Una moyo mwepesi lakini huachi kumfuatilia Mwenza wako, hatuna hela ya rambi rambi zako

Una moyo mwepesi lakini huachi kumfuatilia Mwenza wako, hatuna hela ya rambi rambi zako

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
Mhadhara - 41:
Una moyo mwepesi na mlaini kama karatasi la kufungia maandazi, lakini huachi tabia yako ya kumfuatilia mpenzi/mume/mke wako. Shauri yako, one day tutakuzika kwasababu ya kufumania.

1. Ukikata kitunguu huachi kutoa machozi, lakini kutwa unapekua simu ya mwenzako. Shauri yako.

2. Ukipita kwenye moshi wa majani mabichi unatoa machozi mengi, lakini kutwa unafuatilia nyendo za Mwenza wako. Shauri yako.

3. Ukimenya chungwa kwa mkono unatiririka machozi, lakini kutwa unawauliza marafiki wa Mwenza wako kuhusu tabia ya Mwenza wako. Shauri yako.

"Mwana kulifind mwana kuliget" - Siku moja utamkuta Mwenza wako amekunjwa kama kuku aliyebanikwa kwenye moto. Au amemkunja mtu kama kware aliyebanikwa motoni. Kwa huo moyo wako ulivyo mwepesi na mlaini utaanguka kama gunia "Paaaaaa!" - bila shaka tutakwenda kukuzika.

Acha kumfuatilia Mwenza wako, subiri wakati sahihi ambao Mungu wako atakuonyesha tabia ya mtu wako huku akikupa ujasiri wa kustahimili. Kama si Mungu basi hata shetani anayemtafutia Mwenza wako michepuko, siku moja atakuonyesha maovu ya mtu wako.

Right Marker
Dar es salaam
 
Modern women ambao karibia wote ni wana sifa ya umalaya wanapenda sana aina hii ya wanaume kama wanaotajwa kwenye uzi

Usijihisi insecure kufuatilia nyendo za mwanamke/mke wako

Miaka hii kauli za modern women zimewafanya wanaume wajinga wapotezee nyendo za wake zao. Utamsikia mwanamke akimwambia mwanaume wake

"Don't you trust me?"
Anamaanisha: You're a fool, so you ought to trust me

"You're insecure"
Anamaanisha: I cheated on you, and so?

Mwanaume bwege akiambiwa hivyo anaamua kupotezea. Acha ujinga wewe ni vizuri kujua mwenendo wa mwanamke wako utajiepusha na mengi.

Wakati wa Mungu ni sasa
 
Back
Top Bottom