Una matatizo ambayo yanakusumbua lakini hujui wapi pa kuanzia kuyatatua?

Una matatizo ambayo yanakusumbua lakini hujui wapi pa kuanzia kuyatatua?

Joined
Apr 19, 2018
Posts
83
Reaction score
115
UNA MATATIZO AMBAYO YANAKUSUMBUA LAKINI HUJUI WAPI PA KUANZIA KUYATATUA?

JE, unafikiri ni nani wa kulaumiwa kwa changamoto na matatizo yote unayopitia? Ni mzazi, mlezi, Ndugu, Jamii au serikali yetu?

Na Je, unajua kuwa kusuluhisha tatizo lolote lile bila kujua chanzo chake, ni kama kushindana na mti kwa kupukutisha matunda bila kushughulikia mizizi, shina na matawi yake? Zoezi lako litafanikiwa kwa msimu mmoja tu, lakini jiandae; kwa sababu matatizo hayo (matunda) yatarudi tena mwakani, na mwaka ujao, na mwaka mwingine na mwingine mpaka pale utakapoamua kuyatatua matatizo yako kwa njia iliyo sahihi. Yaani; ung`oe mizizi, shina na matawi yake yote; lakini pia uzitambue mbegu zake na kuziondosha kabisa kwenye eneo lako.

Nakukaribisha “Life Mindsets” ulimwengu wa Saikolojia, uchumi, Afya na Elimu; ambako tutajifunza mambo mbalimbali kuanzia katika ngazi ya mtu binafsi, kwenda katika familia mpaka kwa jamii inayutuzunguka, mambo ambayo yanaathiri jinsi tunavyofikiri, tunavyofanya maamuzi, tunavyo tenda, mafanikio yetu na Tabia zetu kwa ujumla.

Lakini pia tutajifunza ni jinsi gani mambo hayo yanaathiri Afya zetu na uchumi wetu kwa kiasi kikubwa.

INAENDELEA!
 
Haya graduates ambao hamjapata ajira uzi huu mahususi kwajili yenu..wekeni kambi mpate kujifunza.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, ebu usilete siasa kwenye maisha ya watu tafadhali.

Tuna vijana wengi wanaumia huku mtaani, alafu unatuletea hadhithi za isidingo....☹️😬
 
Ukiona ubabembelezewa fursa jua wewe ndiye fursa!
Vijana jiajirini achaneni na hayo maporojo mnapoteza muda

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakati mwingine mtazamo wako unaweza kukuharibia, unapokiangalia kioo unaona taswira mbaya, usikilaumu kioo, unapoona taswira ya kutisha kwenye kioo usikitukane kioo, utakuwa unakosea. Mtazamo wako juu ya dunia na jamii inayokuzunguka, mara nyingi huitengeneza taswira hiyo hiyo ya "Mtazamo wako".

Kama huamini vaa kinyago na kisha jiangalie kwenye kioo, utajua kama sura yako ile iliyokuwa nzuri utaiona au la!
 
OP

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom