Umuhimu wa Pori Tengefu kwa Ikolojia ya Serengeti

Umuhimu wa Pori Tengefu kwa Ikolojia ya Serengeti

Rashda Zunde

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2022
Posts
204
Reaction score
231
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni mojawapo ya maeneo ya urithi wa dunia (World Heritage Site - UNESCO) si kwa ajili ya ardhi yake bali kuwepo kwa makundi makubwa ya wanyama wahamao, maarufu kama “the Great Serengeti wildebeest migration”. Mzunguko huu kwa kiasi kikubwa uko upande wa Tanzania na kiasi kidogo unapita mbuga za Maasai Mara nchini Kenya.

Sababu kubwa ya kuanzishwa kwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni kuhifadhi mzunguko wa nyumbu na umuhimu wake kama urithi wa dunia. Serikali imekuwa ikifanya mabadiliko pale ambapo imeonekana mzunguko huu uko hatarini na hivyo kuhakikisha unalindwa kikamilifu. Mabadiliko yamefanyika kuanzia miaka ya 1960 na ya 1990.
 
Back
Top Bottom