ukiona mkeo na watoto wanataka kukuwahisha basi hiyo familia haina upendo. na wewe na uhusiano wako na familia yako si mzuri.
Sipati picha mwanamke awe na watoto wa kike afu mume afe aandike urith kwa mtoto/watoto wake wa kiume wa nje. Kwa kweli ni dhambi kumnyanyapaa mtoto wa nje; lakini haya mambo ya mali ndiyo yanayofanya wamama wengi kuchukia watoto wa nje. Tuna family friend wetu ana mabinti tu; mumewe ana mtoto mmoja wa nje tena wa kiume; yule mama ni muongeaji huwa anamchana mume wake live kuwa asitegemee mwanae huyo wa nje ataambulia kitu kwani mali wanazisaka wote kwa hiyo jasho lake haliliwi na mtu. Good thing ni kuwa huyo mtoto yuko kwa mama yake. Kwa hiyo kama huyo mama yake ana akili amjengee maisha mwanae mapema ikiwezekana hata kwa kumbana huyo mwanaume.
NyumbaKubwa,huyo mama naye aache za kuleta,hivi alomwambia baba atatangulia kufa wanae na yeye wangali hai nani?
Kila mtu ajitafutie mali zake , ndo mana wenzetu urithi wanaachie mtu yeyote, mtoto akue akijua anatakiwa kufanya juhudi ya maisha afanikiwe, mzazi jukumu lake ni kumwandalia maisha kwa kumsomesha, akifika 18 and above anaanza ya kwake, sasa tatizo huwa tunatolea sana macho mali za familia, wengine wanadiriki hata kuwaua wazazi ili warithi mali, mrithishe ila usimwambie kahifadhi huko bank, ili awe na nguvu ya kutafuta, nakumbuka baba alikuwa anatwambia, mali zangu ni kwa ajili yangu na mke wangu, kama hamsomi mtajijua mkishakua
Tatizo tunaloongelea hapa ni baba kufa wakati watoto ni wadogo. Lazima wife atapenda mali kama majumba nakadhalika vitumike kuwaendeleza watoto wa ndani ya familia. Tatizo linakuja baba ana watoto wengine kadhaa nje. Sasa kimbembe ni nani yuko tayari kugawana mali na mtoto wa nje?? Umemsoma hapo Bishanga?
Of course hamna mtu mzima mwenye akili anayetegemea mali za kurithi; mara nyingi wa hivyo ni wale waliochezea maisha.
Nina mama yangu mdogo alikuwa nyumba ndogo ya kibosile fulani miaka ya 80s; Huyo baba alikuwa na pesa sana nakumbuka alikuwa anakuja na mama mdogo home na magari ya kifahari wakati those days magari mengi yalikuwa peugeot yeye alikuwa na gari tofauti tofauti sijuhi alikuwa anafanya kazi wapi maana nilikuwa mdogo sana. Alimpangishia nyumba sharif shamba.
Sijuhi kilichotokea baada ya muda wakaachana-as usual nyumba ndogo ni nyumba ndogo wengi hupigwa chini sooner or later
Kibaya sasa walikuwa wamezaa mtoto wa kiume; mama mdogo akahamia mwanza; kule akaolewa. Baadaye alifariki. Sasa mtoto ikabidi aende kijijini kwa wajomba zake. Alikuja hapa Dar baada ya kusikia baba yake yuko hoi amepooza. Unaambiwa ndugu zake walimtoa dima wakasema si ndugu yao wakati sura ni anafanana na baba yao kuliko wao. Yule baba alikufa; kijana maisha yake hana mbele wala nyuma maana wajomba zake waliweza msomesha mpaka form four tu kijijini.
Sasa nadhani yule mdingi hakuwahi kuwaambia familia yake kuwa ana mtoto though madada zake walikuwa wanamjua (mashangazi).
Watoto wa nje wasitegemee sana kwa baba zao; ni wamama wawajengee maisha.
Kuna kijana mmoja aliandikwa mrithi wa nyumba pale sinza, na baba yake alipofariki akaamua kumfukuza mama yake eti aende kijijini anataka nyumba yake auze, hamuwezi amini, mie pia naona watoto hata wakiandikishwa kitu wazazi waandike mpak a wote wafariki ndio warithi mali, sababu wengine huwa haziwatoshi kabisa
Nina mama yangu mdogo alikuwa nyumba ndogo ya kibosile fulani miaka ya 80s; Huyo baba alikuwa na pesa sana nakumbuka alikuwa anakuja na mama mdogo home na magari ya kifahari wakati those days magari mengi yalikuwa peugeot yeye alikuwa na gari tofauti tofauti sijuhi alikuwa anafanya kazi wapi maana nilikuwa mdogo sana. Alimpangishia nyumba sharif shamba.
Sijuhi kilichotokea baada ya muda wakaachana-as usual nyumba ndogo ni nyumba ndogo wengi hupigwa chini sooner or later
Kibaya sasa walikuwa wamezaa mtoto wa kiume; mama mdogo akahamia mwanza; kule akaolewa. Baadaye alifariki. Sasa mtoto ikabidi aende kijijini kwa wajomba zake. Alikuja hapa Dar baada ya kusikia baba yake yuko hoi amepooza. Unaambiwa ndugu zake walimtoa dima wakasema si ndugu yao wakati sura ni anafanana na baba yao kuliko wao. Yule baba alikufa; kijana maisha yake hana mbele wala nyuma maana wajomba zake waliweza msomesha mpaka form four tu kijijini.
Sasa nadhani yule mdingi hakuwahi kuwaambia familia yake kuwa ana mtoto though madada zake walikuwa wanamjua (mashangazi).
Watoto wa nje wasitegemee sana kwa baba zao; ni wamama wawajengee maisha.
pole sana Mlabondo,mzee kweli hapo alichemsha big time,msamehe bure lakini.Sie tupo watoto watano kiume mbili kike 3 nyumba ndogo wapo wakike wawili mzee Wangu alimrithisha nyumba ndogo yake kila kitu mashamba Moshi na nyumba mbezi beach. Yaani tulikuwa hatuna thamani kabisa kwake. Inauma nusra ningepata murder case
Wanawake huwa tunajisahau sana, tunahisi kama maisha haya tunayoishi sasa hivi yatadumu milele,kumbe huwa kuna mabadiliko dunia inakugeukia juu chini unaanza kuhaha na njia yaani mwanaume anafariki mwezi huu mwezi ujao tayari watoto wako barabarani wanauza mayai ya kuchemsha sijui kwa nn, mie nasema bora wanawake wa kisasa kwa sasa hivi mtu una kazi yako umesoma vitu vidogovidogo havitakusumbua labda uwe mbishi ku maintain lifestyle ya wakati ule
Kweli hili ni jambo la muhimu sana sana
Sio siri hapa nilipo nishaandika Will yangu nasubiri tuu Executor wangu aipitie aisome aone kama iko sawa niisign
Sijasubiri na wala suala la kuchuria kufa ila naangalia mbele kwa watoto wangu na kwa mke wangu na kwangu mimi pia
Ni suala la muhimu sana maana mwenye uamuzi wa mwisho wa mali yake iende kwa nani au kw awakati gani igawanywe ni yule mwenye mali
Kwa hiyo wandugu nawashauri msisite kuandika Will ni kitu muhimu sana
Hata kama mwenye mali akiamua kutoa mali zake zote kwa Msikiti au Kanisa ni uamuzi wake
sijui nani kachoropoa kibaton cha 'like'!
Kwa sheria ilivyo sasa watoto wa nje wanapoteza haki ya kurithi hasa kama baba hakuwatambulisha/ama kuwaweka wazi kuwa ni wanawe....na kwa kusema ukweli mimi naona hii ni fair tu. Kama una mtoto wa nje ni vema ukamchukuwa na kukaa nae/au kuhakikisha anatambulika formally kuwa ni mwanao/mtegemezi wako.
Kutegemea na dini ya muhusika, wosia peke yake unaweza usiwe na nguvu.....kama kuna vitu unataka 'kumrithisha' mtu ambaye kisheria hana haki ya kukurithi ni vema ukamgawia sehemu yake akaanza kuimiliki kabla wewe hujafa.