Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Fahamu mambo ambayo huruhusiwi kuyafanya unapotembelea Dubai
1. Ingawa Dubai ni kitovu cha mitindo, hauruhusiwi kuvaa Nguo fupi, zinazobana sana, au zenye kufichua Mwili kwa kiasi kikubwa katika maeneo ya Umma. Hakikisha unavaa Mavazi yanayofunika Mabega na Magoti unapokuwa hadharani
2. Pia, hairuhusiwi kuonesha Vitendo vya Kimapenzi hadharani. Kushikana Mikono, Kubusu, au Kukumbatiana ni kosa linaloweza kusababisha kutozwa faini au hata kukamatwa.
3. Heshimu Tamaduni za Kiislamu. Kwa mfano, katika Mwezi mtukufu wa Ramadan, ingawa si lazima kwa wasio Waislamu kufunga, ni vyema kuepuka kula, kunywa (hata Maji), kutafuna chingamu (bubble gum), au kuvuta sigara hadharani wakati wa mchana.
4. Kuwapiga Watu picha ni suala nyeti katika Tamaduni za eneo hilo. Epuka kupiga picha za Watu, hasa Wanawake na Watoto, bila ruhusa yao. Pia, ni kinyume cha sheria kupiga Picha au Video za Watu bila idhini yao na kuzichapisha kwenye Mitandao ya Kijamii.