Mswahili mahiri
New Member
- Jul 31, 2021
- 1
- 6
Kilimo kama tunavyo fahamu ni moja ya sekta ambayo inagusa maisha ya zaidi ya asilimia 70%waishio mijini na vijijini nchini Tanzania. Na kama tunavyoelewa uchumi wa wakazi wengi waishio maeneo ya vijijini umejikita zaidi katika shughuli za kilimo moja kwa moja hivo linapo kuja suala la upatikanaji wa taarifa sahihi katika sekta ya kilimo inakua ni jambo muhimu na lisilo hitaji mchezomchezo. Hapa katika suala la upatikanaji wa taarifa muhimu nitaangazia kuanzia;
1)Taarifa sahihi za uzalishaji wa mazao sahihi katika eneo husika.
2)Taarifa sahihi za mbinu bora za kilimo katika eneo husika
3)Taarifa sahihi za masoko ya mazao yaliyo zalishwa.
Katika suala la taarifa tunaweza angazia ni namna gani mkulima mdogo kijijini anaweza kupata taarifa sahihi na ikamnufaisha katika shughuli zake.
Katika ulimwengu tulionao kwa sasa tumeingia dunia ya utandawazi na tunasema dunia nisawa na kijiji kutokana na kasi ya ukuaji wa teknolojia mbalimbali ambazo kimsingi zimekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo na ukuaji wa uchumi katika nchi mbalimbali. Lakini linapo kuja suala la upatikanaji wa taarifa sahihi katika sekta ya kilimo bado inaonekana teknolojia haijafanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwa saidia wakulima wadogo vijijini.
Nizungumzie moja kwa moja yeknolojia ya habari na tehama ambayo kimsingi ndio nyenzo inayoweza kuunganisha jamii nzima kwa wakati mmoja lakini katika sekta ya kilimo bado imekua kama haipo.
Katika hili ningependa kueleza namna teknolojia ya Tehama ingeweza kusaidia kilimo hasa katika upatikanaji wa taarifa sahihi na namna teknolojia hii inaweza kusaidia kuboresha shughuli za kilimo na kukuza uzalishaji na hatimae kukuza pato la taifa na jamii kwa ujumla.
Mambo hayo ni kama haya ya fuatayo;
1)TAARIFA ZA UTAFITI WA MAZAO KATIKA MAENEO NA WAKATI SAHIHI
-Katika suala hili wakulima wengi wamekua wakilima kienyeji bila kunia ni zao gani linapaswakulimwa eneo lipi na wakati upi.Hii inatokana na kukosrkana kwa taarifa sahihi kuhusu kilimo na kwa undani ukiangalia unaweza kuta kilimo kinafanyika kwa mazoea mfano:ni katika mkoa wa Rukwa wakulima wengi wanalima sana mahindi pekee kama zao la chakula lakini pia mahindi hayo hayo yakibakia kama zao la kibiashara kitu ambacho kimsingi kinaweza changia umasikini lakini pia linapotokea suala la mabadiliko ya tabia ya nchi na hali ya hewa kubadirika wengi huishia kushindwa kua nanmazao mbadala yanayoendana na hali ya ukanda wao, lakini endapo kungekua na taarifa sahihi za kipi kimetafitiwa kulimwa wapi na wakati gani ingesaidia sana.
2)MBINU BORA ZA KILIMO NA KITAALAMU KUHUSU KILIMO
-Katika suala hili ningependa kuelezea namna teknolojia ya habari na tehama ingesaidia mfano ni kua na tovuti au website zinazo waunganisha maafisa ugani moja kwa moja na wakulima ili kutoa msaada wa haraka unapo hitajika kwa wakulima na kuweza kuwapa mbinu bora za kuweza kukabiliana na changamoto mbali mbali za kilimo.mfano uwepo wa app za simu,websites,kuwe na vituo vya habari mfano kupiga simu za bure na kuunganishwa na mtoa huduma kwa haraka.
Hii ingesaidia kupunguza gharama lakini pia hasara mbalimbali zitokakanozo na kukosekana kwa taarifa sahihi katika kilimo na hivo kuboresha sekta ya kilimo.
3)TAARIFA SAHIHI ZA MASOKO
-Katika suala la upatikanaji wa masoko ya mazao ya kilimo imeonekana kua bado ni changamoto kubwa katika nchi ya tanzania na kupelekea wakulima wengi kuendelea kugubikwa nanwimbi la umaskini.
Lakini endapo kungekua na mfumo rasmi unaoratibu masoko ya mazao kwa kupitia njia ya tehama basi wakulima wangenufaika barabara. Katika suala hili la masoko wakulima wengi wamekua wakilalamikia mfumo mbovu wa ulanguzi lakini pia kutokua na bei za kufanana. Mfano mzuri mjini sumbawanga gunia la mahindi linauzwa kiasi cha TZS23,000 wakati mkoani songwe ambako ni kilometa chache mahindi yanabei ya juu kidogo.
Pamoja na hilo lakini pia Taarifa za bei ya mazao mengine ingekua inawekwa bayana labada ingesaidia wakulima pia kuacha kuamini katika kilimo cha aina moja na kubadilisha aina ya kilimo ili kukuza vipato vyao mfano ni kama nilivo kwisha kusema mwanzo ukosefu wa taarifa unawaathiri wa kulima wengi na kushindwa kuziona fulsa zingine za kilimo zinazoweza kupatikana katika maeneo yao
NB:Upatikanaji wa taarifa sahihi katika sekta ya kilimo unaweza kuboresha kilimo,kuleta kilimo chenye tija ,kupunguza umaskini,kuleta utawara bora na kukuza uchumi wa mwananchi mmojammoja nantaifa kwa ujumla
View attachment 1912343View attachment 1912342

Upvote
1