Una-deal vipi na matapeli mtandaoni?

Una-deal vipi na matapeli mtandaoni?

jiwe gizani

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2021
Posts
380
Reaction score
507
Aisee Hawa watu wakuitwa matapeli wanakera sana. Wakipiga simu ukiwastukia wanaporomosha matusi yani hadi kwa wazazi wako wao wanatukana tu.

Hivi haya makampuni ya simu yameshindwa kabisa kutulinda sisi wateja wao waaminifu dhidi ya hawa matapeli?
 
Mimi kwangu huwa nikifanya miamala ya kuweka pesa ndo hapo hapo napata sms za ile pesa tuma kwenye no hii na muda mwngne napigiwa sim na hao matapel baada tu ya kuweka pesa hii imeshatokea Mara nyng sana Cha ajab n kuwa hik kpind kifup kilichopita sijaweka mumala wa pesa ndefu karibia Mwezi na sijapata hzo sms ila jana nmeweka 600k hapo hapo zikaanza sms "tuma kwenye no hii" alaf kna mtu nilikua nmeshawasiliana nae nimtumie pesa yan hata kam unajua Kuna utapel unaweza ukajisahau ukatuma kutokana na uharaka walionao baada ya kuweka pesa
 
Ni kuwapuuza ukipokea ukisikia ni wao kata simu achana nailo. Maana kwa yale matusi siku inaharibika kabisa
 
Huwa hakuna tusi jipya...

Atukane awezavyo ila pesa yq dezo ndio kashaikosa..
 
Mimi kwangu huwa nikifanya miamala ya kuweka pesa ndo hapo hapo napata sms za ile pesa tuma kwenye no hii na muda mwngne napigiwa sim na hao matapel baada tu ya kuweka pesa hii imeshatokea Mara nyng sana Cha ajab n kuwa hik kpind kifup kilichopita sijaweka mumala wa pesa ndefu karibia Mwezi na sijapata hzo sms ila jana nmeweka 600k hapo hapo zikaanza sms "tuma kwenye no hii" alaf kna mtu nilikua nmeshawasiliana nae nimtumie pesa yan hata kam unajua Kuna utapel unaweza ukajisahau ukatuma kutokana na uharaka walionao baada ya kuweka pesa
Kweli kabisa unatuma unaliwa. Hii iluwahi kunitokea binti wa kazi alitaka kutuma pesa kwao sasa ikabidi watutumie namba ya kutuma pesa , msg ya kwao na bint inaingia tuma kwa namba hii na jina ninflani na msg ya matapeli ikaingia baada ya dakika tano ikabid tupige kwa bint wa kazi wataje namba na jina ila kama si zilikuaja zote kwa wakati sawa, ingeanza yao tungetuma
 
Wana uwezo mkubwa sana wa ushawishi sijui kwanini hawaingii kwenye marketing industry wakapige pesa huko
 
Kweli kabisa unatuma unaliwa. Hii iluwahi kunitokea binti wa kazi alitaka kutuma pesa kwao sasa ikabidi watutumie namba ya kutuma pesa , msg ya kwao na bint inaingia tuma kwa namba hii na jina ninflani na msg ya matapeli ikaingia baada ya dakika tano ikabid tupige kwa bint wa kazi wataje namba na jina ila kama si zilikuaja zote kwa wakati sawa, ingeanza yao tungetuma
Yaani ukiwasiliana na mtu tu habar za kutuma pesa ukikata sim na sms hapo hapo had unaweza kuhis huwa wanakuskiliza
 
Halafu kila siku kusajili laini kwa vidole, faida yake nini?

Upuuzi.
 
Kuna matapeli wanatumia mtandao wa instagram kutapeli watu wakijifanya wako mtaa wa chakechake, pemba au mtaa wa wete pemba, Wanajifanya kuuza vifaa vya kielektroniki kwa bei nafuu. Wamefungua akaunti mbalimbali instagram na kutapeli watu, wanawaambia watu wawatumie pesa kisha watawatumia mzigo, watu wengi wamekua wakiwaamini na kuwatumia nusu pesa huku ingine wakiambiwa mzigo ukifika, watamalizia nusu ingine. Mpaka sasa wanatumia haya majina, wakibadili mara kwa mara hayo majina: majina ni haya yanayotumika sana ambazo akaunti ziko active:

@vunja_bei_zanzibar2021

@rashidi_electronicss

@home_electronics_zanzibar

@electronics_pemba

@jumla_rejareja_zanzibar

Pia wana majina mengine ambayo kwa sasa wameyafunga, ila muda ukipita na wakiamini zimesahaulika, basi huzirudisha tena hizi akaunti, akaunti ni hizi hapa:

@zanzibar_electronics_og

@apple_dealers_znz

@zanzibar_electronics_og._2021

@mariamu_electronics

@zanzibar_general_suplier_2021

Pia wanatumia hizi namba za simu

0719413986
0758119391
0654031454
0657140183

Washatapeli watu wengi sana na wanaendelea tapeli. Wanajifanya wako pemba ila wako Dar tu na wanaiba picha za vitu mtandaoni na kujifanya ni wao ndio wanauza kwa bei ya chini kabisa. Tahadhari chukueni kama mtu huwajui hao, usitume pesa yeyote.
 
  • Thanks
Reactions: Ilu
Mimi juzi walinipigia. Wakaniambia unaongea na mtoa huduma wako wa Airtel...nikamjibu karibu. Akiniuliza sijui unaongea kutoka wapi? Nikamuuliza wewe si ndio mtoa huduma wangu sasa kwnn unaniuliza tena. Weeee akanitolea bonge moja la tusi ananitukania mama yangu. Duuuh akakta simu.
 
Back
Top Bottom