SoC01 Umuhimu wa lishe bora katika afya ya akili kwa watoto

SoC01 Umuhimu wa lishe bora katika afya ya akili kwa watoto

Stories of Change - 2021 Competition

David M Mrope

Senior Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
115
Reaction score
74
Lishe bora ni aina mbalimbali za michanganyiko ya vyakula ambavyo hufanya kazi mbalimbali katika mwili wa binadamu. Swala la lishe kwa watoto hasa katika nchi zinazoendelea limekuwa ni changamoto kubwa. Hii hutokana na watu kula chakula kitachopatikana katika siku hiyo,na hii hutokana na hali ya kiuchumi.

Sasa, akili ya mwanadamu hupimwa kwa namna tofauti tofauti,ikiwemo uwezo wa kuelewa kitu,kukariri kitu,kuchambua kitu,kutengeneza kitu n.k. Sasa ili mtu awe na akili bora lazima awe na uwezo wa kuyafanya hayo mambo kwa pamoja,yaani aelewe,akariri,achambue na awe na uwezo wakutengeneza kitu chake binafsi.

Kazi zote hizi hufanywa na ubongo wa mwanadamu. Kumbuka ubongo wa mwanadamu huanza kuundwa kipindi cha awali kabisa katika utungwaji wa mimba,na uendelea kukua mpaka pale mtoto anapozaliwa. Ubongo hukua kutokana na mazingira. Ni kama kioo tuu kama ukikichekea nacho kitakuonesha tabasamu.

Sasa watoto wanapokuwa na lishe duni hupelekea ubongo kushindwa kukua vizuri na ukubwani kushindwa kutimiza kazi zake kwa ubora. Japo kuna sababu zingine zinazoelezea akili ya mtoto kama mazingira na vinasaba,lishe pia inaongoza kusababisha udumavu wa akili.

Mtoto anayepatiwa lishe bora hasa aina ya protini husaidia kujenga mwili pamoja na ubongo. Vyakula vya protini ni kama vile maharage,mayai,maziwa,nyama n.k. Vyakula hivi ni muhimu sana kwa watoto kwa ajili ya kuijenga afya yake pamoja na akili.

Matatizo mengine yanayosababishwa na ukosefu wa lishe bora.

(i) Matatizo ya ukuaji.
Mtoto yeyote ambaye lishe yake bado ni duni,basi huwa na matatizo ya ukuaji. Ili mtoto akue vizuri lazima kuwe na protini yakutosha ambazo pia hufanya kazi ya kuujenga mwili. Watoto wengi kabla ya miaka miwili hukua haraka haraka kutokana na protini nyingi wapatazo kutoka kwa maziwa ya mama. Lakini baada ya kuacha kunyonya watoto hawa wameonekana wakiwa na afya duni kabisa. Hii husababishwa na uhaba wa lishe bora.

(ii) Kushuka kwa kinga za mwili.
Pia mara nyingi mtoto anakuwa anasumbuliwa na magonjwa mbalimbali. Magonjwa hayo hupata nafasi kutokana na kushuka kwa kinga za mwili. Mwili huweza kupambana na magonjwa kama tu atakuwa na kinga imara. Kinga hizi hutokana na lishe bora.

(iii) Mtoto kuishiwa nguvu.
Hii huwakuta watoto wengi sana,ambao mara nyingi hukonda kupita kiasi. Mwili uhitaji vyakula kama vile wanga,protini na mafuta ili uweze kuzalisha nguvu. Ukosefu wa vyakula hivi humfanya mtoto kukosa nguvu.

(iv) Uzito uliopitiliza.
Hii mara nyingi husababishwa na ulaji horera wa vyakula hasa vya nafaka. Kama mtoto akila ugali,wali,ngano n.k kwa muda mrefu basi anauwezekano mkubwa wa kupata hili tatizo.Nafaka ikishajaa mwilini kwa wingi mwili hutuma taarifa ambayo huufanya mwili kuacha kuzalisha nishati, na kile kiasi cha wanga kilichopo tumboni hugeuzwa kuwa mafuta. Na kumfanya mtoto kuwa na uzito mkubwa. Hili tatizo huathiri akili pia.

Hivyo ni vyema watoto wakapatiwa lishe bora kwa ajili ya ukuaji chanya wa akili zao lakini pia kuwaepusha na matatizo mengine.

DAVID M MROPE.
SUA.
 
Upvote 5
Lishe bora yenye protini ya kutosha ina gharama kubwa sana kwa maisha ya mtanzania.
Mleta mada na wadau sasa katika hili wajuvi mngeanza kutupa orodha na mpangilio wa lishe bora kulingana na vinavyopatikana mazingira ya kawaida. Nilichogundua lishe bora si suala la uwezo, ni ufahamu. Mungu alishaturahisishia vyakula muhim ndo cheap!
Case study ya njombe/iringa na kagera na kiwango cha utapiamlo inafikirisha sana kwa namna walivyobarikiwa vyakula vya kujilimia.
 
Mleta mada na wadau sasa katika hili wajuvi mngeanza kutupa orodha na mpangilio wa lishe bora kulingana na vinavyopatikana mazingira ya kawaida. Nilichogundua lishe bora si suala la uwezo, ni ufahamu. Mungu alishaturahisishia vyakula muhim ndo cheap!
Case study ya njombe/iringa na kagera na kiwango cha utapiamlo inafikirisha sana kwa namna walivyobarikiwa vyakula vya kujilimia.
Ni sahihi lakini uchumi bado ni changamoto, mfano watu wa kanda ya ziwa wakivua samaki wale wakubwa wanapeleka sokoni badala ya kupikia watoto.
 
Ni sahihi lakini uchumi bado ni changamoto, mfano watu wa kanda ya ziwa wakivua samaki wale wakubwa wanapeleka sokoni badala ya kupikia watoto.
Hili bado sio tatzo la kiuchumi. Ni la kiufaham zaid. Kuvua tu samak, awe mkubwa awe mdogo , tayar kuliwa ni rahis. Tofaut na angekuwa jangwan. Inahitajika sensitization kubwa. Kampeni kubwa.
Yan jamii ifike mahali.ile kwa sababu. Wengi vitu vya lishe vimetuzunguka katika ardhi zilizopo tayar lakin kuona ulazma na umuhim ndo tatzo.
Mfano mdogo ni je ni familia ngap wana ardhi na muda na nguvukaz hasa vitoto vya shule lakin hawana bustan ya mboga za majan kwa ajir ya familia? Hili sio la umaskin labda umaskin wa akili
 
"Nafaka ikishajaa mwilini kwa wingi mwili hutuma taarifa ambayo huufanya mwili kuacha kuzalisha nishati, na kile kiasi cha wanga kilichopo tumboni hugeuzwa kuwa mafuta. Na kumfanya mtoto kuwa na uzito mkubwa. Hili tatizo huathiri akili pia."
Nilipay attention hadi hiki kipengele kilipofika [emoji1] [emoji1787]...
Kapitie tena vizuri notsi mkuu...
 
Back
Top Bottom