye viwanda.

• Serikali iondoe kodi zote kwenye huduma za maji kwasababu zimesababisha rushwa na utelekezaji mbovu wa huduma za maji kwa wananchi. Huduma ni mbovu sana zinazo sababishwa na Kodi nyingi kwenye maji. Ambapo viongozi wanao tegemewa na wananchi wamekuwa wakipokea rushwa kupitia mgongo wa kodi, Kwahiyo serikali iondoe kodi kwasababu zina sababisha mapungufu kwenye sera za maji ili kupunguza changamoto za maji kwa wananchi.

Hitimisho
Tatizo la uhaba wa maji ni aibu kwenye taifa kubwa kama Tanzania, lenye utajiri unaotosha kutatua changamoto za maji kwa wananchi wote. Taifa lenye malighafi za kutosha pamoja na uoto wa asili, wanyama, mafuta, gesi, madini, mlima mkubwa afrika Kilimanjaro, bila kusahau taifa letu limepakana na bahari kubwa ya hindi. Taifa limekuwa na watalii wengi kutoka mataifa mbalimbali sasa umaskini unatokea wapi, taifa letu ni tajiri Afrika.Tunahitaji tufanye mabadiliko ndani ya taifa letu mabadiliko yatakayo leta maendeleo.
 
Upvote 8
Ni ajabu sana karne ya 21 sisi bado tuna sumbuka na uhaba au ukosefu wa maji safi na salama kwa watanzania na wakati huo huo tunezunguka na mito, maziwa na vyanzo mbalimbali vya maji
 
Ni ajabu sana karne ya 21 sisi bado tuna sumbuka na uhaba au ukosefu wa maji safi na salama kwa watanzania na wakati huo huo tunezunguka na mito, maziwa na vyanzo mbalimbali vya maji
Yani wengine wapo bize kufanya masuala ya teknolojia sisi na utajiri wetu tumeamua kulala nao kitanda kimoja ni aibu.
 
Yani wengine wapo bize kufanya masuala ya teknolojia sisi na utajiri wetu tumeamua kulala nao kitanda kimoja ni aibu.
Hatari sana mkuu. Imagine tuna ziwa nyasa, ziwa Victoria, ziwa Tanganyika nk bado tuna mito mingi sana kila upande wa nchi yetu lakini ukifika sehemu kama handeni tanga kwa asilimia kubwa hakuna maji safi na salama. Ingewezekana haya mambo muhimu viongozi wetu wakayamakiza kabsa ili tuendelee mbele.
 
Haya mambo sizani kama yataisha kwa viongozi hawa tulio nao, kwanza ulisikia ile ripoti ya uchafuzi wa maji ya MTO Mara ?
 
Kwa wageni ambao ndiyo wamejiunga jinsi ya kunipigia kura gusa kiarama cha kijani chini ya post "^" kisha like post hii utakuwa umenipa nafasi ya kuwania ushindi.

Kura yako itasaidia chapisho hili kufika kitaifa ili viongozi wote waone changamoto zetu wananchi.
 
FB_IMG_16596849043602122.jpg

Bendera ya Tanzania ina rangi nne. rangi ya kijani inawakilisha uwaoto was asili uliopo Tanzania, rangi ya njano inawakilisha vivutio vilivyo Tanzania, rangi nyeusi inatuwakilisha sisi watanzania, rangi ya bluu inawakilisha uwepo wa maji Tanzania.

Kwahiyo Tanzania ni nchi tajiri siyo taifa la kupoteza RAIA wake kwenye uhaba wa maji, kama unaipenda Tanzania na unahitaji kuona mabadiliko pigia kura chapisho hili gusa kimshale "^" chini ya post kisha like post utakuwa umepigia kura chapisho hili lifike kitaifa.
 
Sijaifuatikia haya ilisemaje.?
FB_IMG_16593026060737030.jpg
Kulikuwa na uchafuzi wa maji mto mara, uliosababishwa na utiririshaji wa maji machafu yenye kemikali kutoka viwandani. ilipelekea maji kujaa kemikali za viwanda na kusababisha uhaba wa maji kwenye eneo hilo kwa upande wa wananchi.

Ndipo ikaindwa kamati ya uchunguzi wa tatizo hilo majibu yaliyo kuja ni kwamba, wanasema chanzo cha maji kuchafuka ni vinyesi vya ng'ombe vilivyo rundikana ndani ya maji, ndivyo vilivyo pelekea maji kuharibika mpaka samaki kufa.

Ripoti hii baadae serikali ilikuja kupinga kwamba ni ripoti ya hovyo ilipelekea mpaka kiongozi mkubwa wa serikali mbunge msukuma, kujiuzulu kwa sababu ya ripoti ya uongo.

Kama kwenye mamlaka kubwa ya maji Tanzania kuna mambo ya hovyo kama hizi vipi kuhusu mamlaka ndogo ndogo za wilaya na vitongoji zenye kusimamia huduma za maji safi na salama, unazani kuna uwajibikaji wa Sera za maji hapo ?
 
Unajua serikali yote wanaweza kusafiri kwa wakati moja kutoka Africa mpaka marekani ( USA).

FB_IMG_16597113925386192.jpg

Sijaifuatikia haya ilisemaje.?

Lakini kutoka ziwa Victoria mpaka tanga ni( 1126miles ) tu, kwaajili ya wananchi wa tanga ndiyo haiwezekani kwa serikali ?
Lakini kubeba maji kutoka ziwa Victoria mpaka tanga kwaajili ya wananchi hawawezi, unajua serikali jukumu lake kuu ni kutatua changamoto za wananchi.

Ni aibu sana kwenye taifa, ni viongozi wachache sana wenye uwajibikaji kama JPM, yeye alikiwa anatembea nyumba kwa nyumba mkoa kwa mkoa kuwasikiliza wananchi na kutatua shida zao.

Leo hii viongozi tulio wachagua hatuwaoni majimboni, tunaishia kuwaona tu kwenye Television (TV) mara, wameenda marekani, wakati wananchi tuliwaamini na kuwapa kura zetu waje watatue shida zetu
 
View attachment 2315248Kulikuwa na uchafuzi wa maji mto mara, uliosababishwa na utiririshaji wa maji machafu yenye kemikali kutoka viwandani. ilipelekea maji kujaa kemikali za viwanda na kusababisha uhaba wa maji kwenye eneo hilo kwa upande wa wananchi.

Ndipo ikaindwa kamati ya uchunguzi wa tatizo hilo majibu yaliyo kuja ni kwamba, wanasema chanzo cha maji kuchafuka ni vinyesi vya ng'ombe vilivyo rundikana ndani ya maji, ndivyo vilivyo pelekea maji kuharibika mpaka samaki kufa.

Ripoti hii baadae serikali ilikuja kupinga kwamba ni ripoti ya hovyo ilipelekea mpaka kiongozi mkubwa wa serikali mbunge msukuma, kujiuzulu kwa sababu ya ripoti ya uongo.

Kama kwenye mamlaka kubwa ya maji Tanzania kuna mambo ya hovyo kama hizi vipi kuhusu mamlaka ndogo ndogo za wilaya na vitongoji zenye kusimamia huduma za maji safi na salama, unazani kuna uwajibikaji wa Sera za maji hapo ?
Duuh hatari. Vinyesi vichafue maji. Aisee ngumu kuikubali ripoti hiyo. Walivyoikataa walikua sahihi
 
Unajua serikali yote wanaweza kusafiri kwa wakati moja kutoka Africa mpaka marekani ( USA).

View attachment 2315271

Lakini kutoka ziwa Victoria mpaka tanga ni( 1126miles ) tu, kwaajili ya wananchi wa tanga ndiyo haiwezekani kwa serikali ?
Lakini kubeba maji kutoka ziwa Victoria mpaka tanga kwaajili ya wananchi hawawezi, unajua serikali jukumu lake kuu ni kutatua changamoto za wananchi.

Ni aibu sana kwenye taifa, ni viongozi wachache sana wenye uwajibikaji kama JPM, yeye alikiwa anatembea nyumba kwa nyumba mkoa kwa mkoa kuwasikiliza wananchi na kutatua shida zao.

Leo hii viongozi tulio wachagua hatuwaoni majimboni, tunaishia kuwaona tu kwenye Television (TV) mara, wameenda marekani, wakati wananchi tuliwaamini na kuwapa kura zetu waje watatue shida zetu
Huku mbali saana ipo mito mingi inatiririsha maji mengi masafi kutok kaskazini kwenda pwani mfano kuna mto ule unaotoka Kilimanjaro hadi kufikia pwani ya bahari ya hindi
 
Itabidi mamlaka husika zifuate Sera za maji zilizopo ili kutekeleza huduma ya maji kwa wananchi
Kweli. Haya ya muhimu ingependeza zaidi kama yaki tatuliwa kwa haraka ili kuondoa adha za ukosefu wa maji
 
Back
Top Bottom