Mwaka jana nilikua napiga story na mama fulani na hiyo ilikua ni siku yetu ya kwanza kukutana, katikati ya maongezi nikamwambia mipango yangu na kwamba sijui sana kuhusu hiyo ishu ila nataka kujaribu.
Kumbe mme wake anafanya hizo ishu, yule mama akaniahidi kuniunganisha na mme wake kwa muongozo zaidi.
Week iliyofuata nikakutana na mme wake, nilishikwa na butwaa kwakweli, kwa bongo ni kama mtu akwambie nakuunganisha na mtu fulani kumbe huyo mtu ni Mo Dewji (anaweza asiwe na ukwasi kama Dewji ila ana mawe ya kutosha tu).
Yule mzee nawasiliana nae toka siku ile hadi leo kama navyowasiliana na masela tu, mtu poa sana. Hii sio bongo.
Kwa mazingira ya Bongo ni kazi sana mtu akuchukue under his/her wing kukufanyia mentorship tena bure.
Aidha Knowledge is NOT power. Knowledge is only POTENTIAL power. Action is power.
Unaweza kusoma vitabu vyote duniani ila kama hutofanyia kazi utakufa masikini.
Experience is the best teacher, wakati unasoma uwe field kufanyia kazi mawazo yako, usipoteze muda sana kusoma hayo mavitabu maana hakuna point itafika ambayo utaona umeiva na no two situations are the same. Njia aliyopitia mentor wako inaweza kuendana na yako ila haziwezi kufanana.