Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa siku ya Jumatatu imedokeza kuwa mitandao ya kihalifu kote Kusini Mashariki mwa Asia inategemea zaidi app ya ujumbe wa Telegram kwa ajili ya kutekeleza shughuli haramu.
Ripoti hiyo inaangazia jinsi app ya Telegram imewezesh na kufanikisha kwa kiasi kikubwa uhalifu uliopangwa huko Kusini Mashariki mwa Asia.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) inadai kuwa data zilizodukuliwa ikiwemo taarifa kutoka kwenye credit cards, passwords, na browsing history zinauzwa waziwazi kupitiaTelegram.
Ripoti hiyo ilidokeza kuwa app hiyo ya Telegram kutokana na usimamizi mdogo, inawawezesha wahalifu wa mtandao kufanikiwa.
Soma pia: Telegram sasa itaanza kutoa taarifa za watumiaji wake kwa serikali kwa madai halali
Vilevile, zana za uhalifu wa mtandao kama vile programu za kutengeneza picha bandia (deepfake) na programu haribifu za kuiba data zinapatikana kwa wingi kwenye jukwaa hilo.
Ripoti hiyo pia inasema kuwa masoko yasiyo na leseni ya sarafu za kidijitali (unlicensed cryptocurrencies) ambazo hutoa huduma za kutakatisha fedha, hutumiwa sana na makundi ya kihalifu kwenye app ya Telegram.
Tangazo moja lililonukuliwa kwenye ripoti hiyo, lililoandikwa limeandikwa kwa Kichina, lilisema: "Tunahamisha Dola milioni 3 zilizoibiwa kutoka nchi za nje kwa siku."
Aidha, ripoti hiyo ilibainisha kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwa masoko ya data yasiyo rasmi yamehamia Telegram, ambapo wauzaji wa taarifa hizo hulenga zaidi makundi ya kihalifu ya kimataifa yaliyojikita Kusini Mashariki mwa Asia.
Source: CNN