Tomaa Mireni
JF-Expert Member
- Sep 8, 2015
- 2,395
- 2,391
Fingerprint ni nini?
Kwa kiswahili (alama za vidole) ni alama au michoro inayopatikana kwenye vidole vya binadamu na zina maelezo ya kina ambazo hudumu katika maisha ya mtu na hivyo kuzifanya zifae kama viashirio vya muda mrefu vya utambulisho wake. Zinaweza kutumiwa na polisi au mamlaka nyingine kutambua watu ambao wanataka kuficha utambulisho wao au kutambua watu wasio na uwezo au waliokufa na hivyo kushindwa kujitambulisha.
KATIKA NYAKATI NYINGINE
Alama za vidole zimetumika pia katika nyakati za kale hasa kwa wabashiri au wanajimu walioweza kuchunguza alama zako na kukubashiria jambo fulani au kukua asili yenu,hata kipindi hiki kuna wataalamu wanaweza japo walaghai ni wengi. Hii inaonyesha utofauti uliopo kati ya utambulisho huu na mwingine.
Miaka ya nyuma kidogo sahihi ya dole gumba ilikuwa ni salama zaidi kuliko ya kuandika kwa mkono, kwani yahihi ya mkono inaweza kufojiwa kirahisi kuliko ya dole gumba ambalo lilichovywa kwenye vino kisha kugonga sehemu ya sahihi.
📷 BBC & THINKSTOCK
KASORO KATIKA MIFUMO TULIYONAYO SASA
Kwa kawaida mwarobaini wa utambulisho wa mtanzania umekuwa ni kitambulisho kinachokolewa na mamlaka ya vitambulisho Nida. Kitambulisho hiki pamoja na kuwa na namba ya utambulisho ambayo ndani yake kuna usajili wa alama za vidole bado haitoshelezi na si uthibitisho wa kumtambua mtu.
Kama muhalifu atafanya tukio na kisha kujiua itakuwa vigumu sana polisi na vyombo vya usalama kugundua utambulisho wake, labda kupitia ndugu, marafiki au maeneo ya makaazi yake, kwa hiyo kama katoka vijijini hali itakuwa ngumu zaidi sababu ya ukosefu wa mfumo jumla wa utambuzi wa watu.
Kuna watu wanamiliki vitambulisho zaidi ya kimoja na vidole vyake vile vile vya awali na bado hakuna mfumo ulioweza kutambua hilo.
Kupitia mifumo ya mitambuzi mingine ni rahisi kufojiwa kuliko ilivyo alama za vidole. Ukienda kwenye taasisi mbalimbali za serikali na binafsi bado utadaiwa kitambulisho au namba halisi ili hali uko na vidole vyako hapo, kwa nini wasikuscan kwenye mfumo wa alama za vidole na kuweza kuona utambulisho wako? Kupitia kasoro kama hizo ndio maana kuna umuhimu wa serikali kuja na mfumo wa jumla wa kutambua wananchi wake kupitia alama za vidole bila mahitaji ya kitambulisho halisi au namba. Mfumo ambao utatumika nchi nzima kwenye sekta zote.
FAIDA NA UMUHIMU WAKE
Au pia kama umekamatwa barabarani huenda vyombo vya usalama vikahitaji alama zako za vidole ili kuona rekodi zako za nyuma kama uliwahi kutuhumiwa au kutenda kosa kama hilo ili waone uzito wa kosa lako. Bila mfumo huo ungechukua muda sana labda kulala sero huku makabrasha yakipeluliwa kwa ajili ya kuangalia rekodi zako.
Fikiria tena jambo hili, umetuma maombi ya ajira Dodoma umeitwa lakini vyaraka zako ulizotakiwa kwenda nazo unasahu mojawapo, na muda wa usaili umefika, utachukua hatua gani wakati zote zinahitajika? Bila shaka mfumo huu utarahisisha sana mambo mengi.
Uwepo wa mfumo huu hauondoi uhalali wa kutembea na kitambulisho chako, kwa sababu hautakuwa sehemu zote ni sehemu nyeti tu zenye mahitaji ya kutambua utambulisho wa mtu.
HITIMISHO LA NINI KIFANYIKE NA SERIKALI NA NIDA
Kwa sababu ya changamoto za mwanzoni za ukomo wa kitambulisho, kukosewa majina na kutumia mfumo huu, serikali iboreshe vitambulisho vilivyopo kwa kutumia mfumo ambao unawezesha utambuzi wa alama za vidole niliopendeza.
Kuwepo na njia tatu
• Taarifa zijazwe na muhusika mwenyewe kupitia mtandao wa NIDA.
• Kwenda moja kwa moja ofisi za NIDA.
• Serikali ifanye kama ilivyofanya sensa ya watu na maakazi, watumishi wote wa sensa wakiwa na vishikwambi vyao waboreshe utambulisho wa raia. Mambo ya kuongea katika utambulisho huo yawe. (Elimu yako, anuani yako ya makazi {yahusishe postikodi}, nambari ya nyumba pia) utakachojaza kiambatane na kielelezo cha chake, mfano elimu ni form 4 basi uwe na cheti chake, hivyo hivyo kwa kila kitu. Itakuwa na nzuri sana tutapunguziana mizigo ya kutembelea nayo unapotaka kwenda mahali.

- 1. Hii itarahisisha ufanisi mbalimbali kwa serikali na taasisi mbalimbali pamoja na wananchi,yani hutahitaji kutembea na nyaraka nyingi sababu tayari zipo ndani ya mfumo.
- 2. Itasaidi sana kwa upande wa vyombo vya usalama pia kurekodi taarifa za watuhumiwa mbalimbali, yani polisi akikukamata Mwanza hata kama huna kitambulisho anaweza kuona matukio yako ya nyuma.
- 3. Ukienda Benki, TRA au kwa watoa huduma wa mitandao(mifano) huna haja ya kutembea na kitambulisho sababu tayari uko vidole vyako, na utapata huduma kama kawaida.
- 4. Kupunguza uhalifu mbalimbali, kivipi? Yani kama kuna uhalifu sehemu kama jeshi la polisi linaweza kuscan mazingira ya uhalifu huo ni rahisi kumpata mtuhumiwa hata kama hakukuwa na kamera za ulizi.
- 5. Kurahisisha ukusanyaji wa taarifa mbalimbali na kuzirekodi kwa urahisi.
- 6. Kupunguza udanganyifu kwa wananchi sababu hutaweza kumili vitambulisho zaidi ya kimoja wala kudanganya taasisi. Faida zipo nyingi sana.
- 7. Faida zoote hizo kwa ujumla ni kuokoa muda ambao unaweza kupotea pale utakapopatwa na jambo la dharura.

Upvote
3