LGE2024 Una maoni gani kuhusu zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024?

LGE2024 Una maoni gani kuhusu zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa 2024 Lakamilika: Je, Wananchi Wanasemaje?

Mnamo Oktoba 20, 2024, zoezi la Uandikishaji wa Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa limekamilika rasmi Tanzania. Zoezi hili muhimu ni hatua ya kwanza kuelekea uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu, ambapo Watanzania watachagua viongozi wao wa ngazi za vijiji, mitaa, na vitongoji.

Hadi kufikia hatua hii, tumeona mwitikio tofauti kutoka kwa wananchi. Wapo waliojitokeza kwa wingi kuhakikisha majina yao yanapatikana kwenye daftari la wapiga kura, lakini pia wapo wanaoonesha shaka juu ya mchakato wa uchaguzi na wameeleza wasiwasi wao kuhusu uaminifu na uwazi wa zoezi zima la uchaguzi.

Wananchi Wanasemaje?

1. Kuhamasishwa kwa Uandikishaji – Baadhi ya wananchi wamepongeza jitihada za Serikali, Tume ya Uchaguzi, na wadau wengine katika kuwahamasisha watu kushiriki kwenye zoezi la uandikishaji. Wananchi wengi wamejitokeza kutokana na mwamko ulioletwa kupitia kampeni za uhamasishaji, ikiwemo kwenye vyombo vya habari na majukwaa ya mitandao ya kijamii.

2. Wasiwasi wa Usimamizi wa Uchaguzi – Wengine wameonyesha wasiwasi kuhusu usimamizi wa uchaguzi. Kuna hofu juu ya uwezekano wa kuwepo kwa udanganyifu na mbinu zisizo halali ambazo zinaweza kuathiri uchaguzi. Hivyo, wameitaka Tume ya Uchaguzi kuzingatia uadilifu na uwazi katika usimamizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili matokeo yawakilishe matakwa ya wananchi.

3. Umuhimu wa Ushiriki wa Kila Mwananchi – Wengi wamezungumzia umuhimu wa wananchi wote kushiriki kwa sababu uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaathiri maisha yao ya kila siku kwa karibu. Wananchi wamehimizana kuhakikisha wanawachagua viongozi wanaowaamini na wanaoweza kutatua changamoto za maendeleo katika maeneo yao.

Ushiriki wa wananchi kwenye uandikishaji na uchaguzi ni hatua muhimu kwa ajili ya kuimarisha demokrasia na maendeleo katika ngazi ya jamii. Sasa macho yote yameelekezwa Desemba 2024, wakati ambapo wananchi watatekeleza haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wao.

Unadhani uchaguzi huu utaathiri vipi maisha yako na jamii yako? Tupe maoni yako!

#UchaguziSerikalizaMitaa2024 #SautiYaMwananchi #JamiiForums
 
Zoezi la uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024? Limeenda salama kabisa tena kwa mafanikio makubwa, Imani yangu ni kuwa zoezi la uchaguzi litaenda vizuri na haki itatendeka.

Nampongeza sana Rais wetu Mama Samia kwa kuendesha zoezi hili kwa mafanikio makubwa.
 
Tungeachana tu na uchaguzi hizo hela zifanye maendeleo. Dunia inatushangaa jinsi ambavyo tunaendesha mambo yetu. Yaani chama tawala ndio kinaratibu na kusimamia uchaguzi halafu tunaona ni sawa kabisa, tunategemea free and fair election!

Inabidi hili liwekwe kwenye maajabu ya dunia.
 
Pamoja na Mapungufu mengi lakini zoezi limefanyika kwa amani kwa sehemu kubwa, na nakuhakikishia kwamba uchaguzi wake hautatabirika

Hii ni kwa sababu, Hata wale waliohamasisha kwa nguvu kubwa watu wajiandikishe ili wapate mtaji wa kura Wameangushwa vibaya sana kwenye kura za Maoni, Kwa mfano huku kwetu Tandika Mwembe Yanga aliyekuwa kinara wa Uhamasishaji ambaye alidhani anahamasisha ili apate watu wa kumpigia kura ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, ambaye aliomba tena ridhaa hiyo, lakini cha kushangaza ameangushwa vibaya mno kwenye kura za maoni.

Sasa haya yaweza kutokea sana kwenye uchaguzi wenyewe
 
Kutokana na ukiukwaji mkubwa wa kanuni katika zoezi la uandikishaji wapiga kura naamini hata uchaguzi wenyewe utakuwa hauna maana yoyote zaidi ya kupoteza pesa na kuwapotezea muda tu wananchi na sioni kama uchaguzi huu utaleta matokeo halisi kulingana na wananchi watavyochagua viongozi wanaowataka.

Bora muundo huu wa viongozi wa mitaa ungerekebishwa ili wawepo watendaji wa mitaa tu na viongozi wa kuchaguliwa waanzie ngazi ya kata ili kuokoa pesa zinazopotea bure kwa uchaguzi feki.

Kule Zanzibar wana mfumo huo wao watendaji wa mitaa wanawaita masheha/sheha.
 
Back
Top Bottom