Luqman Van Maliki
Member
- Aug 19, 2021
- 6
- 7
Afya ni kitu cha kwanza muhimu kabisa kuliko vyote katika uhai wa mwanadamu. Mtu akikosa afya bora hata kamanakiwa na utajiri wa hadhina za dunia yote bado atakuwa hana furaha ya kufurahia mambo hayo nanutajiri huo. Msingi wa maisha ya binadamu upo katika afya njema.
Vyakula vingi kwa sasa vimekuwa vikileta athari kubwa katika afya ya wanadamu yote hii ni kwa sababu watu na jamii nyingi nchini zinashindwa kuelewa na kutambua umuhimu wa kupata lishe bora na kufanya mazoezi ili kuboresha na kutunza afya zao.
Maisha ya mwanadamu yeyote duniani yanategemea afya njema ya mwili wake ili aweze kuwa na furaha ya maisha na kama mtu akikosa afya njema ataishi kwa matumaini na hofu ya kukiogopa kifo na kuyaona maisha hayana maana tena kama kwamba mgonjwa wa virusi vya ukimwi anavyoishi kwa matumaini.
Siku hizi msingi mkuu kabisa wa matatizo ya magonjwa mengi nyemelezi yanatokana na ulaji mbovu usiofaa wa vyakula na ukosefu wa lishe bora na kutokunya mazoezi.
Wataalamu wa afya wanaeleza lishe bora ni kila kitu kwenye afya ya mwanadamu japo jamii nyingi nchini zinakabiliwa na umaskini uliokithiri hata kushindwa kuendana na mpangilio unaofaa kuhusu chakula na lishe bora na kutenga muda kwa ajili ya mazoezi ya kuweka mwili sawa.
Karibu kila kaya nchini hasa maeneo mengi ya mijini na kwa uchache vijijini kunakabiliwa na tatizo la magonjwa nyemelezi yasiyo ya kuambukiza kwa lugha ya kitaalamu yanajulikana kama (Non-communicable disease) ambayo ni kama vile magonjwa ya moyo, ini, figo na presha haya yote yanakuja baada ya mtu kutumia chakula kwa muda mrefu bila kufuata utaratibu wa lishe bora na kutokufanya mazoezi kwa muda mrefu na utumizi wa chakula kisichofaa au kuhitajika mwilini.
Watu wangeweza au kuongeza jitihada kidogo kwa kutumia chakula kwa misingi ya ufuataji mpangilio wa lishe bora ungesaidia kwa kiasi kikubwa uzuiaji wa magonjwa nyemelezi yasiyo ya kuambukiza.
Jamii zingekuwa na elimu kuhusu ulaji unaofaa afya za watu wengi zingekuwa imara kwa sababu kama mtu akila mchanganyiko wa chakula mbalimbali anapata vitu muhimu au aina yote ya makundi ya chakula kama vile protini, wanga, kabohaidreti na makundi yote yaliyosalia.
Mwili ukipata makundi yote ya chakula na kuzingatia misingi ya ulaji unaofaa unaweza usipate magonjwa nyemelezi pia itasaidia sana ukuaji wa mwili hasa kwa watoto wadogo wanaoendelea kukua, sababu mtoto mdogo akikosa lishe bora wakati wa ukuaji wake anawezakudumaa mwili kwa kupata utapiamlo (kwashiorkor) na udumavu wa akili akawa na uwezo mdogo kabisa wa kufikiri baadaye.
Wataalamu wa afya wanahamasisha sana ulaji wa mbogamboga, karibu kila kituo cha afya kinahamasisha juu ya ulaji wa mbogamboga.
Huku Kina mama wenye watoto wachanga umri kati ya miezi sifuri hadi sita ya mwanzo wanaendelea kuhamasishwa wasiwape chakula chochote watoto wanatakiwa kupewa maziwa ya mama pekee ambayo yana virutubisho vyote kwa ajili ya mtoto.
Matatizo yanayotokana na ulaji usiofaa na kukosa lishe bora yamekuwa yakiongezeka kwa kiasi kikubwa hasa maeneo ya mijini ambapo upatikanaji wa vyakula vingi visivyohitajika sana mwilini kama vya mafuta na sukari vimekua vikitumika zaidi. Huku ulaji uliokithiri wa vyakula hivyo humkokota mtu hata akapata magonjwa ya moyo, sukari, figo na presha.
Kimsingi ulaji usiofaa ni hatari sana kwa afya ya mtu hasa watu wanapenda kula sana vyakula vyenye ladha nzuri mdomoni. Mwili unachukua tu kiasi cha chakula kinachohitajika na kufanya chakula kingi kisiwe na matumizi ndani ya mwili. Mabaki mengi ya chakula yanaweza kuathiri afya ya mwili.
Mtu anayekula chakula kingi anatakiwa afanye mazoezi kila siku ili kulazimisha mabaki ya chakula kilichozidi kiweze kutumika na kufanyika mmeng'enyo wake haraka, endapo asipofanya mazoezi ataweza kukaribisha magonjwa nyemelezi kama sukari au moyo na kupata unene uliokithiri.
Ufanyaji wa mazoezi unashauriwa kila siku kwa wataalamu wa afya na lishe huku madaktari bingwa wote kwa sababu unasaidia kuuweka mwili sawa kuepukana na magonjwa nyemelezi yanayotokana na ulaji usiofaa na kukosa lishe bora
Ulaji wa mbogamboga na vyakula vinavyotokana na nafaka asilia,matunda, vyakula vya protini kama mayai maharage na nyama vinahitajika sana kwenye mwili wa binadamu.
Mambo yote kuhusu afya bora hayawezi kupatikana au watu wataendelea kushindwa kufuata utaratibu na ulaji unaofaa wa kupata lishe bora bila kugundua madhara wanayoendelea kuyapata lakini zaidi elimu kubwa kuhusu mambo hayo inahitajika kutolewa ili watu wote wajue madhara ya ulaji usiofaa na kukosa lishe bora na uvivu wa kutozingatia mazoezi kunaweza kuathiri kiasi kikubwa affya zao.
Sekta zote zinazohusiana na maswala ya lishe na vyakula kama TFDA kwa Tanzania bara na ZFDA kwa Zanzibar kwa kushirikiana na wataalamu wa lishe na afya wanayodhima ya kuendelea na kuongeza juhudi kuwafundisha watu kwa lengo la kuwaeleza kwa kina faida na madhara ya ulaji usiofaa na ukosefu wa lishe bora na kutokufanya mazoezi ya mwili kunavyoathiri afya zao.

Upvote
3