Umuhimu wa mboga mboga & Matunda

Umuhimu wa mboga mboga & Matunda

Jesusfreak08

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2019
Posts
822
Reaction score
1,803
Kutokana na tafiti ambazo zimefanywa na watu mbalimbali wanasayansi mbalimbali duniani (ndani ya Africa na nje ya Africa) wamekuja kugundua kuna umuhimu mkubwa sana wa mboga mboga hasa mboga mboga asilia kama mchicha ,ngogwe ,mgagani.

Kwanini zina umuhimu kwasababu zimebeba virutubisho muhimu ambavyo vinahitajika kwenye mwili wa mwanadamu ambavyo vinaweza kuzuia magonjwa kwa watoto na wazee kwa kuwaongezea kinga katika miili yao

Lakini kutokana na mtazamo hasi kuhusiana na mboga mboga hizi kuwa ni za watu wa hali duni kimaisha na kutoa vipaumbele kwa vyakula kama nyama na vitu vya viwandani (chololate n.k) na vitu vinavyofanana na hivyo.

Na uzuri wa hizi mboga sio kwamba ni gharama kupanda au kuzitunza kwaajili ya matumizi ya nyumbani hapana kwasababu zinachukua eneo dogo hata mbegu sio gharama kama mbegu za mazao mengine ni nirahisi katika upatikanaji wake

Jaribu kufanya hivi kwa faida yako binafsi na kwaajili ya wengine pia.
 
Mboga 7 zote za Majani mchicha tembele figili chainizi mnavu mlenda ukila kwa utaratibu mzuri sahau Kusumbuliwa na bathi ya magonjwa mbl mbl
 
Vizuri sana. Tena ukilima mwenyewe unapata za kutosha na ambazo ni salama. Hazijamwagiwa maji machafu na kupigwa dawa kali.
IMG_20200724_081536.jpg
 
Back
Top Bottom