Umuhimu wa madini ya Calcium kwenye mifupa

Umuhimu wa madini ya Calcium kwenye mifupa

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Mifupa huupa mwili muonekano wake halisi pamoja na kulinda baadhi ya viungo vyake.

Aidha, hufanya kazi ya kutunza baadhi ya madini na virutubisho vya mwili, pia ni sehemu ambayo mwili huitumia katika kutengeneza damu.

Ili mifupa iweze kufanya kazi zake vizuri ni lazima iwe na kiasi cha kutosha cha madini ya Calcium ambayo asilimia 99 ya kiwango chote cha madini haya kinachopatikana mwilini hutunzwa humo.

50AB2470-989D-47E3-8E09-4592831F5907.jpeg


Calcium huongeza ubora na ujazo wa meno na mifupa, hupunguza changamoto ya kusagika na kuvunjika kirahisi kwa mifupa pamoja na kusaidia kuunganisha ile iliyo vunjika.

Kiwango cha kawaida cha uhitaji wa kila siku ni 1000 mg na hupatikana kwa wingi kwenye maziwa pamoja na bidhaa zake, samaki, bamia, spinach, broccoli pamoja na maharage ya soya.

Upungufu wake husababisha kupungua ujazo na kuvunjika kirahisi kwa mifupa hasa kwa wanawake waliofikia umri wa ukomo wa hedhi, kuharibika kwa meno, kupungua kwa mijongeo ya misuli pamoja na kusagika kirahisi kwa mifupa hasa ile ya maungio ya mwili.

Chanzo: National Institutes of Health (Office of Dietary Supplements)
 
Back
Top Bottom