fimboyaukwaju
JF-Expert Member
- Aug 3, 2020
- 2,977
- 3,798
Mimi kipaji changu ambacho sikitumii kabisa ni kupiga gitaa, hasa hasa gita la solo. Hiki kipaji Mungu alinipa toka utoto wangu,nilianza kwa kupiga madebe, makopo, nikapiga marimba, zeze, ndipo nikawa nawafata wana miziki nawaomba gitaa wananipa na hatimae nikafaulu sana nikawa mpiga mzuri mno.
Nilivyoenfa kusoma nje ya nchi niliendelea kupiga gitaa sana,na nikawa najilipia kozi ndogo ndogo za miziki. Nilipokuwa likizo narudi tz na kaka yangu mmoja alikuwa tajiri na biashara nyingi, basi nikawa namsaidia kazi zake na alinipenda sana,kila akisafiri anasafiri nami ili nimsaidie kazi.
Siku moja tukaenda Mwanza tukakaa Mwanza Hotel, jumamosi huwa na dinner and dance, kuliliwa na residence band,ambayo mida ya mchana huwa wanafanya mazoezi, nami siku moja nikaenda nikaomba kufanya nao mazoezi, wakanipa gitaa na nilipiga vizuri sana na nikawa rafiki yao sana.
Siku moja mpiga solo wao akaugua ghafla akiwa jukwaani na watu wamejaa na mimi na kaka yangu tupo hapo, basi wakaja kuniomba nikapanda jukwaani nikalikung'uta gitaa la solo vizuri hadi saa 8 ndipo nikaenda kulala.
Kaka yangu alishangaa kabisa.Siku nyingine ntapa stori nikampigia solo marehemu king kikii.