Umuhimu wa Mipango: Kushindwa kujipanga na kujipanga kushindwa

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Habari za asubuhi

Leo nataka nilete hoja ambayo najua wengi wetu tunaifahamu ambayo inaitwa Planning,katika biashara na katika maisha.Wahenga wamewahi kusema KUSHINDWA KUPANGA/KUJIPANGA ni KUJIPANGA KUSHINDWA.

Watu wengi huwa ama wanadharau au hawaoni umuhimu wa kutumia wataalamu au watu wengine katika kufanya mipango yao.Wengi wanaamini katika uwezo wao na uzoefu wao na wakati huo huo hawana uelewa wa kutosha juu ya uwezo wao.Katika maisha na katika biashara ni vyema ukajenga tabia ya kuwa na mipango ya muda mfupi,wa kati na muda mrefu.Ni lazima uweke mazingira wezeshi katika kuhakikisha kwamba unafikia malengo.

Kupanga linapaswa kuwa zoezi endelevu katika maisha yako.Hii ni kutokana na ukweli kwamba,nyakati inabadilika,fursa mpya zinajitokeza ,mahitaji na changamoto mpya zinabadilika,uelewa wako unabadilika.Kile ambacho kilikuwa sahihi jana kinaweza kisiwe sahihi leo au kesho hivyo basi usifikiri kwamba mipango ni namna ya kukwepa majukumu kwa kusema sio sehemu ya malengo yangu.

Unapaswa kuwa na mpango wa matumizi ya muda wako kuanzia saa,siku,wiki,mwezi na hata mwaka.Unatakiwa kuwa na mpango wa matumizi ya pesa zako kuanzi 1000,10000 hadi bilioni kadhaa,Unatakiwa kuwa na mpango juu ya afya yako,familia yako n.k.Kwa ufupi unatakiwa kuwa na mpango hata katika kula tunda kwa masihara vinginevyo unaweza kweli kukutana na masihara.

Swali la kujiuliza ni je unawezaje kufanya mipango ya maisha ,muda,biashara etc ?Ukweli ni kwamba kwa kujipnga vizuri,jambo ambalo ungetumia siku kulifanya unaweza kutumia nusu saa kulifanya.Yaani kwa kuwa ni mipango thabiti utakuwa na uwezo wa kutumia rasilimali zako vizuri na kwa kiwango kidogo na kupata matokeo makubwa.Hivyo basi usifikiri kwamba muda unaotumia katika kupanga unapotea,Usifikiri gharama unazotumia katika kupanga zinapotea hapana,kwa kujipanga utajikuta ukiokoa gharama na muda na kupunguza au kuondosha hasara.

Kwa mafano watu wengi huanza biashara bila kufanya utafiti wa kina kuhusu aina ya biashara,faida,mauzo n.k. hujipa matumaini kwa kutazama watu wengine wanaofanya biashara kama hio bila kufanya utafiti wa kina.Matokeo yake huingia katika biashara wakiwa na upofu na kujikuta wakipata hasara maradufu wakati kama wangeamua kutumia muda kidogo na gharama na wataalamu katika katika kufanya utafiti wa kina kuhusu kile wanachotaka kufanya wangejikuta wanaokoa kiasi kikubwa sana cha PESA na MUDA.

Tujadili hapa leo ni namna gani unafanya mipango yako na kwa kiasi gani unafikiri kujipanga kumekusaidia zaidi katika kufikia malengo yako.Karibuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…