Uchaguzi 2020 Umuhimu wa uchaguzi mdogo na hatma ya upinzani kuelekea 2020

Huu
Hili pendekezo lako tupe mfano wa nchi zinazotumia utaratibu huu, Mahakamani yapo mengi ikiwepo namna mawakili walivyowasilisha hoja zao.
Vipi ambao mahakama ilijiridhisha na kutengua matokeo?
Ninachoendelea kuamini kama umeibiwa, au uchaguzi una dosari na ukapata Mwanasheria mzuri haki yako utapata tu
 
Naona hatuelewani kabisa..... Nimekuuliza kama mtu kachezewa rafu na hana ushahidi wa kutosha kama ambavyo Tanzania tulichezewa rafu za kutosha na Acacia lakini hatukuwa na ushahidi hadi pale kamati ilipoundwa..... je haki yake ataipataje owa mazingira hayo???

Nachopropose ni kwamba kamati iwepo ya kusimamia malalamiko na kuchunguza kama ambavyo vyuoni usiporidhika na matokeo unasahishiwa upya ingawa huwa hakuna ushahidi kuwa umesahishiwa vibaya!!!

Haijalishi upinzani unacheka au unawatukana swali ni kwamba huoni kamati zikichunguza ndio solution..... Simple and clear

Hayo ya wapinzani kuwa na matusi sijui yanaingiaje hapa maana kama siasa za kusigana zilianzia CCM zanzibar so wanavuna walichopanda. Alafu haki ni takwa la kikatiba sio favor kiasi kwamba upinzani wajikombe kwa CCM eti ili ndio wapewe haki that's cowardice.

Anyway rudi kwenye hoja je kamati haiwezi kuwa suluhisho (assuming mahakamani huna ushahidi wa kutosha)
 
Kwani kila kitu mpaka muige nchi za wenzetu?? Hapa Afrika hakuna nchi yenye demokrasia hivyo usitegemee mfumo huu utumike..... Ukienda nchi za wazungu chaguzi zao zipo kielektroniki so ni rahisi kutrace kila kura ilivyoingizwa kwenye mfumo so hata kesi mahakamani unashinda asubuhi tuu. Hata serikali mbili kwa mchi moja hakuna nchi duniani inautumia ila ni sisi tu je umewahi uliza CCM wameiga nchi gani huu mfumo??

Nimekupa mfano mdogo tu kuwa mavyuoni au NECTA ukirudishiwa matokeo ukakuta marks zimepelea unaruhusiwa kuappeal hata bila ya kuuona mtihani wako.... Then utalipia kiasi fulani alafu mtihani wako utasahishwa upya alafu matokeo yako yatakuwa updated ila sijawahi kuambiwa nilete ushahidi kuwa nimefelishwa au nimesahishiwa vibaya

Na toka mfumo huo utumike malalamiko ya wanafunzi wanaofikiri wamesahishiwa vibaya yanamalizwa..... Ssa kwanini msiige mfumo wa NECTA au mavyuoni ili malalamiko ya wizi yaishe???

Embu tuanzie hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…