SoC02 Umuhimu wa mwanaume kuwa kama Afisa Uchumi wa familia

SoC02 Umuhimu wa mwanaume kuwa kama Afisa Uchumi wa familia

Stories of Change - 2022 Competition

Chakudeka6

New Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
1
Reaction score
1
Utangulizi
Uchumi ni jumla ya shughuli zote za binadamu zinazotenga kutolesha mahitaji yao. Ni hasa uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa bidhaa pamoja na kutolewa kwa huduma kwa njia mbalimbali.

(source WIKIPEDIA)
IMG_2951.jpg


Picha ya mtandaoni

Familia ni kikundi cha watu wanaokaa pamoja kama baba,mama na watoto.Kikundi hicho mara nyingi ni sehemu ya kundi kubwa zaidi la ukoo unaounganisha watu wenye asili katika uzazi wa pamoja.
Source WIKIPEDIA.

IMG_2905.jpg



Picha ya mtandaoni

Mwanaume ni kama afisa uchumi wa familia.
Mwanaume ni nguzo muhimu na imara katika familia, ni kichwa ameshikilia funguo za kulinda na kuisimamia familia kiuchumi. Uchumi wa familia unapoyumba mwanaume anapaswa kuulizwa yeye kama afisa uchumi wa familia anapaswa kufikiria jinsi ya kuitunza na kuilisha familia yake kwa kusaidiana na kushirikiana na familia yake iwe mke,watoto n.k anatakiwa kuwa mbunifu,msimamizi na mtekelezaji wa mipango ya uchumi wa familia.

Mwanaume kama afisa uchumi anahitajika apate msaidizi aliyesahihi atakayesaidiana nae katika kuendesha na kusimamia uchumi wa familia kwa ujumla. Kama tunavyoona wanawake siku hizi ni wachakarikaji wazuri kwelikweli. Inapendeza umwandae msaidizi/wasaidizi wako katika msingi iliyobora ya kusimamia uchumi wa familia hata ikitokea leo na kesho iwe umesafiri,mgonjwa au kupoteza maisha uchumi wa familia hauwezi kuyumba kama msingi bora umejengwa.

Inashangaza kukuta baadhi ya wanaume katika familia tena wasomi wanawakataza wasaidizi wao kujishughulisha na chochote au kujua majukumu yako kwa kuhofia msaidizi wako wa uchumi atabadilka,atakosa uaminifu au unamchukulia ni dhaifu.Ushawahi jiuliza wewe kama afisa uchumi wa familia haupo na msaidizi wako hajui ABC za uchumi wa familia yenu,matokeo yake uchumi kuyumba kwasababu msaidizi hajui jinsi ya kuendesha na kusimamia mipango ya uchumi.

Niliwahi soma bandiko humu nimesahuo kichwa cha bandiko na jina la mwanachama alikuwa ana omba ushauri yeye ni binti wa chuo alidate na mbaba tena ni mume wa mtu mbaya zaidi amefariki ameacha mke na watoto katika mazingira magumu kumbe jamaa alikuwa na mali dada anazifahamu familia hawajui na wameachwa kwenye mazingira magumu vuta picha tukio kama hilo,unaicha familia yako katika mateso.

Inasikitisha na kushangaza zaidi kwa baadhi ya wanaume kutojishughulisha na uchumi wa familia unakuta baadhi yao wanahudumiwa na wasaidizi wao na ni wazima kiafya,kiakili na kimwili si wagonjwa labda msaidizi/wasaidizi wake achukue majukumu hii imepelekea wasaidizi wao kulemewa na mizigo ya madeni chungu mzima yasiyoisha ili tu uchumi wafamilia uwe imara jamani wanaume msiwaachie wasaidizi wenu majukumu peke yao unatakiwa usimame imara wewe kama afisa uchumi wa familia.Unakuta mama anadaiwa mikopo mfano kwa Mangi,Muha,vikoba na bank ili tu uchumi usimame vyema familia ipate mahitaji muhimu kama malazi,makazi na chakula.

Umuhimu wa mwanaume kuwa kam afisa uchumi wa familia.
* Kusimamia bajeti ya familia-kuishi kulingana na kipato mnachopata.Japo kuna baadhi ya familia wana uhakika na pato lao la mwaka huwa kila mwanzoni mwa mwaka wanapanga bajeti yao ya mwaka mzima na mwishoni mwa mwaka wanafunga hesabu.Japo ukipanga nae Mungu anapanga kikubwa kumtanguliza Mungu .

* Kuepusha familia kuingia kwenye mzigo wa madeni usioisha.

* Kusimamia na kuendesha ipasavyo majukumu ya uchumi wa familia.

* Pato la familia litaongezeka- Mwanaume akisimamia Vizuri uchumi wa famili akishirikiana na msaidizi/wasaidizi wake pato la familia litaongezeka.

* Kuwa na familia yenye afya njema.

Niwape simulizi moja
Kuna mzee mmoja wa makamo alikuwa na miradi yake inayomuweka mjini maisha yanasonga na uchumi wa familia unaimarika kila siku, familia inapata mahitaji muhimu.Mzee yule sijui aliingiwa na jinamizi gani gafla tu akaikataza familia yake kutojihusisha na miradi yake ten,kumbe yule mzee alikuwa anahonga balaa yaani anatoa zaidi ya kile anachokiingiza na kukopesha kwa sana kwa watu wasio waaminifu huruma zilimponza.Mwisho wa siku madeni halipwi akafilisika na kukimbiwa na wateja wote uchumi wa familia ukayumba na kufa kabisa. Maisha ya familia yakayumba wasaidizi wote walikuwa wanamtegemea yeye na aliwakataza kufanya shughuli yoyote na kujishughulisha na miradi yake,mtoto wa huyo mzee mkubwa wa kiume alikuja kuokoa jahazi la familia yake kwa kufufua miradi ya familia upya hatimaye uchumi wa familia ukaimarika tena.Mzee alipata funzo kuwa na nidhamu ya fedha na kuwashirikisha wasaidizi wake kwenye mipango ya uchumi.


Hitimisho
Napendekeza afisa uchumi (mwanaume)msimamie majukumu yenu ipasavyo na kugawa majukumu. Pia msaidizi/wasaidizi wa afisa uchumi inapaswa kusimamia ipasavyo uchumi wa familia pale afisa uchumi alipokuamini, kukukabidhi na kukushirikisha mipango ya uchumi wa familia,si una aminiwa unafanya ndivyo sivyo na uchumi wa familia unayumba.Afisa uchumi muwawezeshe wasaidizi wenu, pendeni kuweka akiba, jiepusheni na anasa zisizo na maana, muwaelekeze, washaurini na kuwashirikisha wasaidizi wenu katika mipango ya uchumi wa familia. Mwisho kabisa msisahau kuomba kwa ajili ya uchumi wa familia zenu Mungu awaongoze sawasawa na mapenzi yake.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom