SoC02 Umuhimu wa ultrasound kwa wajawazito

Stories of Change - 2022 Competition

Gidamarirda

Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
37
Reaction score
92
Ningependa kutumia fursa hii kueleza umuhimu wa kipimo cha Ultrasound kwa mama mjamzito na jinsi ambavyo teknolojia hii mpya inayozidi kuboreshwa kila iitwapo leo inavyoweza kuleta manufaa bora kwa afya ya mama na mtoto aliye tumboni katika nchi yetu na kusaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto kabla na wakati wa kujifungua.

Kipimo cha Ultrasound ni Kipimo salama kwa mama na mtoto aliye tumboni na hivyo kufaa katika kufuatilia maendeleo ya mimba tangu hatua za mwanzo za mimba mpaka mwisho wakati wa kujifungua. Ultrasound ni hutumia nguvu ya umeme kuzalisha sauti iliyo juu ya uwezo wa masikio ya wanadamu na hivyo hutuma sauti hiyo ndani ya mwili na kupokea mwangwi wa sauti hiyo na kutengeneza picha za viungo vya ndani ya mwili kulingana ukaribu au umbali wa mawimbi hayo lakini pia uzito au uwepesi wa mawimbi hayo.

Kutokana na takwimu za vifo vya mama na mtoto katika umri wa mimba, Tanzania imekumbwa na vifo 500 vya mama wajawazito kati ya wajawazito 100,000, na sababu za vifo hivyo ni Pamoja na kutoka damu nyingi wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua, matatizo ya kutoka kwa mimba, na asilimia 99 ya vifo hivyo vingeweza kuzuilika ikiwa vingegundulika mapema na kuchukuliwa hatua. Teknolojia hii ya Ultrasound inaweza kutusaidia kupiga hatua katika kupunguza idadi ya vifo hivyo.

Kama tunavyofahamu ujauzito hugawanywa katika hatua tatu za ukuaji wake tumboni (Trimesters), ambazo zimegawanyika katika vipindi vya miezi mitatu kwa kila hatua. Hatua ya awali (1st Trimester), hii huanza katika wiki 1 mpaka wiki ya 13 na hatua ya Pili (2nd Trimester) ambayo huanzia wiki ya 14 mpaka wiki ya 27, na hatua ya tatu na ya mwisho (3rd Trimester) huanzia wiki ya 28 hadi wiki ya 40.

Katika hatua ya kwanza, matatizo ya mimba kutunga nje ya mji wa uzazi na kutoka kwa mimba yamekua ni matatizo makuu yanayopelekea vifo vya mama wajawazito, matatizo hayo husababisha hatari ya kuvuja damu nyingi na hatimae kupoteza maisha. Kutunga mimba nje mji wa uzazi, tatizo hili hutokea mara nyingi na wanawake wengi hushindwa kufahamu ikiwa ni wajawazito, lakini ultrasound hutusaidia kugundua haraka na kupata ufumbuzi kabla halijaleta madhara.

Tatizo la kutoka Mimba nalo husababisha vifo vya wanawake, tatizo hili huweza kugundulika haraka kwa ultrasound na kupata majibu ikiwa ujauzito umetoka kabisa au kama kuna masalia ya ujauzito katika mfuko wa uzazi ambao mara nyingi hupelekea maambukizi katika via vya uzazi na kuhatarisha maisha ya mama. Katika kipindi hiki, kipimo cha ultrasound husaidia kutambua umri wa mimba kwa usahihi hasa kwa wanawake waliosahau tarehe ya mwisho ya hedhi, husaidia kuonesha ikiwa kuna ujauzito wa mapacha na kupunguza matatizo yanayoweza kutokana na ujauzito pacha, huonesha matatizo yatokanayo na Kromosomu na matatizo mengine ya kimaumbile ambayo huweza kuonekana mapema katika wiki ya 11 mpaka wiki ya 13 ya ujauzito.

Hatua ya Pili, katika kipindi hiki ultrasound husaidia kuonesha ikiwa kondo la nyuma limejishikiza sehemu salama, limefunika kabisa njia ya kutokea au kwa sehemu (Partial or complete Placenta Previa) na kujua upana wa njia ya cervix ikiwa imefunga au kufunguka na kusaidia kuonesha ikiwa kuna uwezekano wa kijusi kutoka kabla wakati. Lakini pia ultrasound huonesha ikiwa kuna kitu kinachotatiza ukuaji wa kijusi katika mfuko wa mimba na kuonyesha kiwango cha maji ya amniotiki kinachomzunguka mtoto tumboni (Amniotic Fluid Index).

Hatua ya Tatu, kipindi hiki cha mwisho huwa na matarajio makubwa lakini yote hayo yanaweza kukatishwa. Matatizo kama vile kupasuka/kuchanika kwa mfuko wa kizazi, kutoka damu nyingi baada ya kujifungua na kujifungua kabla ya wakati, hivi vyote huweza kuchangia kwa sehemu kubwa kusababisha vifo vya mama na mtoto aliye tumboni. Teknolojia hii ya Ultrasound husaidia kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya mtoto, mkao wake tumboni (presentation), kondo la nyuma, kuonesha makadirio ya uzito wa kijusi na kuonesha ikiwa kamba ya kitovu imejizungusha katika shingo ya kijusi.

Katika nchi zilizoendelea ultrasound imesaidia kupunguza idadi ya vifo vya mama wajawazito kwa kiwango kikubwa kwa kufuatilia kwa ukaribu hatua za ukuaji wa kiumbe, kwa hivyo linapogundulika tatizo linawasaidia kukabiliana nalo na kuleta matokeo chanya. Kama taifa linalopiga hatua kufikia katika utoaji wa huduma bora za afya ni lazima kufahamu kwamba teknolojia hizi hazikwepeki na hasa ukizingatia kuwa zimeanza kutumika nchini, na ni muhimu kutazama kwa ukaribu changamoto zozote zinazoweza kujitokeza na kuzitatua ili kufikia katika lengo la kutoa huduma iliyo bora na salama kwa jamii yetu,

Changamoto kuu hasa zinazokabili utoaji wa huduma ya ultrasound hapa nchi; Uhaba wa wataalamu wa ugunduzi kwa ultrasound, na hii inatokana na uhaba wa vyuo vya kutolea mafunzo hayo, kufika mwaka 2020 vyuo vinavyotoa mafunzi ya ugunduzi huu vilikua viwili tu na hivyo kushindwa kutosheleza mahitaji ya nchi inayokuwa kwa kasi na kuhitaji huduma bora za afya , na hata wataalamu wachache waliopo wamekua hawana ujuzi mpana juu ya teknolojia hii, hivyo kusababisha mkanganyiko na wakati mwingine kumekuwa na majibu (false-positive) yasiyoonesha weledi wa wanataaluma na kufanya watu wengi kuogopa au kutoamini majibu yanayotolewa, lakini kumekua ununuzi au uingizwa wa mashine za ultrasound zisizokidhi ubora au uhitaji ukizingatia kuwa teknolojia hii inakua kwa kasi, pia gharama za vipimo kuwa kubwa hivyo watu hukimbia gharama hizo na kuamua kufanya mara moja au kutokufanya kabisa kipimo hicho, mwisho wanawake kukataa kufanya kipimo hicho kwa kuamini kuwa ultrasound ina madhara au inapunguza muda wa kuishi.

Ili kuboresha huduma ya afya ya mama na mtoto ni lazima serikali kupitia wizara ya afya kuhakikisha huduma hizi zinapatikana kwa gharama nafuu katika zahanati na vituo vyote vinavyotoa huduma kwa mama wajawazito nchini, na kuweka utaratibu wa upimaji endelevu wa kipimo hicho katika vipindi vyote vitatu vya ujauzito. Lakini pia wizara kupitia bodi ya radiolojia iwajibike katika kukagua na kutoa kibali cha utoaji wa huduma hizi kwa kuzingatia weledi wa wataalamu wetu, aidha bodi inapaswa pia kudhibiti/kusimamia uingizwaji wa vifaa bora na za kisasa ili kukidhi mahitaji ya huduma hii hapa nchini, Ni vizuri pia kupitia mitaala yetu na kuboresha ili kuendana na kasi ya maendeleo haya na weledi uwe mkubwa kwa wataalamu wetu. Elimu itolewe kupitia Serikali na wadau mbali mbali wa afya ili kuongeza uelewa juu ya huduma hii kwa jamii yetu.
 
Upvote 27
Ningependa kutumia fursa hii kueleza umuhimu wa kipimo cha Ultrasound kwa mama mjamzito na jinsi ambavyo teknolojia hii mpya inayozidi kuboreshwa kila iitwapo leo inavyoweza kuleta manufaa bora kwa afya ya mama na mtoto aliye tumboni katika nchi yetu na kusaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto kabla na wakati wa kujifungua.

Kipimo cha Ultrasound ni Kipimo salama kwa mama na mtoto aliye tumboni na hivyo kufaa katika kufuatilia maendeleo ya mimba tangu hatua za mwanzo za mimba mpaka mwisho wakati wa kujifungua. Ultrasound ni hutumia nguvu ya umeme kuzalisha sauti iliyo juu ya uwezo wa masikio ya wanadamu na hivyo hutuma sauti hiyo ndani ya mwili na kupokea mwangwi wa sauti hiyo na kutengeneza picha za viungo vya ndani ya mwili kulingana ukaribu au umbali wa mawimbi hayo lakini pia uzito au uwepesi wa mawimbi hayo.

Kutokana na takwimu za vifo vya mama na mtoto katika umri wa mimba, Tanzania imekumbwa na vifo 500 vya mama wajawazito kati ya wajawazito 100,000, na sababu za vifo hivyo ni Pamoja na kutoka damu nyingi wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua, matatizo ya kutoka kwa mimba, na asilimia 99 ya vifo hivyo vingeweza kuzuilika ikiwa vingegundulika mapema na kuchukuliwa hatua. Teknolojia hii ya Ultrasound inaweza kutusaidia kupiga hatua katika kupunguza idadi ya vifo hivyo.

Kama tunavyofahamu ujauzito hugawanywa katika hatua tatu za ukuaji wake tumboni (Trimesters), ambazo zimegawanyika katika vipindi vya miezi mitatu kwa kila hatua. Hatua ya awali (1st Trimester), hii huanza katika wiki 1 mpaka wiki ya 13 na hatua ya Pili (2nd Trimester) ambayo huanzia wiki ya 14 mpaka wiki ya 27, na hatua ya tatu na ya mwisho (3rd Trimester) huanzia wiki ya 28 hadi wiki ya 40.

Katika hatua ya kwanza, matatizo ya mimba kutunga nje ya mji wa uzazi na kutoka kwa mimba yamekua ni matatizo makuu yanayopelekea vifo vya mama wajawazito, matatizo hayo husababisha hatari ya kuvuja damu nyingi na hatimae kupoteza maisha. Kutunga mimba nje mji wa uzazi, tatizo hili hutokea mara nyingi na wanawake wengi hushindwa kufahamu ikiwa ni wajawazito, lakini ultrasound hutusaidia kugundua haraka na kupata ufumbuzi kabla halijaleta madhara.

Tatizo la kutoka Mimba nalo husababisha vifo vya wanawake, tatizo hili huweza kugundulika haraka kwa ultrasound na kupata majibu ikiwa ujauzito umetoka kabisa au kama kuna masalia ya ujauzito katika mfuko wa uzazi ambao mara nyingi hupelekea maambukizi katika via vya uzazi na kuhatarisha maisha ya mama. Katika kipindi hiki, kipimo cha ultrasound husaidia kutambua umri wa mimba kwa usahihi hasa kwa wanawake waliosahau tarehe ya mwisho ya hedhi, husaidia kuonesha ikiwa kuna ujauzito wa mapacha na kupunguza matatizo yanayoweza kutokana na ujauzito pacha, huonesha matatizo yatokanayo na Kromosomu na matatizo mengine ya kimaumbile ambayo huweza kuonekana mapema katika wiki ya 11 mpaka wiki ya 13 ya ujauzito.

Hatua ya Pili, katika kipindi hiki ultrasound husaidia kuonesha ikiwa kondo la nyuma limejishikiza sehemu salama, limefunika kabisa njia ya kutokea au kwa sehemu (Partial or complete Placenta Previa) na kujua upana wa njia ya cervix ikiwa imefunga au kufunguka na kusaidia kuonesha ikiwa kuna uwezekano wa kijusi kutoka kabla wakati. Lakini pia ultrasound huonesha ikiwa kuna kitu kinachotatiza ukuaji wa kijusi katika mfuko wa mimba na kuonyesha kiwango cha maji ya amniotiki kinachomzunguka mtoto tumboni (Amniotic Fluid Index).

Hatua ya Tatu, kipindi hiki cha mwisho huwa na matarajio makubwa lakini yote hayo yanaweza kukatishwa. Matatizo kama vile kupasuka/kuchanika kwa mfuko wa kizazi, kutoka damu nyingi baada ya kujifungua na kujifungua kabla ya wakati, hivi vyote huweza kuchangia kwa sehemu kubwa kusababisha vifo vya mama na mtoto aliye tumboni. Teknolojia hii ya Ultrasound husaidia kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya mtoto, mkao wake tumboni (presentation), kondo la nyuma, kuonesha makadirio ya uzito wa kijusi na kuonesha ikiwa kamba ya kitovu imejizungusha katika shingo ya kijusi.

Katika nchi zilizoendelea ultrasound imesaidia kupunguza idadi ya vifo vya mama wajawazito kwa kiwango kikubwa kwa kufuatilia kwa ukaribu hatua za ukuaji wa kiumbe, kwa hivyo linapogundulika tatizo linawasaidia kukabiliana nalo na kuleta matokeo chanya. Kama taifa linalopiga hatua kufikia katika utoaji wa huduma bora za afya ni lazima kufahamu kwamba teknolojia hizi hazikwepeki na hasa ukizingatia kuwa zimeanza kutumika nchini, na ni muhimu kutazama kwa ukaribu changamoto zozote zinazoweza kujitokeza na kuzitatua ili kufikia katika lengo la kutoa huduma iliyo bora na salama kwa jamii yetu,

Changamoto kuu hasa zinazokabili utoaji wa huduma ya ultrasound hapa nchi; Uhaba wa wataalamu wa ugunduzi kwa ultrasound, na hii inatokana na uhaba wa vyuo vya kutolea mafunzo hayo, kufika mwaka 2020 vyuo vinavyotoa mafunzi ya ugunduzi huu vilikua viwili tu na hivyo kushindwa kutosheleza mahitaji ya nchi inayokuwa kwa kasi na kuhitaji huduma bora za afya , na hata wataalamu wachache waliopo wamekua hawana ujuzi mpana juu ya teknolojia hii, hivyo kusababisha mkanganyiko na wakati mwingine kumekuwa na majibu (false-positive) yasiyoonesha weledi wa wanataaluma na kufanya watu wengi kuogopa au kutoamini majibu yanayotolewa, lakini kumekua ununuzi au uingizwa wa mashine za ultrasound zisizokidhi ubora au uhitaji ukizingatia kuwa teknolojia hii inakua kwa kasi, pia gharama za vipimo kuwa kubwa hivyo watu hukimbia gharama hizo na kuamua kufanya mara moja au kutokufanya kabisa kipimo hicho, mwisho wanawake kukataa kufanya kipimo hicho kwa kuamini kuwa ultrasound ina madhara au inapunguza m.

Kaka Saimon

Mimi naitwa Lumola Nimekupigia Kura Naomba na Mimi unipigie Kura kupitia SoC 2022 - Tufuge nyuki kwa maendeleo endelevu na tuwalinde kwa wivu mkubwa
 
Hongera sana mkuu kwa kuikumbuka afya ya mama na mtoto.
 
Afya ya mama na mtoto ni muhimu sana kwenye jamii kwani elimu ya kutosha bado inahitaji sana .wengi wana dhana potevu kuhusu matumizi ya ultrasound kwa mama hasa wajawazito ivyo jamii bado inahitaji kupata elimu ya kutosha kuhusu upimaji kwa ultrasound
 
Asante sana Kwa Somo lako zuri sana ndugu . Ila nina swali kidogo nahitaji kufahamishwa,Je ni kweli vipimo vya ultrasound vinaweza kubaini jinsia ya mtoto aliye tumboni!!?
Nawasilisha.
 
Asante sana kwa swali zuri, Ndio Ultrasound Huweza kubaini Jinsia ya mtoto aliye tumbo, lakini huweza kutambulika kuanzia katika Wiki ya 20 ya Umri wa Mimba Kwenda Mbele.
NB: mtaalamu wa afya anaruhusiwe kutokusema jinsia ikiwa hajawa na uhakika bado na kumwomba Mgonjwa arudi wakati mwingine kuhakikisha.
 
Afya ya mama na mtoto ni muhimu sana kwenye jamii kwani elimu ya kutosha bado inahitaji sana .wengi wana dhana potevu kuhusu matumizi ya ultrasound kwa mama hasa wajawazito ivyo jamii bado inahitaji kupata elimu ya kutosha kuhusu upimaji kwa ultrasound
Asante Sana, Muda ni Sasa na Wakati ndio Huu.
 
Mkuuu,nnahitaji kusoma diploma ya utrasuound au radiologia je nivyuo vipi vinatoa hiyo course??
 
Course Nzuri hiyo.

Vyuo vinavyotoa Diploma in Diagnostic Radiography (DDR) Bachelor ni Vyuo Viwili hapa Nchini, Muhas (Muhimbili) na Cuhas (Bugando).
 
Back
Top Bottom