UN yaikana taarifa ya Tanzania kuipigia kura Djibouti, Kenya lazima waisafishe Tanzania

UN yaikana taarifa ya Tanzania kuipigia kura Djibouti, Kenya lazima waisafishe Tanzania

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617
Kuna taarifa kwamba UN imekanusha kwamba hiyo karati inayozunguka mitandaoni sio kweli ni "Fake", ni wazi kwamba hiyo karatasi imetengenezwa na wakenya kama wafanavyo miaka yote kwa lengo baya la kutaka kuipakazia Tanzania.

Kwasababu hii sio Mara ya kwanza wala Mara ya PILI, hii imekua ni mkakati maalum uliopangwa na wakenya ili kuipakazia Tanzania kwa makusudi, ninawaomba watanzania kuwachukulia wakenya kama ni maadui wakubwa wa Tanzania hadi pale watakapo jirejebisha.

Naomba kuwakilisha.

---

- Kenya na Djibouti zilikuwa zinang'ang'ania uanachama katika baraza la Umoja wa Mataifa

- Kenya ilishinda katika mkondo wa kwanza na kura 113 dhidi ya Djibouti 78 lakini kuweka pengo kubwa wakati wa awamu ya pili kwa kura 129 dhidi ya 62

- Duru kutoka Umoja wa Mataifa imebainisha kwamba uchaguzi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ni siri na hivyo matokeo yanayosambaa mtandaoni ni feki


Wakenya kupitia mtandao wa Twitter walikuwa wameonyesha kukerwa na hatua ya mataifa jirani ya Tanzania, Ethiopia na Somali kuwageuka wakati wa kura ya kupata kiti muhimu cha uanachama katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Katika kura hiyo iliyoandaliwa siku ya Jumatano, Juni 14, Kenya ilishinda kura 113 dhidi ya Djibouti iliyopigiwa kura na mataifa 78 katika awamu ya kwanza.


476f996a66c85371.jpg

Japo hakuna aliyeibuka mshindi kwani ziliitajika kura 128 ili kutawazwa mshindi, zoezi hilo liliendelea siku ya Alhamisi, Juni 14, ambapo Kenya iliibuka mshindi kwa kura 129 huku idadi ya kura za Djibouti zikipingua hadi 62.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa katika Kundi la Dharura, Richard Gowan alikanusha matokeo hayo ambayo yalianza kuibika mtandaoni kuanzia Alhamisi, Juni 18 baada ya matokeo rasmi kutangazwa.

"Mjitahadhari na matokeo ya uchaguzi wa UNSC. Kura za UNSC huandaliwa kama siri na huongozwa na Rais wa Bunge la Umoja wa Mataifa kulingana na kipengee cha 83 cha sheria za UNSC," alisema Gowan.

Gowan pia aliweka bayana kuwa wanachama ambao wameorodhoshwa kwenye orodha hiyo sio wanachama wa UNSC.

"Jambo lingine kwa wale wanaghushi matokeo ya UNSC. Kosovo sio mwanachama wa UN," aliongezea Gowan.

Matokeo hayo yalikuwa yamezua ghadhabu miongoni mwa Wakenya huku jambo ambalo liliwashangaza Wakenya zaidi ni kuwa pia China ilikuwa miongoni mwa mataifa ambayo yalipigia Djibouti kura.
 
"Kuna taarifa kwamba" taarifa hizi zinatoka wapi ? Hawa "Wakenya" ambao wanaipakazia nchi yetu katika hili, dawa yao ni ndogo na tuta'waumbua' kwa kushare "link" /chanzo cha taarifa hizi nzuri za kuonyesha unadhifu wa taifa letu adhimu ambazo UN wenyewe wametoa au walau wizara yetu ya mambo ya kigeni kukanusha habari hii yenye lengo la kuifitinisha serikali yetu na taifa ndugu la Kenya.
 
Kwanini hadi UN iseme Kwani serikali ya Tanzania iliyopiga hiyo kura haipo ikanushe. Hizi taarifa zinatuchanganya sana wananchi.
 
"Kuna taarifa kwamba .." taarifa hizi zinatoka wapi ? Hawa "Wakenya" ambao wanaipakazia nchi yetu katika hili, dawa yao ni ndogo na tuta'waumbua' kwa kushare "link" /chanzo cha taarifa hizi nzuri za kuonyesha unadhifu wa taifa letu adhimu ambazo UN wenyewe wametoa au walau wizara yetu ya mambo ya kigeni kukanusha habari hii yenye lengo la kuifitinisha serikali yetu na taifa ndugu la kenya.
Acha hiyo mkuu. Kenya sio Taifa ndugu. Wakenya ni majirani zetu, lakini hatuna kitu in common. Wakenya ni wasanii. Wababaishaji. Watu wa kuomba bomba ma kuandika stories za uongo juu ya mataifa mengine.

Ni wanafiki wa kupindukia. Sasa nafikiri wameumbuka na Story hii.
 
Je, Djibouti siyo Afrika? Ikipata Kenya au Djibouti imepata Afrka - Afrika ni moja! Kenya itasimama kwa niaba ya Afrika kama ilivyokuwa kwa Afrika Kusini. Haitasimama kwa niaba yake yenyewe au Afrika Mashariki.

Vivyo hivyo ingepata Djibouti ingesimama kwa niaba ya Afrika, si Pembe ya Afrika au Djibouti yenyewe!
 
Je, Djibouti siyo Afrika? Ikipata Kenya au Djibouti imepata Afrka - Afrika ni moja! Kenya itasimama kwa niaba ya Afrika kama ilivyokuwa kwa Afrika Kusini. Haitasimama kwa niaba yake yenyewe au Afrika Mashariki.

Vivyo hivyo ingepata Djibouti ingesimama kwa niaba ya Afrika, si Pembe ya Afrika au Djibouti yenyewe!
Wakenya ni wabinafsi sana, Tanzania/Africa tusitarajie kufaidika kwa lolote kwa ushindi wa Kenya
 
Acha hiyo mkuu. Kenya sio Taifa ndugu. Wakenya ni majirani zetu, lakini hatuna kitu in common. Wakenya ni wasanii. Wababaishaji. Watu wa kuomba bomba ma kuandika stories za uongo juu ya mataifa mengine.

Ni wanafiki wa kupindukia. Sasa nafikiri wameumbuka na Story hii.
"Wababaishaji na wasanii" na wenye kila aina hila wameumbuka kwa bandiko lako hili ?, maana wao wameshinda nadhani namna pekee ya "kuwaumbua" ni ushahidi wa hilo bandiko la UN kukana andiko hilo na kutuhumu wa Kenya kwa hilo andiko AU wizara yetu ya mambo ya kigeni kuthibitisha hilo. Hilo litathibitisha haya usemayo kuwa na kweli na hakika na si porojo na stori za kwenye vibanda umiza
 
Back
Top Bottom